Ndugu waislam wenzangu, hongereni kwa kuisafisha CHADEMA kuwa si chama cha vurugu!

Status
Not open for further replies.
Wewe raia na Mkristu kinachokuwasha kipi ikiwa Waislaam wanaandamana kuishinikiza serikali kuwaacha huru watu wake?. Ni wapi uliwahi kuona kibali kinatolewa kwa watu wanaitaka serikali kuwaachia huru wafungwa?. Hivi unaweza kunambia waandishi wa habari wanaweza kuomba kibali kulaani kifo cha mwandishi mwenzao?..
Mkuu wangu hujui Harakati za Waislaam na pengine mngejua tusingekuwa tukitawaliwa na CCM hadi leo. I thought nilikuwa Chadema the right party kinachopigania haki za wananchi wake, sasa naanza kufikiria tofauti.


Mkuu Mkandara heshima mbele...
wewe ni mmoja kati ya watu ninaoheshimu michango yao hapa JF.
Kwa heshima ulionayo please nakuomba uachane na huu mjadala.

Migongano ya kidini ni hatari sana Kaka.
Plz nakusihi Kaka.
 
Mkuu Mkandara heshima mbele...
wewe ni mmoja kati ya watu ninaoheshimu michango yao hapa JF.
Kwa heshima ulionayo please nakuomba uachane na huu mjadala.

Migongano ya kidini ni hatari sana Kaka.
Plz nakusihi Kaka.
Kama utanisoma vizuri siku zote naingia mijadala hii kwa kuwatahadharisha ubaya wa mijadala hii. Na siku zote nitaisimamia haki ilipo hata kama itaniweka pabaya maana kinachotakiwa ni ELIMU ya URAIA ambayo wengi wa hawa watu hawana isipokuwa Udini na Umimi..Hivyo huuingia ktk mioyo yao kuwaonyesha wapi wanapokosea na nini athari zake.
 
Tafsiri ya viongozi wa serikali hii juu ya maandamano ya CHADEMA imekuwa ni chama cha vurugu na kinachovunja amani! Je Police hawa na viongozi wanasemaje juu ya maandamano ya Amani ya waislam, je wanaweza thubutu kusema uislam ni dini ya vurugu kwasababu imefanya maandamano tena yasiyokuwa na kibali? Je wanasemaje juu watu kutokupigwa, kujeruhiwa au kuuwawa? Je hii haithibitishi kwa wazi kabisa police waliotumwa ndo huwa wanasababisha uvunjifu wa amani na utulivu wanapoingilia maandamano ya amani wa wafuasi wa CHADEMA? Asanteni ndugu zangu waislam kwa kuwaaibisha wauaji!

Mkuu ulichoandika hata mimi nakubaliana nacho na wamejaribu kuwafungua macho waTz waliokuwa bado hawaamini kama yote hayo yalikuwa yakisababishwa na polic na si CDM na serikali ya ccm imeumbuka ndanh ya riku chache na malipo ndo tunasubiri sasa
 
We pad acha urongo na fikra potof za kua na chuki na waislam..sasa kama viongozi wa kiislam ndo walituma polic kuua raia je yale mauaji ya mwembechai nani aliwatuma askari??hao waliotuma askar kuua waislam wasiokua na hatia mwembechai ndo haohao waliotumwa kwenye maandamano ya chama cha kanisa!!

Chama cha kanisa ndo kipi?
 
Dini zimeoa fikra ya mtanzania masikini tz yangi wanaosema dini ni bange ya fikra hawakesei.
 
Mkuu, nilikuwa kijijini, ndio nimerudi leo. Wawza kubandika humu hiyo kau;li ya aislamu ili niweze kuchangia nikijuacho

Waislam waliandamana kuishinikiza serikali iwaachilia huru waislam waliokataa kuhesabiwa kwenye sensa na waliachiliwa huru! Waliandamana kwa maelfu bila kibali hafi wizara ya mambo ya ndani!
 
mleta mada umekurupuka, waislam hawakufanya maandamano ili kukisafisha wala kukichafua chama chochote.
Uislam unajitosheleza na unajitegemea wenyewe, hauihitaji support ya chama chochote hivyo hauna haja ya ktmsafisha au kumchafua mtu.
Tunachodai waislam ni dhulma na unyanyasaji unaofanya dhidi yetu ukomeshwe.
Tumedhulumiwa na kuonewa vya kutosha, muda umefika wa kuondosha dhulma na kusimamisha haki.
Hayo ya kusafisha au kuchafua chama fulani hayahusiani na waislamu na madai yao.

Wewe ndo umekurupuka, sikusema mliandamana kuisafisha CHADEMA! ila maandamano yenu yametoa tafsiri kuwa kuandsmana si vurugu wala kuvunja amani, lakini pia imeonesha maandamano yasipoingiliwa na police hayawezi kuvuruga amani! Police ndo huwa wanavunja amani!
 
Wewe ndo umekurupuka, sikusema mliandamana kuisafisha CHADEMA! ila maandamano yenu yametoa tafsiri kuwa kuandsmana si vurugu wala kuvunja amani, lakini pia imeonesha maandamano yasipoingiliwa na police hayawezi kuvuruga amani! Police ndo huwa wanavunja amani!

haujanielewa, tatizo umetoa pongezi kwa jambo ambalo hatukulifanya wala hatujawahi kulifanya.
Ungesema maandamano ya jana yameisafisha chadema na sio kusema Ndugu waislam wenzangu, hongereni kwa kuisafisha CHADEMA kwakuwa hawakufanya hivyo.
Umetupa sifa na shukrani tusizostahili.
 
-Umefukua thread.
-Umesoma mwanzo tu.
-Hukuelewa mantiki ya mleta thread.
-Umekurupuka kuchangia.
My Take:
HUU NI UKILAZA.
Eliah G Kamwela says sorry for this very kilazaful post.


haujanielewa, tatizo mleta mada ametoa pongezi kwa jambo ambalo hatukulifanya wala hatujawahi kulifanya.
Angesema maandamano ya jana yameisafisha chadema na sio kusema Ndugu waislam wenzangu, hongereni kwa kuisafisha CHADEMA kwakuwa hawakufanya hivyo.
Ametupa sifa na shukrani tusizostahili.

Hayo ya ukilaza naomba nisikujibu, ila Sihitaji uombe radhi kwa ajili yangu kwani nikikosea nitaomba mwenyewe manake ndio uungwana na ndivyo imani yangu inavyo nifunza.
 
Hapo kwenye red ndipo panapoacha maswali. Anza wewe kuweka ushahidi hapa, ukiwa kama muislamu, umeshawahi kupoteza au kunyimwa haki yako ipi kwa kigezo cha uislamu wako??? Toa mfano 1 tu wa kwako binafsi nikusaidie mkuu.

Ushahidi upo mwingi sana na mtu yeyote makini anauona na kuuelewa, kuanzia mauaji ya mwembe chai mapaka uchakachuaji wa matokeo unaofanywa na necta.
Binafsi nimeshafanyiwa vitimbizaidi ya mara 3 wakati nasoma sekondari kutokana na imani yangu.
Sina sababu ya kukutajia kwasababu yameshapita na kwa sasa hauwezi kunisaidia.
Kikubwa ni kila mtu kama raia wa tz atimize wajibu wake bila upendeleo wala uonevu na aheshimu imani ya mwingine, tukifanya hivyo tutakuwa na amani na mshikamano kama taifa.
Kinyume chake ni maafa na machafuko.
 
kawaeleze kina nape na ccm mliowapa kura.wawape mnachotaka .hapa unatokoraga tuu .sisi hapa tunapigania haki kwa watanzania wote .
sikueleza ili kutaka msaada wa yeyote, uislamu unajitosheleza na wala hauhitaji nyongeza. Hakuna uhusiano kati ya uislamu na ccm, ingekuwa hivyo wangeweka kipengele cha dini kwenye sensa na madai yetu mengine wangetekeleza, halafu unapaswa uelewe Haki ktk jamii haiwezi kuja ikiwa kuna kundi linadhulumiwa. Huko ni kujidnganya.
 
Huu ni ujinga unaoendelea hapa. CCM wanataka kusababisha kutokuelewana kati ya chama cha CHADEMA na waumini wa dini ya kiislamu ambao wengi wao ni wanachama safi wa CHADEMA. Hali ya kuandamana ni haki ya msingi.
 
Ushahidi upo mwingi sana na mtu yeyote makini anauona na kuuelewa, kuanzia mauaji ya mwembe chai mapaka uchakachuaji wa matokeo unaofanywa na necta.
Binafsi nimeshafanyiwa vitimbizaidi ya mara 3 wakati nasoma sekondari kutokana na imani yangu.
Sina sababu ya kukutajia kwasababu yameshapita na kwa sasa hauwezi kunisaidia.
Kikubwa ni kila mtu kama raia wa tz atimize wajibu wake bila upendeleo wala uonevu na aheshimu imani ya mwingine, tukifanya hivyo tutakuwa na amani na mshikamano kama taifa.
Kinyume chake ni maafa na machafuko.

Huna hoja. Matokeo ya NECTA kwa taarifa yako huchakachuliwa yanapofika kwenye halmashauri. Kila mtihani husahihishwa kwa NAMBA na hakuna anayejua nani ni nani. Kuwa mtafiti zaidi alafu tumia zaidi akili yako kuangalia mambo.
 
Kiasi flani napata matumaini kwa wale waelewa wanaochangia mijadala kwa amani

Nimepitia uzi huu huku mwishoni nimeona majibizano ya hekima kiasi flani.

Tulumbane kwa amani. Matusi, dharau, kejeri na kashifa hazijengi, sana sana hutugawa na kututenganisha.

Lugha nzuri, ujumbe wa hekima na kujibizana kwa kujenga hoja huku tukiheshimiana kwa pamoja ni kuutukuza ummoja na utanzania wetu.

Tuheshimu imani ya kila mmoja wetu kwa manufaa yetu sote. Inshallah tutaipata amani.
 
Kiasi flani napata matumaini kwa wale waelewa wanaochangia mijadala kwa amani

Nimepitia uzi huu huku mwishoni nimeona majibizano ya hekima kiasi flani.

Tulumbane kwa amani. Matusi, dharau, kejeri na kashifa hazijengi, sana sana hutugawa na kututenganisha.

Lugha nzuri, ujumbe wa hekima na kujibizana kwa kujenga hoja huku tukiheshimiana kwa pamoja ni kuutukuza ummoja na utanzania wetu.

Tuheshimu imani ya kila mmoja wetu kwa manufaa yetu sote. Inshallah tutaipata amani.

Mkuu, umeongea vizuri sana, na umeongea mawazo yangu kabisa. Nilitaka kumwambia PERI kuwa ameonesha ustahimilivu na weledi wa hali ya juu kujibu hoja na maswali bila kutoa tusi wala kejeli kwa mtu. Huu ni uungwana wa hali ya juu.

Pili mkuu, mm binafsi hoja za kidini huwa zinanisononesha sana, kwani ushabiki huu si mzuri na ukizingatia wengi sisi tumezaliwa na wazazi wa dini zote, siwezi kuikana kweli na kumdharau Mama yangu ambae ni Muislam au Baba yangu ambae ni Mkristo!

Tatu, mleta mada nimemwelewa sana ila tafsiri ya wachangiaji baadhi naona ndo shida kidogo. Nathubutu kusema kuwa, Maandamano ya Ndugu zangu Waislamu ile juzi yamedhihirisha umma kuwa Polisi ndo chanzo cha vurugu katika maandamano na mukutano mingi.

Mungu Bariki Tanzania kwa kuiondoa CCM madarakani!
 
Kama waislam hawakuwa na kibali nawakafanya maandamano ya amani nawapongeza wao na polisi kwani kimsingi raia hawahitaji kibali bali ulinzi ili kuandamana.Mambo ya kibali ni hofu ya watawala tu kutaka kupora haki za raia.Mimi ni mkristo na siamini kuwa viongozi wa waislam ndio wamekuwa wakiwatuma polisi ili kufanya mauaji mikutano ya CDM.Wenyewe pia ni waathirika wa uonevu wa polisi kama vile mauaji ya mwembechai na vurugu za kule Unguja hivi karibuni.Kimsingi, polisi walihofu kuendeleza chuki dhidi yao baada ya mauaji ya Iringa hivi majuzi. mikutano ya CDM kwa mazishi ya Arusha, na M4C Mtwara na Lindi ilikuwa ya amani kama maandamano ya waislam Ijumaa, kwasababu tu polisi na watawala wao waliacha kuingilia kati na kuanzisha vurugu ambazo huishia kumwaga damu.
Kama tunaipenda nchi yetu, tuupende ukweli.ASmani ya jirani inapoondoka, yako pia iko hatarinibila ya kujali nani anaathirika kwanza.Hongera waislam kwa kuthubutu,hongera wapenda amani kwa kuweza kuidumisha,hakika wapenda haki tutasonga mbele.
 
Watanzania hawana maandamano ya Vurugu. Ni Rushwa tu kwa mapolisi ndio inaleta Tatizo. Yaani CCM na Rushwa zao, kwa kuogopa M4C.
 
Ni lini mtawaacha Waislaam peke yao?. Hivi kweli mtu mwenye akili zake timamu anaweza kulinganisha swala la Chadema na Maandamano ya jana?.. Swala la Chadema kwanza halikuwa maandamano isipokuwa Mkutano ambao wao walikatazwa kufungua tawi la Chama kupisha usimamizi wa zoezi la sensa.. Kesi yao itatazamwa tofauti na jinsi gani polisi walitumia nguvu za ziada na sio kuchukua mfano wa maandamano ya Waislaam ilihali mnaonyesha chuki zenu wenyewe kwa waislaam.



Chadema mkiendelea na propaganda hizi za kuonyesha serikali na Uislaam basi nina hakika uchaguzi wa mwaka 2015 msahau USHINDI na dalili zitaanza kuonekana soon. CCM imefanikiw akw akiasi kikubwa sana kuwajaza Ujinga na mmeuvaa vizuri sana. Chadema Mnajimaliza wenyewe..

Tunajua sana mlichukia waislaam kutoshiriki sensa yenye kutukuza Ujinga mtupu. Sensa ambayo inahesabu vichwa vya watu wakati hatuna database ya kufananisha hesabu hiyo na records tulizokuwa nazo. Sensa ambayo kwa msomi yeyote atakwambia haiwezi kuwa na mafao yoyote kwa wananchi kwa sababu sii wingi wa watu au uchache wa watu ndio huiwezesha serikali kupanga maendeleo isipokuwa kutambua jamii nzima ktk makundi yao. Iwe Immigrants wangapi, raia wangapi, wanawake wangapi, watoto wangai, wazee wangapi na kadhalika na ktk sehemu zao za makazi na uzalishaji...Kukosekana kwa data kamili ni sawa na ahadi tupu ambaz hazitaweza kumsaidia Mtanzania kwa lolote na mtakuja nambia..
Mimi sina tatizo na waislamu kugomea sensa, kwa sababu walikuwa na maelezo ambayo ni muhimu. lakini sikubaliani na Polisi kuzuia CDM kufungua matawi. Hapo hawana haki wala sababu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom