Ndugu wa Tanzania Mnakielewa chanzo cha Misukosuko ya Nchi? (Ali H. Mwinyi)

Bintimkonge asante kwa kufafanua, ni kweli kabisa Tanzania haikuwa nchi pekee iliyokuwa na uhaba wa bidhaa enzi zile. Hata wenzetu wa Zambia ambao walionekana kuwa na unaffuu (kama mnakumbuka zile sabuni muruwa za bafuni kutoka Zambia enzi hizo) walitamba kwa siku chache tu kabla ya 'new international economic order' kuwakumbatia! Naamini kabisa ni kosa kufikiri kwamba matatizo/mafanikio ya uchumi kwa nyakati fulani yanawiana na sera binafsi za kiongozi fulani. Nionavyo Nyerere angekuwa ni kiongozi wa awamu ya tatu, ukuzi uchumi ungaliweza kuwafaidi wengi zaidi kuliko ilivyokuwa.

Dhana nninayoilaani kwa nguvu zote ni hii ya umimi au uyeye katika maendeleo ya taifa. Inavunja nguvu za wale wanaopenda kujenga. Tukiamini kuwa sio rais na wala nani tuliyemchagua anaweza kubadili mwenendo wetu wa maendeleo, tunajiwekea uwigo mkubwa wa maendeleo. Sharti ni moja tu hao viongozi wawe kweli ni matunda ya demokrasia ili wasimamie yale tunayoyataka, sio wao wajisemee eti uwazi na ukweli wakati sisi tunaamini tofauti, au ari mpya maisha bora wakati hata hatung'amua tuko na ari gani. Naamini ni dhambi kupachika majina ya viongozi kwa miradi mbalimbali, mara eti ni Daraja la sijui Mkapa(wapi na wapi jamaini Mkapa hajaanza uwaziri, watu walikuwa wanajadili ujenzi huo), Sijui BWMkapa Towers badala ya Mafuta House hali mradi huo ulikuwepo tangu miaka ya 1970 ikawa imecheleweshwa na Kumekucha Auction Mart kama wapangaji, na mradi ukaanza kwa mikiki kabla ya 1995. Tusiwape sifa watu bila sababu
 
Naona taratibu unaanza kuachia au sivyo? Sawa umeshakubali kuwa ufisadi ulikuwepo, sasa na tuangalie huo uamuzi mgumu na mkali aliofanya Nyerere ulisaidia kiasi gani kwa maendeleo ya Tanzania? Ni kweli tulishuhudia Nyerere akitowa hutuba kali lakini hebu tujiulize nani mwenye uwezo na nafasi nzuri ya kufisadi? Sasa natujiulize wakati wake Kigogo gani tuliona akichukuliwa hatuwa za mfano kama wakati huu? Jambo jengine ni kujiuliza!Nyerere na ukali wake aliweza kuliokowa Taifa na kufilisika kulikosababishwa na ufisadi?

huyo kaisha eleke kunapotakia anaonge kwa kumtetea nyerere

ufisadi ulikuwepo toka kwa huyo jamaa pia mtoto hupatikana baada ya kutunga mimba halafu kuzaliwa na kuanza kukua

kwa sasa ufisadi ni mkuwa saana angalai mafisadi waliotajwa awamu hii wametokea awamu ipi?
 
Sikiliza bwana we! Nyerere alikuwa mtu anayechukua maamuzi magumu. Waliokuwa wakijaribu kufanya hivyo walifanya kwa woga sana na alipowagundua aliwashughulikia kikweli.
Watu walifikia mahala wanajenga nyumba kwa majina ya marafiki zao. Wanafungua biashara kwa majina ya jamaa zao tu, kama ilivyofanywa kwa wakina Gachuma.
Sio hawa wanaomuuliza Mr President "wewe umeshatengeneza shiling ngapi toka uingie madarakani?"

HAyo maamuzu magumu mugumu yametusaidia nini?

Na nani alishgulikia? na faida yake

kujenga majumba na kuweka jina la mwezako ilikuwa ni uwoga wakati wa hujumu uchumi lakini kijana sasa hivi toka alipoachi madaraka nyerere nani atakaye kusumbua ukiweka jula lako ukijenga nyumba hata tatu
 
Binafsi mimi ninadhani kuwa pamoja na udhaifu wake wa kutokuwa madhubuti kiongozi, Mwinyi alijenga msingi mkubwa sana wa demokrasi kwa kutumia ile filosofi yake ya RUKSA. Ninachomlaumu zaidi ni pale alipotumia filosofi hiyo kukubali uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi vya siasa bila kujenga level ground kwa vyama hivyo; matokeo yake Tanzania imekuwa na vyama dhaifu hadi leo kwa vile chini ya mfumo uliokuwapo wa Chama Kushika Hatamu, CCM ilikuwa na raslimali nyingi sana za kitaifa tofauti na kwa majirani zetu wa Kenya, Zambia na Malawi ambako hawakuwa na hizo sera za Chama kushika Hatamu.
 
Sasa wewe ulitaka wakati nchi inakosa mapato kutokana na wahujumu wa uchumi kuhodhi bidhaa adimu zikiwemo vyakula na kuikosesha Serikali mapato chungu nzima kiasi ambacho cha kukaribia kushindwa kujiendesha, ulitaka tuagize sabuni za manukato au vitu vya anasa! na wewe hayo unayaona ni maendeleo! Kweli vipaumbele vyako vimekaa kushoto sana. Wakati wa Nyerere hakukuwa na viongozi wenye uroho wa utajiri wa haraka haraka kama tunavyoona leo ambao wanatumia nafasi zao kuifisadi nchi kwa mabilioni ya fedha na kuziweka nchi za nje. Nchi iache kuagiza chakula na madawa bali iagize sabuni za manukato! unachekesha kweli! Ungekula sabuni za manukato kama ungekuwa huna chakula?


Sadakta Bwana Mkubwa, Hakukukuwa na viongozi waroho Sasa nani alitafuna vyama vya Ushirika? Nani alishusha uzalishaji wa mashamba makubwa? Nani aliviondowa Viwanda? Hivyo umasikini uliokuwepo katika MIAKA YA 1980 ULIKUWEPO WAKATI TUKIPATA UHURU?
Kuhusu hili la kurapa na uchaguzi wa bidhaa nahisi wewe ni Bwana mdogo hukuonana huo wakati. Kwa kweli kulikuwa hakuna uchaguzi si bidhaa muhimu si anasa zilizokuwepo wakati huo. Pengine ungewauliza wakubwa wako nini maduka ya RTC?
 
Ndiyo nyie ambao mnasimama na kumtetea mwinyi kwa sababu tu ni muislamu mwenzenu na wengine mkidai eti wakristo wanataka kumweka mkristo mwenzao ndiyo maana wanampiga vita Kikwete! Kwa maana nyingine mnaridhika na utendaji ZERO wa Kikwete kwa kuwa tu ni muislamu mwenzenu! Nyerere alipendelea wakristo wenzake. Makubwa haya!


Alaa kumbe ni wale wa kiwaraka waraka. Bora usipoteze wakati wetu nenda kwenye uwanja wa dini ukamwage !
 
Black Jesus unaufahamu msemo wa 'Shukurani za Punda mateke?' Basi ndio baadhi yenu nyinyi.

Enzi zile kila kitu ilikuwa foleni foleni foleni - sabuni ya mawingu kwa foleni, vitenge TZ yote inavaa aina moja nayo ni kwa foleni. Watu walifikia hata kuvaa mifuko ya unga ngano (enzi zile mifuko ya kg 50 ilikuwa ya vitambaa), kuwa na TV au friji ni haramu, gari kuendesha mwisho saa nane mchana siku za jpili, kuwa na dola za kimarekani au foreign currency yo yote ni uhaini.

Sera ya ujamaa na kujitegemea ni nzuri kinadharia lakini kiuhalisia haifanyi kazi. Na huo ni ukweli nyinyi vijana wa leo mubaki kuimba tu na kukumbuka mabaya badala ya kushukuru kwa yale maendeleo yaliyofanyika kwa kubadilisha sera zile.

You are taking too many things for granted.
Kwani enzi hizo wangapi walikufa njaa? kutugeuza gulio la waarabu wachina na wazungu ndo solution. kufanywa gulio au ili la sasa la kuwaleta wazungu wachukue mali zetu si maamuzi yanayoitaji akili.Ni maamuzi ya kichovi ambayo yataturudisha tu kwenye utumwa.
 
Zhule wacha kujidanganya kwamba umegeuzwa gulio la waarabu na wachina. Ni wewe mwenyewe ndio umetaka kugeuzwa gulio. Nani anasaini mikataba mibovu kwa tamaa ya kupata commission? Na nani anawapa wahindi akina Patel na wenzake hizo tender ili wapate chao? Ni sisi wenyewe ngozi nyeusi watanzania wazawa. Hakuna mchina wala muhindi aliyekulazimisha usaini mikataba mibovu kwa njaa yako, au utoe tenda kwa tamaa ya kuwekewa kwenye account huko nje.

Amka ndugu amka jichunguze wewe kwanza kabla ya kulaumu wenzako.
 
Wewe binti mkongwe umeamua kuandika uwongo, nami sitauruhusu uwongo huu ubaki kama ulivyo. Si kweli kwamba ilikuwa haramu kuwa na TV au friji. Binafsi nawafahamu Watanzania wengi waliokuwa na TV enzi za Mwalimu na walikuwa wanaangalia station ya Zenj au Kenya kwa wale walio kaskazini. Kulikuwa na makampuni kama DABCO na RTC ambayo yalikuwa yanauza friji.

Mwaka 73 kulitokea matatizo makubwa ya upatikanaji wa Petroli na hii ilisababisha bei ya petroli duniani kupanda kwa kasi sana na hata nchi za magharibi ziliathirika sana. Nakumbuka US kulikuwa na foleni za kutisha za wenye magari wakisubiri petroli kwa masaa chungu nzima na halii hii pamoja na uchumi kuanguka kutokana na athari za bei ya mafuta na kuwa adimu kulisababisha Jimmy Carter akae madarakani kwa kipindi kimoja tu.

Kutokana na matatizo hayo ya mafuta Serikali ikaamua kubana matumizi ya magari ya Serikali na ya mashirika ya umma kila siku ya Jumapili kuanzia saa nane mchana lakini wenye magari binafsi waliruhusiwa kuyaendesha (kama nakumbuka vizuri) lakini wakati huo Watanzania waliokuwa na magari yao binafsi walikuwa wachache mno.

Pia ni lazima ukumbuke jinsi Sera za Nyerere zilivyopigwa vita na nchi za magharibi. Hivyo hii iliathiri kwa namna moja au nyingine kupatikana kwa bidhaa mbali mbali

Swali kwako baada ya kuzikumbatia sera za kibepari tangu wakati wa Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete je Watanzania tumeona maendeleo yoyote ya kuridhisha ukilinganisha na enzi za Mwalimu? au tumeona jinsi wageni wakishirikiana na wateule wakifanya wizi wa mapesa chungu nzima na kupora rasilimali zetu?


wewe ndio mwongo. hao waliokuwa na tv walikuwa wanaangalia kituo gani na tv tanznaia zimeanza mwaka 1994? mmeshasahau maduka ya ushirika? ama kweli
 
Ama kweli, tunasahau mno upesi! Sera ya soko huria ilipitishwa 1984, Mh Alhaji Mwinyi alichaguliwa kuongoza nchi 1985! Uamuzi wa watanzania wa au kuwa na sera ya vyama vingi ama la ulipigiwa kura (referandum) na wengi wakataka wabaki na chama kimoja, Nyerere akalazimisha pamoja na haja ya kuheshimu demokrasia, nchi haikuwa na budi walau wakati ule kuupa uzito uamuzi wa wachache yaani kuchagua kuwa na sera ya vyama vingi. Ni pale Zanzibar tu ambako hatujui kilichojiri, hakuna sera yeyote iliyowekwa wazi pale, ni vurugu tu! Sasa wewe Bimkonge na wengine, mnawezaje kudhani Mwinyi ndiye aliyeboresha sera wakati unaona kabisa Nyerere akiwa ni kinara wa kuleta soko huru (1984) na sera ya vyama vingi(1991)?

Lakini yote tisa, sera na mfumo sio miliki ya mtu mmoja!!! Hata huko Marekani, hakuna kinachobadilika eti tu kwa kuwa yupo Obama, yale yale yanaendelea, ni harafu tu ya juu tunayoona kama kihalalisho cha kuwepo aliye katika madaraka....habari ndio hiooo

Watu wakushukuru kwa soko huria ni Marehemu Sokoine(Waziri mkuu) na marehemu Kombe(Mkuu wa usalama wa Taifa)kwa wakati huo ambao walifanya kazi kkubwa sana kmshawishi Mwalimu Nyerere hadi akakubali Mwaka 1984 Mwinyi amekuta kazi hiyo imeisha fanywa mwaka 1985 alipochaguliwa kuwa Rais.
 
Kwani enzi hizo wangapi walikufa njaa? kutugeuza gulio la waarabu wachina na wazungu ndo solution. kufanywa gulio au ili la sasa la kuwaleta wazungu wachukue mali zetu si maamuzi yanayoitaji akili.Ni maamuzi ya kichovi ambayo yataturudisha tu kwenye utumwa.

Inaelekea wewe ni kijana mdogo sana! mwaka 1974 kulkiuwa na njaa haijapata kutokea katika historia ya nchi yetu watu wengi walikufa kwa njaa mpaka tukaletewa mahindi ya njano kutoka marekani,zama hizo ulijulikana mahindi ya yanga!Unalijua hilo?
 
Back
Top Bottom