Ndugai bize na simu huku akiongoza bunge, ajabu kweli!

Yawezekana alikua anawasiliana na wanaohisiwa kupokea rushwa wamkatie asiwataje na asiunde kamati ya kuwachunguza maana nae niwalewale
 
Hapo kuna mawili mkuu.

1) Labda alikuwa Facebook na vitoto vya CBE hapo vikimsifia anavyoonekana hendisamu kwenye Luninga.
2) Au alikuwa anachukua maagizo na kuripoti kwa wakubwa zake wa kazi nani analeta fujo mnadani(Bungeni).

Ni hayo tu mkuu.
 
bunge siku hizi limekua kama ile show maarufu ya BIG BROTHER AFRICA, tusijeshangaa siku moja wakaanza na kuvuta FEGI mle ndani, hakyaMungu tena mi nasema.
 
Ameshasema hajui ana watoto wangapi. Kwenye simu ndo kama hivyo anaweka appointment ya kuchinja kope
 
Mungu atakupiga wewe, ewe ukuta uliopakwa chokaa! Wewe umeketi hapo ili kunihukumu kwa mujibu wa sheria, lakini wewe mwenyewe unakiuka sheria kwa kucheza na simu kinyume cha sheria!” Mdo 23:3
 
Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo ameonekana kuwa bize na kuchati na simu yake ya mkononi huku akiwa anaongoza kikao cha bunge.

Ndugai ameonekana akitumia muda mwingi kubofya bofya simu yake bila kuwa makini na nini anachokiongoza.

Hii imekaaje wana JF, kiuwajibikani na unyeti wa kiti chenyewe?

Source: Channel 10 - habari saa1

Labda anaelekezwa kanuni kwa simu
 
tatizo wabunge wetu wanatumia bangi sana,pia wanaenda bungen ili wapate posho lakin awapend kwenda uko ila imewabid tu kusimamia maslah yao
 
Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo ameonekana kuwa bize na kuchati na simu yake ya mkononi huku akiwa anaongoza kikao cha bunge.

Ndugai ameonekana akitumia muda mwingi kubofya bofya simu yake bila kuwa makini na nini anachokiongoza.

Hii imekaaje wana JF, kiuwajibikani na unyeti wa kiti chenyewe?

Source: Channel 10 - habari saa1
I miss SS speed and standard aka Samwel Sita
 
wakati wanazindua huo mjengo sifa mojawapo ilikuwa
ukiwa mjengoni huwezi kupata mawasiliano ya simu ya mkononi
ina maana walikuwa wanatupiga changa la macho.

Ingekua mi ni spika ningepiga marufuku simu bungeni au ziwe zimezimwa sasa bora hiyo.. Kuna mbunge alipigwa picha anasafisha viatu vyake bungeni.. Hiyo iliniacha hoi ilikua ni wakati wa kuchangia bajeti ya wizara ya kilimo na ushirika sasa kama alikua kaboreka si angetoroka ka wabunge wenzake walivyofanya
 
Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo ameonekana kuwa bize na kuchati na simu yake ya mkononi huku akiwa anaongoza kikao cha bunge.

Ndugai ameonekana akitumia muda mwingi kubofya bofya simu yake bila kuwa makini na nini anachokiongoza.

Hii imekaaje wana JF, kiuwajibikani na unyeti wa kiti chenyewe?

Source: Channel 10 - habari saa1

Usijali, alikuwa anapokea maagizo toka Ikulu namna ya ku-deal na makamanda.
 
Jamani, he is also a social being though ni dalili ya kukosa nidhamu na umakini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom