GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
Bunge haliwezi kukubali Waziri mkuu adharauriwe na sisi tukae kimya, hizo dharau wafanyie huko huko Ndugai
Unaweza kuyaona maneno mafupi yasiyokuwa na Tija lakini kwa tafsiri iliyoshiba yametosha kumtikisa Rais aliyeamua kuonyesha ubabe kwa kumrudisha Kazini Jairo, na masaa machache baadaye akala matapishi yake kwa kuwahadaa watanzania wasiojua protokali kuwa anamrudisha Likizo ili kupisha uchunguzi wa Tume huru ya Bunge.
Anayafanya haya huku anamsahau Ngeleja ambaye naye jana tena alionyesha furaha isiyo kifani akipongeza Uamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo.
Kwa Serikali iliyo makini Ngeleja anapaswa kujipanga sasa kuachia ofisi. Kauli ya Ndugai ni Fumbo zito kwa Wizara ya Nishati na Madini na Mtihani Mkubwa kwa JK jinsi anavyoendesha Nchi kwa ushikaji.
Hapa kintendawili bado ni Kizito sitashangaa haya mabadiliko yanayokuja ya Baraza Mawaziri yakathibitisha ukurasa wa Bifu hili jipya naliliona kwa fasiri yangu juu ya kauli ya Ndugai
ADIOS