Ndugai amvaa Sumaye, asema hana usafi wa kubeza posho!

Tunasema kila siku humu kuwa Tz hakuna msafiiiiiiiiiii,wote tu wachafu either tulichafuka tukiwa wadogo ama tumechafuka ukubwana

kwa hiyo hakuna wa kumnyooshea kidole,tunazidiana ktk uchafu huo

bado siamini kama mkuu wa nchi alibaliki kwa kuipitisha posho inayokataliwa na kila mtu,hivi sisi tumekuwaje jamani?
 
Kweli hata mwendawazimu anaonekana ni mwenye busara iwapo amekaa kimya. Baada ya Ndugai kuongea ndo tumejua kuwa kumbe ni Mpuuzi kabisa. How can he say so!!! Eti "hebu na yeye (Sumaye) atuache na sisi tuandike kitabu chetu". Na hii ndiyo rangi halisi ya CCM na viongozi wake na ndio maana kwenye chama hiki kukemea uovu ni mwiko maana wote ni wachafu na wapo kwa maslahi binafsi. Hii ni hoja nzuri sana Kampeni za 2015.

Hili jamaa hatuna namna ya haraka ya kuliadhibu, ngoja angalau nilizomee tu ..................ooooooooooooooooooooohhhhh!!!! Shame on you!!!!
 
Ndugai kaongelea kauli ya kinafiki ya FTS juu ya posho za Wabunge. Ndugai kamkumbusha tu FTS baadhi ya maamuzi yaliyowahi kufanywa na Bunge lililopita wakati akiwa KIONGOZI wa shughuli za serikali Bungeni. Unadhani ni kwa nini Ndugai hakuwajibu watu wengine wengi tu walioliongelea suala hili?

Kwa hiyo Ndugai katangaza vita na Sumaye?
 
Ndugai hayuko timamu lazima anafile Mirembe sijui kama alimsikiliza Sumaye kwa makini au alisimuliwa?
Yaani hapo ndo kawaza kawazua na ametoka hivyo baada ya kufkiria kwa kina na umakini mkubwa. Huyu atakuwa ni Naibu Spika wakwanza duniani kuongea upumbavu.
 
Mkuu umeongea kitu cha maana sana yani hizi kauli zao wakati mwingine zinaweza kukutoa machozi hawana huruma kabisa, mm najiuliza hivi hawaoni maisha yanavyotugonga sisi wananchi tunaolipwa 1500 kwa siku kwenye makampuni ya kichina na wahindi.
Tatizo viongozi wetu wengi hawapendi kuambiwa ukweli wao wamezoea kutudanga kwa makaratasi yaliyojaa takwimu za uongo, wanatakiwa waelewe kuwa watz sio mambumbu tena kama walivyozoea.
Kiongozi kama Ndugai amejionesha utupu wake hivyo nawashauri watu wa jimbo lake kumnyima kura maana huo ubunge ameufanya kama sehemu ya kutengenezea utajiri.

Vilaza kama Ndungai na wenzake ropo,ropoka hawa...

Ni lazima tuwataftie dawa mapema, mara 2 wanapotoa kauli za kuchefua na kuonyesha moja kwa moja nia ya kutuibia na uroho wa rasilimali zetu..

Kukaa na vilazi na Wajinga kama Ndungai na watu kama Magufuli regadls wanaelimu kiasi gani kwa miaka iliyobaki kufikia uchaguzi,wanaweza wakatuua kwa presha au kwakutumalizia pesa zetu kwa kujipandishia posho...!!
Muhimu kwenye KATIBA MPYA,, lazima 2weke sheria..
Na kwa kuwa katiba itachelewa,,, 2andamane na 2wakatae kwa sauti kuu..
Wanatutia Aibu bwana...
 
Majibu ya Mh. Job Ndugai kwa Mh. Sumaye kwamba eti 'hana haki' ya kuongelea posho ya laki mbili ni kielelezo kingine cha ULEVI wa madaraka na uroho uliopindukia ambao uko deep ndani ya baadhi ya viongozi wetu.

Tafsiri ya kauli ya Mh. Ndugai ni kwamba:
- si ruksa (ni dhambi) kwa mtu aliyekuwa na tabia mbaya zamani (kama ulevi, umalaya, wizi, uchawi, etc.) kuongelea tabia hizo mbaya au kutoa ushauri kwa wengine ili nao waziache. HILI NI JANGA!
 
mawazo ya njaa za viongozi wenu kina ndugai. watanzania watawakumbuka kwa ufisadi, ulafi, wizi na kila maovu dhidi ya wananchi wanaolia kila siku bila hata mkate. ndugai na wenzako mjiandae kutoa majibu kwa mungu dhidi ya mateso mnayosababisha kwa watanzania kwa ulafi wenu.
Mi nadhan haina haja ya kusubiria hadi huko kwa mungu, kwan hakuna cha kuwafanyia nyakati hizi???kwani hawa viongoz waliojisahau hatuna namna ya kuwavua utawala????Inamana pale anazo siri nyingi za uhujumu uchumi alizomfichia sumaye na ndo mana kasema hataki kusema mengi, hivi huo si ndio unaoitwa usaliti kwa watanzania??kweli mtu wa hivyo ana sifa ya kuendelea kututawala???
 
Ndungai anasema kwa ujasiri kwasababu anauhakika hakuna awakumfanya chochote. Kwa kifupi anasema nyie mlikula kwa urefu wa kamba zenu na sisi pia twala. Watz watalalama na baadae watanyamaza. Kwa mantiki hiyo anamtaka Sumaye kusema live anataka nafasi nyingine yakula period. Kheri yao wabunge na viongoz wa seriali kwa maana ugumu wa maisha hautazikuta familia zao.
 
Kitu kimoja tu nachojifunza - Hakuna msafi CCM!...

Yaani, Naibu Spika Ndugai anasimama kuelezea uchafu wa Sumaye ili kupunguza makali ya Posho au? maana simuelewi mtu anapohoji mabovu ya mtu kwa huruma ya wananchi wakati yeye pia anataka kuwaongezea wananchi mzigo ule ule..

Kama anajua mafao ya viongozi yaliwekwa kinyemela imekuwaje muda wote huo alikaa kimya bungeni asihoji isipokuwa pale ulaji wake unapowekwa mashakani?... Jamani, Jamani Wadanganyika miye sitaki weee!
 
duh!dr bana!!!ndugai!!msomi ***** anachumia tumbo na anatumia masaburi kufikiria na kutoa ushauri wa kisomi na juzi juzi nilimuona tbc akijikomba kwa mukama badala ya kushauri.ndugai yy hata sitaki kusema coz alishaanza siku nyingi,kutoa mke wake wa pili kongwa hosp.na kumpeleka wizarani,jimbo lake lenyewe usiseme nimepita juzi utadhani halina mwalikilshi miaka kumi iliopita.lao moja na spika waandike kitabu ni zama yao lol magambaa....jk matunda yako ya kupachika watu wasionasifa kwenye nafasi nyeti!!
 
Mimi nilishajua tu kuwa safari moja huanzisha nyingine, huu ni mwanzo tu tusubirie mengine yaja.
 
Sijui kwanini hawa magamba huwa hawatafakari mambo ya kuongea kwa wananchi? Sijui ndo mwisho wao wa kufikiria !
 
Back
Top Bottom