Ndugai alipompiga mkwara Halima Mdee Bungeni Leo

ukada umemzidi ndugai kuliko kuwa kiongozi, abadilike la sivyo hali itakuwa mbaya sana kwake
 
Yani huyu NDUNGAI namchukia kupita maelezo, anajiona yeye ndio yeye na anaona Tanzania nzima hakuna anejua sheria kama yeye.Huwa ana ubabe sana kwa wapinzani na ushabiki wa wazi wazi na usiokuwa na maana kwa CCM.Yani ni afadhali makinda kuliko huyu kibaraka anaejiskia na kujiona ni mbabe.Kuna siku huko mitaani watampiga mawe

Jamani naomba CV za Job Ndugai, he has proved to be one of those CCM vihiyos!
Hebu mwenye kujua CV yake aiweke hapa jamvini tuichambue. Kwa kweeri jamaa ameni-bore stiff kinoma. Jana nilikuwa natamani nikamzabue kibao kwenye runinga wakti akitapika kejeli zake za kinafiki.

CCM bwana imejaa majuha na vihiyo watupu.

Pambaf kabsaa!
 
Kitendo cha spika aliyepitwa na wakati, kuwaita wabunge wa upinzani (Chadema) wanafiki ni cha dharau kinaonyesha anavyojikweza pale anapopata nafasi ya kukaimu uwaziri mkuu. Chadema wamepinga posho hizo kwenye bunge la 10 na siyo la 9 baada ya kugundua ubadhirifu wa pesa za umma ili zisijitokeze tena katika siku zijazo, jambo la kujiuliza Sitta anachokasirika ni nini!!!. Sitta analeta mambo ya kitoto wakati anamvi hadi miguuni, je Sitta yuko tayari kurudisha pesa zote alizopokea ikiwemo mshahara wake alioutumikia katika Bunge la 9???? Posho za watumishi serikalini lazima zipunguzwe zikafanye kazi ya maendeleo. Pamoja na kwamba Job Ndugai alimkingia kifua Sitta kutofuta kauli yake lakini Watanzania wameelewa utoto unaofanywa na Serikali na Bunge dhidi ya wapambanaji wa Chadema.
 
Ndugai siku zenu zinahesabika sijui kwnini hamwezi kujifunza na kusoma alama za nyakati! Wananchi wana hasira sana na kukosekana kwa umeme nyie wabunge mnakula vizuri mnatibiwa vizuri bado mnafanya mizaha bungeni, wabunge wa chadema hongereni kwa kazi nzuri mko pamoja na wananchi magamba tutakutana nao kwenye chaguzi, na sasa tutahamasisha vijana nchi nzima wajiandikishe ili waje wawape adabu hao magamba
 
Hatukuoneshwa ni nini Mdee kafanya ambacho kilimfanya Ndugai kuwa MPUUZI (unapopuuzia jambo lili/nalofanywa na mtu au kikundi cha watu, ww ndo unakuwa MPUUZI) ila hisia zangu zinanilazimisha kusema kuwa Mdee alitoka bungeni kwa hasira kitendo ambacho kilifuatia yeye Halima kutopatiwa nafasii ya kuongea kama utaratibu unavyotaka, so akamfanya Naibu Spika MPUUZI, na akakubali kuwa mpuuzi mwenye heshima
 
Ndugai,

Vipi mzee, Matokeo ya semina elekezi au ulipitiwa, kuwa mkweli, siamini nilichokiona na kukisikia kikitoka kwako jana, au mnadhani hatuangalii bunge??
 
bado najiuliza.. hivi huko CCm wanalishwa kiapo cha kuukana uzalendo? na ntaendelea kujiuliza mpaka ntakapopata jibu
 
Tumeona dhamira halisi ya ccm sababu upinzani inakuwa kama dhambi wakati ni taratibu halali za kiuongozi!
 
Hili Bunge limejaa wanafiki..
Wanafiki wenye kujipenda na kutokujali hisia za wenye kujaribu kuleta uzalendo kwa Taifa. Maneno ya chini chini pamoja na kejeli zinaligeuza Bunge kuwa dangulo la vijembe na si Bunge kwa maendeleo ya Taifa. Hii ni dharau wanayofanya wawakilishi wa CCM ndani ya Bunge. Vitendo vya jinsi hii si vya Spika wa Bunge pekee kuvipinga na kuvizuia visitokee bali Rais wa nchi alipaswa kwenda Bungeni na kukemea hili na kuweka msisitizo wa sheria za bunge kipindi chote cha mahudhulio.
Sishangai endapo nitasikia Rais hufurahishwa na tabia hizi za mawaziri wake na wabunge wa CCM kutoa maneno na kauli za kebehi kwa wabunge pinzani.
Tabia ya jinsi hii haiwezi kutufikisha mahala popote.
 
Kwa mara nyingine tena nasema, ukishaona kwamba huu ni mkaa usitegemee kitu cheupe kwenye huo mkaa, vile vile ukishaona huyu ni magamba usitegemee kumuona mwadilifu hapo.


A friend of my enemy is my enemy too.
 
waaaaai.....................ndo maana nimeacha kabisa kufuatilia hii mijadala! Hata mie na mwanangu hatuwezi jibizana hivi seuze mwakilishi wa wananchi?
 
Nilikuwa nafuatilia Bunge na nikakuta sehemu ambayo walikuwa wanazungumzia suala la Bima za Wabunge - wakijadili kauli ya Kafulila kuwa Wabunge ni "privileged class" kuwa wanapata huduma ya afya wao na watoto wao. Ndugai alipokuwa akijaribu kutoa ufafanuzi alidokeza kitu kuwa wabunge hawana bima ya afya na Bungeni linawafanyia utaratibu. Akatumia muda pia kurusha vidonge vya mwisho na kama utakavyosikia Halima Mdee akataka kupata "taarifa"... well listen

View attachment 33772

Mimi ninavyoelewa hata mwajiri anapokulipia huduma za afya wewe na wategemezi wako kwa asilimia mia moja nayo ni bima ya afya kwa mfaidika. Tofauti na hii bima ya afya mfano ya NHIF ni kuwa mwajiri na mwajiriwa wanalipia michango (au premium) kwenye mfuko ambao hutoa cover kwa magonjwa yaliyoainishwa. Kuna wananchi wengi ambao hawana bima ya aina hiyo na hivyo wabunge wasitake kutuaminisha kuwa wao ni waathirika wa kukosa bima ya afya kwani ukweli ni kuwa wakiugua hutibiwa kwa gharama za serikali.
 
Jamani naomba CV za Job Ndugai, he has proved to be one of those CCM vihiyos!
Hebu mwenye kujua CV yake aiweke hapa jamvini tuichambue. Kwa kweeri jamaa ameni-bore stiff kinoma. Jana nilikuwa natamani nikamzabue kibao kwenye runinga wakti akitapika kejeli zake za kinafiki.

CCM bwana imejaa majuha na vihiyo watupu.

Pambaf kabsaa!

Kuona vyeti vya Ndugai haitakusaidia sana kwani hata wenye Phd za ukweli wakiingia bungeni kwa ticket ya CCM hulewa mvinyo wa ufisadi na kufanya vitendo sawa na wale ambao wameghushi vyeti vya usomi. CCM ndivyo walivyo.
 
Wabunge wa CCM ni vilaza sana wanajifanya kujikosha kwa wananchi kua wao wanatibiwa humu humu, mbona hata siku moja sijawahi kukutana na waziri kwenye foleni pale muhimbili? waache unafiki wanadhani sie wananchi ni wajinga
Swali la Kizushi: Hivi na Mzee malecela amelazwa hospitali gani pale Mtera?
 
ndugu zangu hili bunge letu linaaribiwa na ccm kuanzia spika,naibu spika na hata viongozi wa selikali bungeni.kwa kweli naanza kupata mashaka na spika aliyepita samwel sitta, huyu jamaa sio mzuri kabisa naanza kuamnini maneno ya watu kwamba ,msimamo wake wa kipindi kile sababu alikosa madaraka fulani serikalini so alipopata madaraka ya uspika akalipiza kisasi kwa serikali,jamaa ni mpenda madaraka misiimamo yake ya siku za karibuni ni ya kifisadi mwisho namalizia hivi, NDANI YA SERIKALI LEGELEGE ILIYOSHINDWA KUKUSANYA KODI ,NDANI YA CCM HAKUNA MTU MSAFI,LAKUVUNDA HALINA UBANI,CCM IMESHAVUNDA

NAWASILISHA.........
 
Inauma sana aisee!
Hii ndo mision ya ccm, kufanya bunge kuwa genge coz wao hawawezi kutoa hoja zenye mashiko.

Sita huyu huyu! Sita mnafiki aliyeanzisha ccj akita ccm?

Kuna sababu za msingi za kuwa na bunge la mtaani baada ya bunge hili. Wananchi wanahitaji kuelezwa kwa undani yanayofanyika bungeni na ni kwa jinsi gani ccm wamekataa mapendekezo ya maendeleo na kukumbatia posho, kutoa misamaha ya kodi huku watz wakiteseka kwa kukosa huduma muhimu za msingi.
 
Ndugai na Mr.6 walikuwa ni miongoni wa wanaccm wachache niliokuwa ninawaheshim lkn kadiri siku zinavyozidi kwenda nagundua ukishakuwa kiongozi katka ccm katika ngazi yoyote ile basi akil zako za kawaida lazima uziweke kando na kuendelea kushabikia uchizi kwa maslah ya chama. Hivi mtu ukiwa mlevi ukaamua kuacha pombe basi ni lazima kurudisha zile pombe zote ulizokunywa ndio tukujue kuwa umeacha ulevi.

Kauli za kudhalilishana na kuvunjiana heshima zinaongozwa na wanaccm wenyewe na hakuna mtu wa kuzikemea hata kama zinakiuka kanuni na sheria na bunge badala yake wanaziacha na kuzidi kulishushia heshima bunge na ni bora wangeacha kauli za kuliita bunge TUKUFU kwani halina utukufu wowote ila waliite bunge la mipasho.
Naomba Pro. Kahigi awakumbushe maana ya unafiki kwa kiswahili fasaha na waone kama wako sawa kutumia kauli hizo au kuumpuuza mtu anayetaka kutoa taarifa wkt hujajua ni taarifa ipi iliyokuwa anataka kuitoa. Mwisho wa siku watz tutakabidhiwa rungu na tutawahukumu kwa ukatili bila ya kuwaonea huruma.viva chadema msichoke na mapambano wanasema mtafutaji hachoki na akichoka ujue kashapata. hata kama wakiwadhalilisha na kuwashutumu fahamuni njia ni ngumu ikiwa na mabonde, milima, miiba na mbigili kwa ajili ya ukombozi wa mtz..
 
Jamani naomba CV za Job Ndugai, he has proved to be one of those CCM vihiyos!
Hebu mwenye kujua CV yake aiweke hapa jamvini tuichambue. Kwa kweeri jamaa ameni-bore stiff kinoma. Jana nilikuwa natamani nikamzabue kibao kwenye runinga wakti akitapika kejeli zake za kinafiki.

CCM bwana imejaa majuha na vihiyo watupu.

Pambaf kabsaa!


CV yake hii hapa.


GENERAL
SalutationHonourableMember picture
1199.jpg
First Name:Job
Middle Name:Yustino
Last Name:Ndugai
Member Type:Constituency Member
Constituent:Kongwa
Political Party:CCM
Office Location:P.O. Box 64, Kongwa - Dodoma
Office Phone:+255 762 605 951/+255 655 605 951
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:
Member Status:
Date of Birth
EDUCATIONS
School Name/LocationCourse/Degree/AwardStart DateEnd DateLevel
University of NorwayMSc. in Mgt. Natural Resources&Sustainable Agric.19951996MASTERS DEGREE
University of Dar es SalaamBSc.(Zoology Wildlife Ecology)19891993GRADUATE
University of NorwayPG Diploma in Mgt of Natural Resources19941995POSTGRADUTE
MWEKA Wildlife CollegeDiploma in Wildlife Management19861988DIPLOMA
Open University of TanzaniaLLB2000TodateNOT COMPLETED
Kibaha Secondary SchoolO-Level Education19781981SECONDARY
Old Moshi High SchoolA-Level Education19821984HIGH SCHOOL
Matare Primary SchoolPrimary Education19711977PRIMARY
CERTIFICATIONS
Certification Name or TypeCertification No.IssuedExpires
No items on list
EMPLOYMENT HISTORY
Company NamePositionFrom DateTo Date
Frankfurt Zoological SocietyTechnical Officer20002000
Serengeti Regional Conservation ProjectManager19971999
Ministry of Natural Resources and TourismCoordination Officer19961996
Selous Game ReserveManager19931999
Ministry of Natural Resources & Tourism-Liwale DistrictWildlife Officer19881989
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
CCM-Chama Cha MapinduziMember of Parliament(Kongwa District)2000Todate
CCM-Chama Cha MapinduziWard Youth Commander19961999
CCM-Chama Cha MapinduziChairman(Work Place)19961999
CCM-Chama Cha MapinduziMember1981Todate
PUBLICATIONS
DescriptionPublished Date
No items on list
SPECIAL SKILLS
Skill Name or DescriptionYears ExperienceAcquired ThroughSkill Level
No items on list

RECOGNITIONS
Recognition TypeRecognition DateReasonAction TakenIssued by
No items on list
 
Back
Top Bottom