Ndugai alipompiga mkwara Halima Mdee Bungeni Leo

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Nilikuwa nafuatilia Bunge na nikakuta sehemu ambayo walikuwa wanazungumzia suala la Bima za Wabunge - wakijadili kauli ya Kafulila kuwa Wabunge ni "privileged class" kuwa wanapata huduma ya afya wao na watoto wao. Ndugai alipokuwa akijaribu kutoa ufafanuzi alidokeza kitu kuwa wabunge hawana bima ya afya na Bungeni linawafanyia utaratibu. Akatumia muda pia kurusha vidonge vya mwisho na kama utakavyosikia Halima Mdee akataka kupata "taarifa"... well listen

View attachment ndugai.mp3
 
Nilikuwa nafuatilia Bunge na nikakuta sehemu ambayo walikuwa wanazungumzia suala la Bima za Wabunge - wakijadili kauli ya Kafulila kuwa Wabunge ni "privileged class" kuwa wanapata huduma ya afya wao na watoto wao. Ndugai alipokuwa akijaribu kutoa ufafanuzi alidokeza kitu kuwa wabunge hawana bima ya afya na Bungeni linawafanyia utaratibu. Akatumia muda pia kurusha vidonge vya mwisho na kama utakavyosikia Halima Mdee akataka kupata "taarifa"... well listen

View attachment 33772
Kaka kama vile sijakupata hapa
 
Sitta na yeye ni MNAFIKI tu. Kama siyo kweli basi na yeye arudishe hela alizochota pale CDA Dodoma.

Hiyo mimama inayoropoka naona ni ile ya ubunge wa KUHONGWA.

Naona mwaka 2015 moto utawaka. Hawa wengi itabidi kuwapandisha kizimbani.
 
leo nina kupuuza duh, ina maana halima mpuuzi?
yeye kama naibu spika anaposema wanaopinga ni wanafiki ina maana hajui hao hao anao waita wanafiki ni kina nani?
ina kuwaje hivyo vipaza sauti lakini kila mtu anaweza kuongea tu anavyotaka bila kuchukuliwa hatua.
hivi ili suhala la posho kwa nini wana ccm wanaita wabunge wa chadema majina ya kijinga?
kama wanataka kujua msimamo wa wananchi wafanye POLL moja kwa wananchi wapate message wananchi wako upande gani, kama hawajakuta na sisi wananchi wanatuita wanafiki ya kwamba walikuwa wanalipwa toka zamani na sasa tunapingwa kwa nini hatukupinga zamani?

dunia ni mabadiliko mbona na wao wanatumia pc leo na wasibaki na mambo ya zamani?
sasa ni wakati wa mabadiliko ndio maana mambo yanaibuka na ccm wanapaswa kuheshimu hilo
 
Wananchi wananchi wanaoteseka wao wafe tuu hawastahili kabisa bima ya afya, ila wabunge wanastahili zaidi bima ya afya.

Sounds weird sort of.
 
Tulishasema hawa magamba wanadhani wananchi bado wanadanganyika. Ngoja wajifariji kuwa itakuwa business as usual 2015, wengi watakuja kuzimia kama siyo kufa kabisa maana hawatamini yatakayokuwa yanatokea.


Pengine wanataka kuchukuwa chao mapema na wengi wao wameshajua kuwa 2015 hawatarudi tena. Nahisi wanataka kukikimbia chama chao 2015 ,maana kila mtu hajiamini tena.
 
Kwanza nikushukuru sana MM kwa kutu-keep us posted kwani watu wengine hatukubahatika kufuatilia shughuli za Bunge kutokana mgao wa umeme. Jamani hoja ya CHADEMA si kurudisha posho bali kufuta posho za vikao (sitting allowance) katika mfumo wetu wa malipo. Na muongozo ulioombwa ni kuhusu kauli iliyotolewa na Sitta ya kuwaita Wabunge wa upinzani WANAFIKI.

Sasa muongozo unaotolewa ni mwingine kabis! wala haiitaji kwenda shule kujua kuwa Mh. Ndugai hakuwa IMPARTIAL kabisa, yaan warudishe posho!? Ndugai Vipi tena? Toa muongozo unaostahili. Vice President wa Tanzania Visiwani ameshasema hii ni HOJA YA MSINGI na inapaswa kupatiwa majibu ya MSINGI, sasa hizi kebehi zinatoka wapi? Na huyu Sitta sasa ameanza kulewa madaraka, binafsi nilikuwa ninamtunzia heshima sana, but kauli zake zimeanza kunipa wasiwasi
 
Nimesikiliza hii Audio, nadhani Mh. Halima Mdee ana haki kabisa kuandika lalamiko rasmi kwa kamati ya uongozi wa bunge kutokana na maneno makali aliyotumia Naibu Spika dhidi yake pale aliposema 'kwa leo nakupuuza'. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu ikizingatiwa kuwa Naibu Speaker huyu hakuwa amesikia ni taarifa gani Mh Halima Mdee alitaka kutoa Bungeni.

Kadri siku zinavyosonga mbele wabunge wa ccm wanazidi kujiamini kuwa wamewashinda wabunge wa CHADEMA. Laiti wangejuwa huku mtaani hukumu wanayolimbikizia wangejirudi. Wao waendelee kutetea posho lakini come 2015 every man and woman will have to fend for him/herself. Na hakuna pa kutokea maana DVD zitapigwa kila kona.
 
Nimesikiliza hii Audio, nadhani Mh. Halima Mdee ana haki kabisa kuandika lalamiko rasmi kwa kamati ya uongozi wa bunge kutokana na maneno makali aliyotumia Naibu Spika dhidi yake pale aliposema 'kwa leo nakupuuza'. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu ikizingatiwa kuwa Naibu Speaker huyu hakuwa amesikia ni taarifa gani Mh Halima Mdee alitaka kutoa Bungeni.

Kadri siku zinavyosonga mbele wabunge wa ccm wanazidi kujiamini kuwa wamewashinda wabunge wa CHADEMA. Laiti wangejuwa huku mtaani hukumu wanayolimbikizia wangejirudi. Wao waendelee kutetea posho lakini come 2015 every man and woman will have to fend for him/herself. Na hakuna pa kutokea maana DVD zitapigwa kila kona.

its a message kwa wananchi kuwapuuza wao ambao hawajui wananchi wanataka nini. Halima hakuongea kama yeye kama unampuuza halima ina maana unapuuza wapigakura wake wote na watu anaowawakilisha
 
Asante sana Mzee Mwanakijiji kwa hii audio. Nimesikitika na sichangii kwa leo.
 
Hivi hajui Halima anawakilisha jimbo lenye wananchi waelewa kuliko majimbo yote nchini? Nadhani umefika wakati turekebishe sheria zetu,haiwezekani mbunge anayewakilisha Kawe kura yake ilingane na mbunge kama Ndugui ama mbunge toka Znz anayewakilisha watu elfu 5!
 
Na hasira na hiyo mijitu kusema kweli imechafua hali ya hewa
Sure!tena ni tangu mchana.maana hii issue ya kafulila na bima ya afya imeanza asubuhi!mi nimekerwa sana!bunge limekuwa km vikao au mikutano ya kijiji!sauti zinatoka mpaka maneno makali,km kavuta huyo! Siyo mwongozo! Achia kiti! N k!ni aibu sana.
 
Nimesikiliza hii Audio, nadhani Mh. Halima Mdee ana haki kabisa kuandika lalamiko rasmi kwa kamati ya uongozi wa bunge kutokana na maneno makali aliyotumia Naibu Spika dhidi yake pale aliposema 'kwa leo nakupuuza'. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu ikizingatiwa kuwa Naibu Speaker huyu hakuwa amesikia ni taarifa gani Mh Halima Mdee alitaka kutoa Bungeni. Kadri siku zinavyosonga mbele wabunge wa ccm wanazidi kujiamini kuwa wamewashinda wabunge wa CHADEMA. Laiti wangejuwa huku mtaani hukumu wanayolimbikizia wangejirudi. Wao waendelee kutetea posho lakini come 2015 every man and woman will have to fend for him/herself. Na hakuna pa kutokea maana DVD zitapigwa kila kona.
Mkuu nahisi wabunge wetu wa cdm kama wameishiwa mbinu za kupambana na mbinu za ccm kuzima hoja nyingi mle ndani.hoja nyingi kuzimwa ni ushindi kwa ccm hasa tukiangalia namna wananchi wengi wakiwa bado hawajakomaa na elimu ya democrasia na uwajibikaji wa viongozi.siku zinakwenda na hoja zinazimwa kwa mbinu zile zile huku wabunge wetu wakionekana kama walalamikaji tu bila hatua zozote.cdm tunapaswa kuwa wamoja mle ndani kiitikadi na ki mbinu.inabidi utumike mtindo wa kijeshi wa collective responsibility kulazimisha kusikilizwa na kufanyiwa kazi hoja zao.wabunge wanadhalilishwa mno kama kuambiwa kaa chini! Nakupuuza na kukamatwa kama vibaka tena kwa kejeli!binafsi sitaki kumlaumu spika wala wabunge wa ccm maana wanafanya kazi waliyotumwa! Lakini wabunge wa cdm wanakabiliana vp na uhuni huu? Uhuni umezidi bungeni hakuna hatua na matamko yametuchosha inabidi kutumia sheria zilizopo na za kimataifa kulazimisha demokrasia kuchukua nafasi.tusiwalaumu ccm wanafanya waliyotumwa,cdm wanafanya nini mle kabla hawajarudi kwetu mitaani?
 
MTAZAMO,
Siasa ni mchezo na mnapokuwa wengi ni advantage. Naamini wabunge wa ccm na spika/naibu spika hawajatumwa na wananchi hayo wanayoyafanya. Maadamu tunaona, tuchukue hatua. Cdm kwa uchache wao hawana la kufanya zaidi ya kuwashitaki kwetu na hasa kwa wale ambao hawakuona au hawakuelewa kilichotokea ili maamuzi yetu yazingatie mambo hayo. Tuwahukumu hao wanaowadhalilisha viongozi tuliowachagua maana wanatudhalilisha hata sisi kwa manufaa ya chama chao badala ya wananchi waliowapigia kura!
 
Ndugai, mwiso wako waja na wala hautakawia. Huwezi kuendelea kuwadhalilisha wananchi kwa kutumia kiti cha spika. unaijua taarifa aliyotaka Mdee? Hujui! Mwisho wako unakuja!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom