Ndoto za watanzania katika kupata mafanikio na raha soka.............

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Ni jambo lililowazi kuwa watanzania tumekuwa na kiu ya muda mrefu kupata mafanikio katika michezo na hasa soka kuanzia timu ya taifa hadi ngazi ya klabu. Serikali kwa kushirikiana na TFF wameleta makocha wa kigeni, klabu nyingi ingawa si zote zimejitahidi kuleta makocha wa kigeni.

Lakini kwa mtazamo wangu bado naona mlima tunaojaribu kuupanda ni mrefu mno kulinganisha na mikakati yetu. Jambo moja linalonikera ni tabia iliyojengeka kuanzia kwenye vilabu mpaka timu ya taifa. Inapotokea timu ya taifa au klabu kuingia katika mashindano na hatimaye kupambana na timu zenye kiwango cha juu cha soka basi kuna mtu, kikundi cha watu au taasisi fulani kutoa ahadi kwa wachezaji kuwa endapo wataishinda timuhiyo basi watazawadiwa kitita cha fedha.

Mifano ni mingi na tunaijua. Lakini sidhani kama kwa ahadi za fedha tunajenga timu zetu ikiwemo Taifa Stars. Kwa mtazamo wangu naona kuwa ni danganya toto kwa kitu ambacho tunajua fika kuwa timu zetu hazitaweza. Kwa nini basi mapesa haya na vitu vingine vikatolewa kama ni nyenzo za kuijenga timu ikijiandaa kwa mashindano husika??? Juzi friends of Simba waliahidi wachezaji wa Simba kuwa wakiifunga TP Mazembe watazawadia Mil 100 sitashangaa keshokutwa Taifa Stars wakipamba na Afrika ya Kati tukasikia wanaahidiwa bingo.....Kwa kweli tunahitaji kubadirika kama kweli tunataka ndoto yetu iwe kweli.....
 
Back
Top Bottom