Ndoto yangu usiku wa leo

bakuza

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
490
100
Nimeuota mti ,mti huu ni chotara maana ulitokana na mbegu mbili moja toka Zanzibar na nyingine Tanganyika nakumbuka ilikuwa 1977 ndipo zilipochanganywa ili kupata mbegu moja.Nao ulikua na kuwa mkubwa ajabu babu na baba zetu walishirikiana kuupanda ili watoto na wajukuu tupate kivuli chake na liwe pumziko letu badala ya ile michongoma iliyokuwepo mwanzo ikituchoma kwa miba yake.Namkumbuka babu mmoja aliyekuwa mpandaji mkuu siku ile na alijitahidi kuumwagilia na kuulinda usiharibiwe na wadudu na wanyama wafugwao na hata wale wa mwituni,ni kweli ktk uhai wake ulistawi mpaka tukautungia nyimbo rukuki mashuleni na majeshini.Ulionesha dalili njema za kutupa kivuli cha kutosha na ukijani wake ulivutia macho,ni wengi tuliupenda mti huu.
Babu kachoka kaona nguvu zinamuishia kawakabidhi wanawe yaani baba zetu ili waumwagilie,kuutilia mbolea na kuutunza ili majani yake na ukijani wake uzidi kuwa faraja na matumaini kwa watoto na wajukuu zake Laaahaula!!!!!! hakujua kuwa wanawe walikuwa na shauku ya kupata mbao za mti ule basi wakamhifadhi babu mapema.Nakumbuka walivuka maji kwenda kujadili jinsi ya kupata mbao,kuni na hata majani ya mti wetu,walivuka maji ili babu na wajukuu tusisikie wanayopanga.Wakapanga ikapangika nao wakaanza kuupekecha mti kuanzia katika mizizi yake na mti ukaanza kusinyaa babu akastuka na kuuliza wanaye kulikoni mti wasinyaa.. haa..!! wanaye na mkubwa wao akiitwa Ben si wakastuka wakaona isiwe noma na tumuhifadhi huyu babu mapema ili asiiharibu mipango yetu tuliyopanga.Maskini babu yetu wakampeleka kwa wale waliotupandia michongoma ikatuchoma ati wanamtibia wakamhifadhi na kutwambia ni Leukemia imemuondoa.

Baada ya babu kuondoka ndipo wakazidisha kasi ya kukata kuni na mbao toka mti ule ilihali umesimama nao ukazidi kunyauka kwa kasi ya ajabu na kupoteza majani yake na kivuli kilichobaki ni cha shina na ni kwa ajiri ya wakata mbao,maana majani yanapukutika na yakaribia kuisha.Nilipouangalia kwa ndani maskini umeliwa na kuoza lakini wakati wowote waweza kuanguka na anguko lake ni kuu na laweza kuwadhuru waliokaribu na walio mbali.Na msimamizi kutoka Bwagamoyo aliyeachiwa na Ben hana ujuzi wa kukata mbao asidhuru watu naye mara nyingi huukimbia mti akienda safari zake za kila uchao huku nyuma wadogo zake nao wazidisha kasi ya kuupurula majani yake na kuni kujikatia huku wakijifariji na kumfariji msimamizi mpya wakiuimbia nyimbo za kuusifu kuwa ni nambali moja.
Punde si punde watu si wakastuka wakaanza kukimbilia miti iliyooteshwa 1992 na kati ya miti hiyo mmoja waonekana kuwa na kivuli cha kupumzikia na ukuaji wake ni mzuri ajabu waweza kuwa mkombozi kwa wajukuu wa babu.


Msimamizi toka Bwagamoyo na wakata mbao wenzie wakastuka kuona kunawili na kustawi kwa mti mpya na jinsi wajukuu wa babu wanavyokimbilia huko,Mkakati ukasukwa kuufitinisha mti mpya na wajukuu wa babu ila ikashindikana wakakosa hoja maguvu ya wenyenguvu waliostahili kutulinda yakatumika na hata wazee wa baraza wanatumika sasa lakini mpaka sasa twasubilia anguko kuu la mti wa babu sababu umeoza hadi kwa nje na njia zote za kuzuia anguko la mti wa babu zimeshindwa.Vitawi vyake vimesha anza kudondoka na kuwadhuru wajukuu wa babu na wengine wanapoteza maisha lakini wameamua kuona ukidondoka.Enyi wakata Mbao nawe msimamizi wao kateni kwa ustarabu anguko lake lisiwadhuru wajukuu wa babu na dunia yote ikasisimka.Kumbuka msimamizi mkuu na wafuasi wako mkatao mbao katika mti huo waweza usiwaangukie lakini kumbuka damu za wajukuu wa babu zitakazo mwagika hazitowaacha na hata hizi zilizoanza kumwagwa na matawi ya mti wenu ni kitanzi kweni.

 
Asante muotaji yawezekana nikawa mtafsiri kama Yusuf. Hakika yatatokea anguko na liwe acha lisage watu na liondoke na damu za watu wa karibu na wa mbali ili pawe na kumbukumbu ya ubarudhuli kama tunavyosoma wakoloni walivyo watesa mababu zetu.. kupe aking'ang'ania sana kwenye ngozi mwisho anaondoka na damu! kupe ang'oleweeeee
 
Waliondolewa wakoloni wenye ngozi nyeupe, ambao siku zote walikuwa wakituaminisha kuwa wao si binadamu wa kawaida na kwa hivyo isingekuwa rahisi kwetu kujinasua kutoka kwenye minyororo yao ya utumwa, itakuwa hawa!! tunaoishi nao kwenye mitaa yetu? tunavijua hata vibanda vyao na familia zao. Wasijidanganye kwa kuvitegemea vyombo vya dola. hao nao ni ndugu zetu wahanga pamoja na sisi wa madhara ya utawala wa ccm. Ni kweli kabisa hao wanaoukata huo mti nawataadharisha waangalie hayo matawi yasiendelee kuwadhuru wajukuu wa babu. la sivyo wajue tunawajua hadi vibanda wanamoishi. tunawavutia pumzi tu.
 
Back
Top Bottom