Ndoto hizi ni utata mtupu, Naomba msaada

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,534
Wanajamvi hii ni mara ya pili sasa nakuja kwenu,

Mimi ni kijana masikini ambaye nina amini ipo siku katika hii mihangaiko yangu nitafanikiwa kimaisha, huwa naota ndoto na %90 huwa zinatokea kweli, miezi mitatu iliyopita niliota pikipiki yangu inaungua moto na kweli jana mida ya saa 12 jioni wakati naifanyia service ilishika moto na kuanza kuungua bahati nzuri nikaiwahi kwa kuizima na maji hivyo haikuharibika.

Usiku wa kuamkia leo nimeota nipo na rais Kikwete pamoja na mkewe Salma tunakula, hii ikiwa ni mara ya tatu kuota nipo na Kikwete, rais Bush akiwa madarakani niliota zaidi ya mara nne nikiwa naye na mara ya mwisho nikiwa nimekaa naye ndani ya Air Force One, Obama nimeota nipo naye mara mbili, Tony Blair niliota nikiwa naye Israel katika dhifa maalumu..

Hata Mkapa, Mwinyi nimeota mara nyingi nikiwa nao, napata hasira napoamka asubuhi na kujikuta nipo na shida zangu tu, ndoto hizi zina maana gani kujirudiarudia miaka yote? Wataalamu wa ndoto mnisaidie.
 
Kweli hao wakina obama ulikua nao ila ndotoni tatizo ulovyoota hukuomba hata mchongo wowote ndio maana haupati mualiko

ngoja uote unakufa kama utataka hiyo ndoto itimie
 
Hizo zinaitwa manic hallusination, na zinatokana na maisha yako magumu na expectation ulizonazo, usisiamini hata siku moja kama una pikipiki ni sehemu nzr ya kuanzia wakati unazndelea kutafuta kazi..
 
Zifanyie kazi hizo ndoto.

Unapo ota unakula chakula na Mtu fulani, maana yake utapita katika baadhi ya mambo ambayo na yeye alipitia, kama taabu flani na wewe utazipitia hizo taabu, kama ni raha na wewe utapita katika hizo raha.
 
Ndoto zinakuonesha waweza kufika wapi.Ila hazitoshi kama hauzifanyii kazi yaani huna mkakati wowote wa kuzifikia.Anza na hatua ndogo ndogo za kufika kule unakoota kwa kufanya kazi kwa bidii la sivyo unaweza kufa hujafikia hata ndoto moja maishani
 
Mimi si mtalaam wa kutafsiri ndoto,lakini Nina ushauri kwako,iko hivi,ukiota ndoto yoyote ile unapozinduka tu ongea na Mungu wako! Kama in ndoto mbaya ikemee isije ikatokea,kama in nzuri,omba Mungu akubariki itimie! Usiwe na hasira mkuu,omba tu Mungu kwa imani yatatimia!
 
Tazama movie zinaitwa Final Destination 1-6.
Something bad follow you behind,if you neglect it by now problem will be wider by then.
Watch out.
 
Wanajamvi hii ni mara ya pili sasa nakuja kwenu,mimi ni kijana masikini ambaye nina amini ipo siku katika hii mihangaiko yangu nitafanikiwa kimaisha, huwa naota ndoto na %90 huwa zinatokea kweli, miezi mitatu iliyopita niliota pikipiki yangu inaungua moto na kweli jana mida ya saa 12 jioni wakati naifanyia service ilishika moto na kuanza kuungua bahati nzuri nikaiwahi kwa kuizima na maji hivyo haikuharibika, usiku wa kuamkia leo nimeota nipo na rais Kikwete pamoja na mkewe Salma tunakula, hii ikiwa ni mara ya tatu kuota nipo na Kikwete, rais Bush akiwa madarakani niliota zaidi ya mara nne nikiwa naye na mara ya mwisho nikiwa nimekaa naye ndani ya Air Force One, Obama nimeota nipo naye mara mbili, Tony Blair niliota nikiwa naye Israel katika dhifa maalumu, hata Mkapa, Mwinyi nimeota mara nyingi nikiwa nao, napata hasira napoamka asubuhi na kujikuta nipo na shida zangu tu, ndoto hizi zina maana gani kujirudiarudia miaka yote? Wataalamu wa ndoto mnisaidie.
Huun ni ugojwa wa akili unaitwa wa a akili grandiosity., unaweza ukaota wewe ni Rais, Tumia anti-psychotic drags eg Hallopuridol ii may help.
 
Tazama movie zinaitwa Final Destination 1-6.
Something bad follow you behind,if you neglect it by now problem will be wider by then.
Watch out.

hehe, we ndo poyoyo wa mwisho!! muvi imefikaje hapa?

anyways, back to topic...
nadhani mtoa mada unanyemelewa na kaugonjwa ka akili (kama hujawa mgonjwa mpaka sasa).. its as simple as that
 
ili ndoto iwe na maana lazima uwe normal
sio unaumwa au unakunywa dawa za aina fulani ukaota,..hizo ndoto zinakuwa hazina maana
 
hehe, we ndo poyoyo wa mwisho!! muvi imefikaje hapa?

anyways, back to topic...
nadhani mtoa mada unanyemelewa na kaugonjwa ka akili (kama hujawa mgonjwa mpaka sasa).. its as simple as that

Acha kudharau wenzako. Final destination means something about what other ppos think in a normal life. Labda sema hujaiona tyuuu
 
Wanajamvi hii ni mara ya pili sasa nakuja kwenu,mimi ni kijana masikini ambaye nina amini ipo siku katika hii mihangaiko yangu nitafanikiwa kimaisha, huwa naota ndoto na %90 huwa zinatokea kweli, miezi mitatu iliyopita niliota pikipiki yangu inaungua moto na kweli jana mida ya saa 12 jioni wakati naifanyia service ilishika moto na kuanza kuungua bahati nzuri nikaiwahi kwa kuizima na maji hivyo haikuharibika, usiku wa kuamkia leo nimeota nipo na rais Kikwete pamoja na mkewe Salma tunakula, hii ikiwa ni mara ya tatu kuota nipo na Kikwete, rais Bush akiwa madarakani niliota zaidi ya mara nne nikiwa naye na mara ya mwisho nikiwa nimekaa naye ndani ya Air Force One, Obama nimeota nipo naye mara mbili, Tony Blair niliota nikiwa naye Israel katika dhifa maalumu, hata Mkapa, Mwinyi nimeota mara nyingi nikiwa nao, napata hasira napoamka asubuhi na kujikuta nipo na shida zangu tu, ndoto hizi zina maana gani kujirudiarudia miaka yote? Wataalamu wa ndoto mnisaidie.

Hizo Ndoto Zako Zote Zinaonyesha Kuwa Siku Zako Za Kufa Zinakaribia Na Kwamba Utakuwa Masikini Wa Kutupwa Hapa Tanzania.
 
Polesana kijana japo umenichekesha sanaaa lakini jambo kama hili kwamfano nikifahamu umri wako pia huwa ni rahisi kukushauri.
kuna vijarida vingi sana na watu wengi sana wamekuwa wakijiuliza mwaswali kama ya kwako watuwalio bobea katika psychology walitowa majibu yafyuatayo,Ndoto mara nyingi sana hutokana na Mawazo yako ya mchana,Pia usiku kama unaweza kukumbuka umeota saangapi pia kuna muda wa ndoto za matokeo na ndoto za mazingira tuu,na pia wakasema ndoto ni uchovu kwani kunawengine wanaweza kulala na kuanza kuzungumza mambo yamchana kama vili ni mchana.
Sasa basi sio kila ndoto ni ya kupuuzia,mfano unaota wewe umekuwa raisi wa nchifulani wakati unajielewa kabisaa hata darasa lasaba hujamaliza ndio zinakuwa ndoto za abunuasi!!!!!!!!!!
 
Wanajamvi hii ni mara ya pili sasa nakuja kwenu,mimi ni kijana masikini ambaye nina amini ipo siku katika hii mihangaiko yangu nitafanikiwa kimaisha, huwa naota ndoto na %90 huwa zinatokea kweli, miezi mitatu iliyopita niliota pikipiki yangu inaungua moto na kweli jana mida ya saa 12 jioni wakati naifanyia service ilishika moto na kuanza kuungua bahati nzuri nikaiwahi kwa kuizima na maji hivyo haikuharibika, usiku wa kuamkia leo nimeota nipo na rais Kikwete pamoja na mkewe Salma tunakula, hii ikiwa ni mara ya tatu kuota nipo na Kikwete, rais Bush akiwa madarakani niliota zaidi ya mara nne nikiwa naye na mara ya mwisho nikiwa nimekaa naye ndani ya Air Force One, Obama nimeota nipo naye mara mbili, Tony Blair niliota nikiwa naye Israel katika dhifa maalumu, hata Mkapa, Mwinyi nimeota mara nyingi nikiwa nao, napata hasira napoamka asubuhi na kujikuta nipo na shida zangu tu, ndoto hizi zina maana gani kujirudiarudia miaka yote? Wataalamu wa ndoto mnisaidie.

Mkuu; ndoto ni UBATILI tu. Asikuremberembe mtu yeyote humu. Zipuuze kabisa na fanya mambo yako . Tia juhudi ktk kila fursa iliyoko karibu yako na zaid Muombe na kumtegemea Mungu tu.

Mengineyo hayo muachie shetani.
 
Tazama movie zinaitwa Final Destination 1-6.
Something bad follow you behind,if you neglect it by now problem will be wider by then.
Watch out.
hahahahahahahhahaha hiki kizazi cha digital ni shida unampa mtu ushauri based on movie ambayo ni kazi ya fiction.
by the way mleta mada unaonekana una msongo wa mawazo ww piga kazi achana na ndoto
 
Back
Top Bottom