Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,594
- Thread starter
- #61
Hii ni topic ya muhimu sana, i wish watu wangeitolea michango yao mingi na experience tofauti. Kiukweli swala la kufichana mali zilizopo kwenye familia linazidi kushika kasi, kwa lugha nyingine utakuta watu wamekaa kimitego mitego utadhani si wanandoa. mimi sioni sababu ya mume kumficha mkewe mali alizonazo au hata flow ya kipato kwenye familia na especially pale ambapo kuna watoto kwenye familia, mume akifa ghafla mali nyingi ambazo zingesaidia watoto huwa zinakufa huko ziliko, ni mara chache sana kurecover kitu ambacho ulikuwa hujui kama kina exist. Hata wanamama, wanapoamua kuwa na mali binafsi nje ya familia na kuzificha kunatokea same problem kama mtu akifa ghafla, ila experience inaonyesha mara nyingi wanawake ndo victim wa hii ishu maana ndugu wa mume mara nyingi wanamgeuka mara tu anapofiwa na mumewe. Nionavyo mimi, kama unaona mkeo atafaidi sana mali zako na wewe hutaki andika majina ya watoto na iwekwe wazi, ni vizuri pia tukijifunza kutumia wanasheria kutunza wosia wetu katika mambo kama haya kama hatutaki wenza wetu wajue ili zile mali zisijepotea bure kwenye mikono ya wajanja.
Asante Michelle kwa mchango wako. Sina hakika lakini nadhani sheria ya ndoa haiwatambui watoto kama warithi wa mali ya ndoa endapo hakuna wosia. Kwa hiyo kuandika majina ya watoto siyo suluhisho. Bado napendekeza kwanza tujitahidi kuelewa nini kinahusika kama mali za ndoa kwa mujibu wa sheria. Pili tujadiliane na wenzetu. Hakuna njia ya mkato!
Pia nawaonea huruma wanaume wanaojidai kuficha. Endapo Mke akitoa ushahidi kuwa hizo mali zilipatikana kwenye ndoa hata kama ziko sayari nyingine zitapigwa panga 50% by 50%. Kwa hiyo wanawake wajitahidi kufuatialia na kupata nyalaka za mali ambazo waume zao wanajidai kuficha. Hiyo ndiyo dawa yao watu wa namna hiyo!!