Ndoa yangu ipo kimya na imetawaliwa na upweke sana

Mamii ni mapito tu hayo try to spice it up kwa kufanya yale ambayo ulikuwa unayafanya enzi za uchumba au kabla hujapata mtoto. Pengine na mumeo naye analia hivi hivi. Vunjeni ukimya usisubiri akuanze!
 
pole mie ushauri langu lianzishe
kama mumeo yuko kimya,wewe initiate mambo naye atarudisha favour....

kuna mahali nahisi ulimuumiza hisia zake kwa kuropoka au kitu kingine kimemfanya ajidistant himself,jichunguze na usirudie....otherwise vunja ukimya kwa hisani ya watu wa marekani lol
 
NDOA ZOTE ZIPO HIVYO
wewe sasa anza kutafuta hobby na wewe
fuatilia tamthilia kama wenzio..
mpaka aone unamsahau...

The Boss jamani asa yeye akitafuta hobby mbadala na mume naye si atatafuta ya kwake na ndio tunazika ndoa hivyo?! Kuna wanandoa ambao walikuwa kwenye situasion kama hii matokeo yake wana miaka miwili ndani ya ndoa hakuna kugusana! Ni ndoa jina
 
Pole sana dada.. Sasa kama unaona mwenzio yuko kimya wewe usiwe mkimya pia.. Tafuta mbinu mbalimbali za kumchangamsha na kumfanya asiwe mkimya.. You have to be creative ili uboreshe na kufufua hilo penzi lenu... Usichoke dadangu jaribu tene na tena bila kuchoka mwisho wa siku utafurahi mwenyewe..
 
neylu, utundu hausomewi, anaweza tafuta cha kumfurahisha ndo akawa kam-mute kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Ndoa haziko hivyo bana ongea naye mpaka kieleweke, pole sana
 
Kwanini wanawake kila siku hadi tuanzwe? Akiuchuna we lianzishe mama. Vunja ukimya.
 
Mmmmmh!mna2tisha ambao ha2ko bado kwenye ndoa!!kwan ndo zilivyo kweli??
Luluka wala usiogope mdogo wangu mara nyingi wanasema uvumilivu ni kitu muhimu sana kwani kuishi nyumba moja, kushare kila kitu na ile hali ya kujifunza kuwa kitu kimoja si kazi ndogo ati.......Hasa miaka ya mwanzo mwanzo. Wengi wetu uvumilivu darasani tulipata zero na ukiangalia migogoro mingi ya wanandoa hutokea ndani ya miaka miwili mpaka mitano ukiwezavumilia kwa kuamini kuwa ni katika kujuana na kuelewana vema mbona utayashinda?!

Usiogope!
 
Pole sana, inaonekana kuna hali ya mazoea imewaingia wewew na mumeo, kila mmoja anajiona amemzoea saaana mwenzake, kaa nae uzungumze, mkumbushe jinsi ambavyo mlikua mkiongea na na kufurahiana hapo awali, mweleze kua unataka hali hio irudi, then wewe bibie uwe wa kwanza kufanya yale mambo ambayo yalikua yanawapa furaha na uhai katika ndoa yenu, utaona mumeo nae anaanza ku respond postively. Pia angalia kama kuna jambo baya ulimfanyia akapretend kukusamehe, hali hio inaweza kumfanya akawa bado ana kinyongo moyoni.
 
Back
Top Bottom