Ndoa yangu hatarini kuvunjika

Pole sana ila huyo mkeo ni Futuhi kweli ugonjwa tu ndo humsaharishe kiapo chenu cha ndoa wala usihangaike nae we hangaika na kuundoa ugonjwa mwilini mi naudhika sana kwa nini Wabongo tunashindwa kuyaishi MAPENZI YA KWELI tumebaki kushupalia:makalio,hela,weupe,urefu bila kujua hayo mambo yanaweza badilika wakati wowote.Tujaribu kutohoa maudhui kutoka hata kwenye Movies umuhimu wa kumvumilia mwenzio apatapo matatizo haswa haya ambayo sio ya kujitakia.
 
Pole sana mkuu, Mungu akuponye.
Jaribu pia maombi, kama una imani unaweza kupona.
Huyo mwanamke asikupe shida, tena mwambie kabisa kuwa wewe hukuomba huo ugonjwa, kama anaona umeshakuwa mzigo aanze zake, una ndugu, watakutunza.
Nimesikitika sana kusikia wadada huwa wanakimbia ndoa zao kwa ajili ya shida za mume, i.e. ugonjwa, kipato, etc. hii ni tofauti sana na mafikirio yangu. mimi nadhani kipindi ambacho mume anakuwa down ni kipindi kizuri sana cha kuimarisha mahusiano yenu, kuwa karibu sana naye na kumtia moyo. hawa watu siyo ma-superman kama wenyewe wanavyodhani (https://www.jamiiforums.com/mahusia...ume-wa-kweli-a-real-man-tena-wa-kiafrika.html), wanatuhitaji sana katika maisha yao...... bila sisi they are nothing...... mkubali mkatae - habari ndo hiyo
 
Huyo mke, hata kama ukija kupona, nakuhakikishia SI WAKO,!
Pole sana mdau, kuna rafiki yangu humu anaitwa MziziMkavu huyu anaweza kutusaidia kwa namna yoyote!
Naingia kunako maombi kwaajili yako!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana jamani.endelea kuhangaika hujui wapi utafanikiwa.. Huyo wife asikusumbue hajui utu huyo
 
ndugu nimekuwa kwenye ndoa kwa miaka 5 maisha yalikuwa mazuri sana. Tatizo limeanza mwaka mwanzoni pale nilipopata ugonjwa usio eleweka. Ghafla hali ilibadilika maumivu yakianzia kwenye unyao mpaka kiunoni misuli kuvuta ikiambatana na maumivu makali na UUME KUANZA KUINGIA NDANI YAANI KUWA MFUPI NA MGUMU NA MAUMIVU MAKALI YA MGONGO. NIMEPIMA MAGONJWA YOTE YA ZINAA SINA. X - RAY PAMOJA ULTRA SOUND PIA HAKUNA TATIZO. MITISHAMBA NIMETUMIA HAKUNA MABADILIKO NA NGUVU ZINAENDELEA KUPUNGUA MPAKA MKE WANGU AMETISHIA KUONDOKA KAMA MPAKA MWISHO WA MWAKA TAKUWA BADO SIJAPONA. NAOMBENI MSAADA WENU WA MAWAZO NA TIBA

pole sana, mpaka hapo huna mke, una mwanamke tu ndani
 
Hebu tujiulize je ni kweli dhana ya ndoa ni kufanya mapenzi? Jibu ni siyo kweli hata kidogo. Hebu tujiulize tena baada ya kuoana na kuishi kwenye ndoa kwa muda fulani wake au waume zetu wakapata matatizo ya kimaradhi au ajali au mengine ambayo yatawafanya wasiweze kabisa kushiriki jambo hili tutafanyaje? Huenda jibu kwa wale wanaoamini kwamba ndoa maana yake ni kufanya mapenzi watasema kwamba watakwenda nje au kwa wanaume wataoa wake wengine. Huu ni ujinga mkubwa mno kwani tunaweza kufanya hivyo ikiwa ni wenzetu waliopata matatizo lakini kama ni sisi tutaona inavyoumiza.

Tendo la ndoa katika ndoa ni muhimu na kwa kiasi cha kutosha husaidia pia kuimarisha uhusiano. Lakini pale kunapokuwa na tatizo kwenye suala hilo ndipo hapo upendo unapopimwa kama ni wa dhati, bandia, au upendo wa kimradi. Kama upendo wetu ni wa dhati tutajitahidi kuangalia mazingira ambayo huenda yatawafanya hao wenzetu wawe kama walivyo. Tunapojadili kwa upendo udhaifu fulani ni wazi tutawapa wengine nguvu ya kujikagua na kuzidisha upendo kwetu.
11.jpg

Lakini tunapokuwa wakali na kulaumu au kuchukia na kulaani tutawafanya wenzetu wajione wanyonge na pia tutawafanya au kuwapa nafasi ya kuhalalisha kwamba huenda sisi tumetawaliwa sana na tamaa ya kimwili kuliko uwezo wa kufikiri kiasi kwamba linapotokea tatizo tunakuwa vichaa na hivyo uwezekano wa kutoka nje au kuvuruga ndoa ni mkubwa. tujifunze kufahamu na kukubali ukweli kwamba ndoa bora na imara hazifanywi hivyo na tendo la ndoa, bali hufanywa hivyo na wanandoa kusaidia kutatua kila tatizo linalotokea.

Ni vizuri tukawa wazi kusema matatizo tunayohisi kwa wenzetu badala ya kuhisi tu na kudhani watayaona. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeshindwa jukumu letu la kupenda kwani tutakuwa tumejitazama wenyewe zaidi..
 
Pole sana kwa yanayoendelea. omba Mungu atakusaidia na jaribu kuonana na madaktari. Ila isiende kwa hao toboa tobo.
Mimi naona huyo mama hakufai hata ukipona. aliapa kuwa na wewe kwa uzima au ugonjwa, kwa shida na raha sasa anakupa altimatum. Hafai kabisa
 
Is any one of you in trouble? He should pray. Is anyone happy? Let him sing songs of praise. Is any one of you sick? He should call the elders of the church to pray over him and anoint him with oil in the name of the Lord. And the prayer offered in faith will make the sick person well; the Lord will raise him up. If he has sinned, he will be forgiven. Therefore confess your sins to each other and pray for each other so that you may be healed. The prayer of a righteous man is powerful and effective. Elijah was a man just like us. He prayed earnestly that it would not rain, and it did not rain on the land for three and a half years. (James 5:13-18)
 
Litupe jf doctors utapata ushauri mzuri, wasomi madaktari wakishindwa jaribu pia kienyeji, mambo haya yapo!
 
jamani pole sana my dear! nimekuonea huruma wallah! sikiliza ushauri huko juu, MUNGU NI MWEMA ATAKUPONYA!

Jamani Cacico naomba tuu urudishe ile avator yako ya macho pleaseeeeeeee...!
 
Nenda ukafanyiwe MAOMBI

Kwa Mungu Hakuna linsilowezekana, ila tu Vigezo na Masharti kuzingatiwa
 
kamanda pole sana mungu atakujaalia utapona..ila "kama hospital wanasema hawaoni tatizo" nenda kwa "wataalamu" wa tiba asili..waswahili walisema kikulacho mara nyingi huwa kiko nguoni mwako...kama upo dar panda basi nenda kibaha kwa mfipa kuna mtaalamu maeneo hayo naamini atakusaidia sana.

Mkuu WC? hebu mpatie number au jina na namna ya kufika huko kwa mtaalam. Unaweza mp maana kweli hali hii ni tete.
 
Tatizo watu wanaoa "wake maslahi" how on earth unaweza kumuacha mume ulompenda kisa umekosa sex. Atakuwa amepata sababu tu hakukuwa na love at first place.

aisee magonjwa yapo mengi sana duniani...wanawake wachache sana katika 100 ni 1 tu ndio anaweza kuvumilia matatizo yanapotokea..ila cha msingi msihi asiondoke maana hujapenda kuugua na kama akilazimisha kuondoka let her go...wewe angalia matibabu ukipona wapo weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeengi sana
 
Mtambuzi kwa hili mimi naomba niwatetee wanawake...wengi ni wavumilivu; wengi wanaishi na wanaume wenye visukari na BP ambao perfomance zao ni karibu na zero.

Ila kwa wanaume...mke akiwa mjamzito tu akakosa k miezi miwili ameshatoka nje (most of you)
Ndio maana hapa watu wanashangaa huyu ni mke wa aina gani kwani wake wengi wanakubali kuishi na wagonjwa mpaka kifo kiwatenge.

Back
Top Bottom