Ndoa Yangu haina mapenzi

ngonzi zomukama

Senior Member
Apr 13, 2010
170
5
najisikia kumchoka mwenzangu bila sbbu yuko sawa kila k2 ila sina ham naye tena kama zamani tulipokuwa wachumba najitahidi nashindwa sina nyumba ndogo ila natamani wakti mwingine ila cjawahi fanya ila mwenzangu wa ndoa nimechoka kabisa hajanikosea haja badilika ila nahisi kumchoka nisaidieni nifanyeje jamani?
 
Umekuja na kasi mbaya sana bingwa!, post ya 2 unataka kummwaga mtu?
Tulia kaka tukupe ushauri mzuri...mwache shemegi bana!
 
UNAHITAJI MAOMBI
Unamchoka mtu bila sababu jamani, pole sana sali sana Mungu akusaidie
 
Kwanza hujaeleza mmeishi kwa muda gani, na kama mna watoto, wangapi!
Lakini hiyo nyumba yenu inaonyesha ni ya wachovu, maana hamna ubunifu wowote unaozaliwa hapo chumbani kwenu, mmefanya mbuzi kagoma weeeee, na sasa hamtaki staili zingine, kunani?
 
@PJ mie hudhani uvivu wa kuwa wabunifu ni kwenye sector za maendeleo tu kumbe mpaka za chumbani??? Kazi ipo kwa kweli!!!
 
Hiyo roho ya chuki ISHINDWE KABISA. Hiyo ni roho ya uharibifu.....kwa nini ndugu umchukie mke wako bila sababu, TAFAKARI, ZINDUKA NA CHUKUA HATUA. Mungu anachukia kuachana
 
Ndugu yangu hata kama utaachana naye na kuchukua mwingine itakuwa hivyo hivyo tu baada ya muda mfupi japo sijui mmeishi muda gani. Dawa ni kutafuta chanzo cha kuchokana baada ya hapo rekebisha mambo. Inawezekana kuna monotony ya aina fulani imewachosha. Nakuhakikishia mwanamke ni matunzo. Mpende, mlishe vizuri, mvishe vizuri, outing mara kwa mara sio mpaka sikukuu, style za majambo nazo ziwe zinabadilika kuongeza ladha, unaweza kumfundisha kwa kumletea vitabu/magazeti/miziki mbalimbali lengo nikuondoa ile kujisikia mpweke. Nakuhakikishia ukimjali mkeo nae atakujali na mtaishi vizuri. Pamoja na yote niliyoeleza kwa kila jambo mtangulizeni Mungu mbele.
 
najisikia kumchoka mwenzangu bila sbbu yuko sawa kila k2 ila sina ham naye tena kama zamani tulipokuwa wachumba najitahidi nashindwa sina nyumba ndogo ila natamani wakti mwingine ila cjawahi fanya ila mwenzangu wa ndoa nimechoka kabisa hajanikosea haja badilika ila nahisi kumchoka nisaidieni nifanyeje jamani?

DUH..bila sababu??

jaribuni kujipa 'break'...mmoja asafiri,mkae mbali....msionane kwa kipindi...mkija kuonana mtakuwa 'mmemisiana' vya kutosha....

au,jaribuni kutoka wote holiday muende nje ya mji,na kujikumbushia mambo mliyofanya honeymoon km mlikuwa nayo...LOL,hii itawasaidia kubadilisha mazingira!

aah...hivyo hivyo tu...!!!
 
Mkuu,

Tatizo lako si la mmoja. Yawezekana wanaoandika hapa wanaandika bila kujua umeathirika vipi kisaikolojia.

Mimi ni mtu mwenye ndoa na ningependa nikushauri kwa ninavyoona inafaa (kama ninavyoiishi ndoa yangu).

Mosi; popote penye tatizo pana chanzo. Hujatufahamisha chanzo cha wewe kumchoka ni kipi, unakijua lakini inaelekea imekuwa ngumu kukiweka bayana, ingekuwa rahisi kwetu kuweza kukushauri kulingana na chanzo cha tatizo.

Pili; kuchokana kwenye ndoa kunatokana na mambo mengi, yawezekana mwenzi wako amebeba ujauzito au kajifungua hivyo yuko kwenye kipindi kigumu kimatamanio, hapa unatakiwa kumvumilia, ni kipindi cha mpito. Yawezekana unamhisi mwenzio kuwa na mahusiano na mtu/watu kitu ambacho ni obvious mapenzi kwako pia yatashuka. Yawezekana pia wewe binafsi umeruhusu mambo ambayo unajua wazi kuwa yatapunguza mapenzi yenu. Ukifanya kazi muda mrefu bila kupumzika ni wazi hata mwili unachoka na unajikuta una muda mdogo sana wa kuwa na mwenzi wako, unaanza kupoteza hamu nae.

Tatu; kama mmefunga ndoa kihalali; kumbuka ahadi zenu za ndoa, ulisema utampenda katika shida na raha, huu ndio wakati wa shida, unatakiwa kuitekeleza ahadi yako sasa! Lakini pia, hata kama hamjafunga ndoa kihalali ila mnaishi kama mme na mke; lazima kuna kitu kiliwafanya mkafikia maamuzi haya, hamkulazimishwa na mtu. Uliona katika viumbe wote huyo ndiye anafaa kuwa mwandani wako; kabla hata ya kutueleza ulitakiwa kuwa umeyaongea na mwenzi wako na kutafuta suluhu ya matatizo yenu.

Mkuu; ndoa ni tamu sana, ina raha mno! Inahitaji kuelewa kuwa mapenzi huchochewa ili yaendelee kukua na kuchanua, wewe ndiye unatakiwa sasa baada ya kubaini kuwa umepungukiwa mapenzi kujifunza ni kipi kizuri kwa mwenzi wako na kuhakikisha unakuwa unakiona kila wakati. Sitaki kuamini ulimpenda sababu ya sura au maumbile tu; kuna mvuto flani ulikupeleka kwake. Pata muda, mwende nje ya maeneo yenu mnapoishi (outing) mkakae na kujaribu kula vilivyopikwa na wengine huku mkifurahia pamoja; jaribu kuilazimisha furaha ikibidi lakini hatma yake utagundua tofauti.

Yawezekana pia chanzo ni kubadilika tabia kwa mwenzi wako na unamfichia siri; hapo ndipo pia unatakiwa kumweleza katika faragha juu ya tatizo lake. Usimweleze kwa kumgombeza au kwa sauti kubwa; kuwa na hekima, mwambie polepole huku ukimweleza unampenda kiasi gani na mabadiliko unayoyaona yanavyokuathiri sana mpaka kupoteza hamu yako kimapenzi kwake.

Mkuu, naweza kuandika mengi lakini bila kujua chanzo inakuwa ni kumpigia mbuzi gitaa, hebu kuwa wazi kidogo tuinusuru ndoa yako, ni ya thamani kwako na thamani kwetu pia kwani mkiparana, wanaoumia ni watoto ambao huenda wakahangaika mitaani na watakaokutana nao ni sisi (Jamii).

Ahsante
 
Kwanza hujaeleza mmeishi kwa muda gani, na kama mna watoto, wangapi!
Lakini hiyo nyumba yenu inaonyesha ni ya wachovu, maana hamna ubunifu wowote unaozaliwa hapo chumbani kwenu, mmefanya mbuzi kagoma weeeee, na sasa hamtaki staili zingine, kunani?

Kaka PakaJimmy, hiyo staili ya mbuzi kagoma kwenda si ilimuua MC mmoja huko kanda ya kaskazini, unataka huyu kaka naye arudi kwa Muumbaji wake? Naona tumshauri huyu kijana aende kumuona mtaalamu wa saikologia atamsaidia.
 
najisikia kumchoka mwenzangu bila sbbu yuko sawa kila k2 ila sina ham naye tena kama zamani tulipokuwa wachumba najitahidi nashindwa sina nyumba ndogo ila natamani wakti mwingine ila cjawahi fanya ila mwenzangu wa ndoa nimechoka kabisa hajanikosea haja badilika ila nahisi kumchoka nisaidieni nifanyeje jamani?
katembelee nyumba ambazo wanaume wanaekwa kibano na wake zao. hii itakusaidia kuweka sawa saikolojia yako ambayo inaonekana ipo antiklokwise.
 
ila, ila , ila ,ila zimejaa thread nzima?!!

una lako jambo we sema kama humtaki, hakika nakwambia hata kutangulizana na mpenzi wako huyo huwezi.

sema kinachokusumbua tukusaidie
 
Acha maskhara kaka kwani huyo mke ulilazimishwa kumuoa na familia yenu...unafikiri ndoa ni mchezo wa kuigiza. Mbona hujachoka kuishi kama wewe ni bingwa wa kuchoka.
 
Kwanza hujaeleza mmeishi kwa muda gani, na kama mna watoto, wangapi!
Lakini hiyo nyumba yenu inaonyesha ni ya wachovu, maana hamna ubunifu wowote unaozaliwa hapo chumbani kwenu, mmefanya mbuzi kagoma weeeee, na sasa hamtaki staili zingine, kunani?

Mbona ile ya staili ya dirishani ambayo ndio kiboko kupita zote hujampa huo ubunifu...PJ acha uchoyo bana...
 
najisikia kumchoka mwenzangu bila sbbu yuko sawa kila k2 ila sina ham naye tena kama zamani tulipokuwa wachumba najitahidi nashindwa sina nyumba ndogo ila natamani wakti mwingine ila cjawahi fanya ila mwenzangu wa ndoa nimechoka kabisa hajanikosea haja badilika ila nahisi kumchoka nisaidieni nifanyeje jamani?
we zomukama usituyayushe,we umeshapata kicheche huko nje sasa mara oooh natamani kuwa na nyumba ndogo....ila sijawahi.;
1.Wanawake hubadilika kimaumbile,baada ya kuzaa na kuanza kulea nahisi tayari mna watoto.
2.Tatizo lako ni hao vicheche unaowaza waza nje,hawaishi hao toka enzi hizo.
3.Kama si pepo mbaya ulie nae basi ulifanya kosa kuoa mtu ambae hukumpenda,ndio hukumpenda ulimtamani tu,umecheza mechiiiiiiiiii,umefunga magoliiiiii sasa humpendi tena USHINDWE.
4.Fanya fasta mwombe mungu akusaidie,pepolikutoke na mawazo ya kutamani vya nje yasiwepo.
 
Life is how you make it. Usione vyaelea, vyaundwa!
Mgharimikie mkeo yaani mvishe, mtembeze, mtafutie safari mf. aende kusalimia kijijini, akikaa wk 3, utakuwa na hamu ya kumwona kama vile ndo unamuoa.

Matatizo haya yanatokea kwa sababu muko wote mara kwa mara, hakuna ubunifu wa kufurahishana, kufikiria umfanyie nini mke wako kitu kizuri kwani ukiona wake wa wenzio wanapendeza jua kuwa wenye nao wanachukua hatua ili hayo yasitokee.

Uchaji Mungu ukipungua pia ni tatizo. Yawezekana hilo ni pepo hivyo ulishughurikie ki-imani.
 
nimekuelewa ahsante nitafanya hayo

Back
Top Bottom