Ndoa yako ifanye kuwa ya furaha na upendo

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by bemg, Jul 25, 2012.

 1. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,704
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyakatihizi kuna hatari kwenye ndoa za watu kutokuaminiana, usaliti umekuwa mkubwa mnokuliko wakati mwingine wowote.Waume hawashikiki kwa vischana vinavyoonyeshakifua kimejaa embe mbili , wake nao hawakamati kwa wanaume wenye mshiko na wasiona mshiko ili hali ni kuvutwa na kila tamaa ya mwili na dunia na shetani wa uzinifu .vilio kwenye ndoa ni vingi mno kuliko hata tunavyolia na majanga mengine ya kitaifa. Ukatali kwenye ndoa unazidi kukua kwa sababu ndoa nyingi hazijajengwa kwa misingi imara ya kujua neno la Mungu.Hii ni hatari sana kwa wanandoa wanaoishi bila kuifanya ndoa yao imjue Mungu na matakwa yake kwa wanandoa.Ifanye ndoa yako kuwa mpya na yenye furaha kila siku utaona matokeo yake na mtastawi kwa kila kitu......................... mikwaruzano haitakuwepo..........mtasharikiana kwa kila jambo............hakutakuwa na kufanya mambo kisirisiri................hautaweza kusaidia ndugu zako au rafiki zako kisirisir............hautawaza wanaume au wanawake wa barabarani....................

  Ndoa nimpango wa Mungu tangu alipomuumba Eva kwa ajili ya Adamu.Ndiyo maana mwanamumehumwacha baba yake na mama yake akambatana na mkewe nao wawili huwa mwilimmoja.Ndoanyingi za kikristo zimekuwa na matatizo mengi kwa sababu hazikujengwa kwenyemsingi mzuri wa neno la Mungu.Na mara nyingi tatizo linalonekana ni masuala yapesa na mambo mengine ya kinyumba.Kwa mfano yawezekana uko kwenye ndoa, nikweli wewe ni mwanamume mwenye uwezo wa fedha, wengine wanawanunulia magari aukuwafanyia mambo mazuri wake zao lakini wewe humfanyii hivyo mke wako. Hata kwa wanawake pia, wapo ambao wamekuwa wakiwafanyia yaliyomazuri waume zao hasa kwa kuwapa fedha na kadhalika, lakini wanashindwakufahamu kuwa suala la kula vizuri au fedha siyo vitu muhimu kwa wanandoa.

  Lamuhimu katika ndoa ni kuishi kwa upendo na amani na pia kuangalia pandezote, kwa mfano kama ni kweli uko sawa kwenye sualala fedha, unapaswa kuangalia pia katika suala la mahusiano na mahaba kwaujumla, je, kama mwanamume, una uwezo wa kushughulika kama ambavyo mwanamumeanapaswa vilevile na mwanamke ana uwezo wa kushughulika kama ambavyomwanamke anapaswa.

  Jambola msingi kwa wanandoa kupenda kuwa na mazungumzo ya wazi huku mkiwa na shinaimara katika Neno la Mungu. Eeh hata nyumbani,utakuta Pia mke usipende kumuachia housegirl kila kazi za kumtunza mme wako na watoto wako.Ni wajibu wako mwanamkekuhakikisha mumewe wako anajisikia raha kuwa na wewe na hakukosea kukuoa na hana sababu ya kutembea nje ya ndoa kwa sababu roho yake itakuwa imetulizwana mahaba yako.Lakinini vizuri wakati fulani kumuuliza unaonaje leo nikakupikia chapati, viazi,tambi na kadhalika.Pia wanaume utakuta wanaendamatembezi bila kumjulisha mke wake na akirudi akiulizwa ulikuwa wapi eeheanakuwa mkali kama nyati aliyekosa malisho kwenye mbunga ya Masai Mara.

  naweza k
  Maranyingi wana ndoa wamejikuta kila mtu anafanya mambo yake bila kumshirikishamwenzake kwa kukosa uaminifu kati yao.Unaweza kufanya kitu ukafikiriunatengeneza, kumbe unaharibu. Mpendwa tuzifanye ndoa zetu kuwa zenye upendo na salama nyingi.Kitu muhimu kwenye ndoa ni kuwa na upendo maana upendo uvumilia yote shida na raha,hauhesabu mabaya.Mara nyingi watu wana pokuwa kwenye hatua ya uchumba huwa wanaupendo usiokuwa na kifani lakini wengi wanashindwa kuendelea kuutuza upendo huopindi wanapoanza maisha ya ndoa.Mtume Paulo aliandika juu ya upendo katikabarua yake ya kwanza kwa wakorintho akisema ''Mwenyeupendo huvumilia,hufadhili, mwenye upendo hana wivu, hajidai, walahajivuni.Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hanawepesi wa hasira, haweki kumbukumbu ya mabaya, hafurahii uovu, bali hurahiaukweli.Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote na hustahimili yote.Upendo hauna kikomo kamwe(1Korintho13:4-8)’

  ’Kuna baraka katika maisha ya ndoa kama wanandoa wakiishi pamoja kwa upendo na kama ndugu na mwili mmoja. Kwa mwanamke anayemtii mume
  wake anaweza kubadili mwenendo wa mumewe kama mwanamume huyo hajaamini neno la Mungu kwa kuona mwenendo wa mkewe ukiwasafi. Na kwa wanaume wanaowatendea wake zao kwa heshima watapokea zawadi ya uhai anaowapeni Mungu napia sala zao hazitatiliwa kizuizi na Mungu.
  Kwa wanaotafuta wa chumba nilazima utafute mwenzi ambaye hamtofautiani interest na itapendeza kama kumpata mwenzi mcha Mungu na wote muwe wenye imani inayofanana na kama haifanani mmoja wenu akubali kufuata imani ya mwenzake kwa kuishika na kutenda kama inavyoelekeza.Pia acha tabia ya kutest kwanza kabla ya ndoa hiyo hupunguza upendo wakati mtakapoanza kuishi pamoja utaona kama tena hufurahishwi na penzi la mwenzi wako.

  Jenga ndoa yako katika Msingi wa upendo na kumcha Mungu

   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,709
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ameeeen.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,120
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 38
  God bless
   
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 38
  Asante kwa neno!
   
 5. j

  jupeka Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuru kwa ushauri wako
   
 6. l

  luku_77 JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dah niko hapa kwa mwezi mmoja sijaona post kama hii, imenivutia sana maana mii natarajia kuingia kwenye ndoa mda sii mrefu, nafikiri umeniongezea kitu ambacho sikukitilia maanani sana be4.»»» mungu akulide ili siku nyingine uelewa wako juu ya unachokiamini uwafikishie na wengine. nakutakia siku njema.
   
 7. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 926
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 18
  Be blessed!!!
   
 8. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,704
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ubarikiwe
   
 9. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,704
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante na Mungu akutangulie katika kila hatua uliyonayo ili mwenzi wako utakayeishi naye awe ni tulizo halisi la moyo wako naye akufurahie siku zote za maisha yenu.Kitu muhimu ni kujua kuna majaribu mengi mno kwa wanandoa na majaribu haya yakupasa kuyashinda kwa kumcha Mungu na kwa kujitahid kuifanya kila jambo kwa ushirikiano na kusikiliza mawazo ya kila mmoja wenu.Maneno kama dear nataka tufanye hiki au kile ni mazuri sana kwa wanandoa.Pia usiache kutumia maneno kama haya kila siku sweet, honey, missing you, i love you,pole mpenzi, wewe ni mrembo,wewe ni handsome, ninabahati ya kuwa na mme/mke kama wewe na mengine yenye kuonyesha hisia za mapenzi na kuthaminiana na mwenzi wako
  Ubarikiwe sana
   
 10. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,704
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks.you too
   
 11. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,704
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana
   
 12. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,704
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana na ufurahie mke wa ujana wako
   
 13. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,704
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amen.Stay blessed
   
 14. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,704
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks.Blessed
   
 15. M

  MASABURI Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana naamini nimepata jambo...mkuu
   
 16. k

  kbz Member

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana na ubarikiwe nimejifunza kitu Asubuhi ya leo
  kazi njema
   
 17. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,704
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante Kbz.Mungu azidi kukubariki kwa kila kitu
   
 18. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,704
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ubarikiwe na tuzidi kujifunza na kuyafanyia kazi ili tuwe na ndoa zilizo na upendo na jamii yetu itapona na wimbi la maumivu katika ndoa
   

Share This Page