Ndoa ya sambaratika few days before..............

Sinai

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
288
47
:msela::msela:Kuna jambo limetokea hapa mtaani kwetu jana. Kuna kijana mmoja ambaye kwa kweli alikuwa anajulikana kama mtu wa vimwana sana, ikafika wakati akataka kumwoa tena kwa ndoa mtoto wa mchungaji wa kanisa moja la Moroviani. Wazazi wa binti wakatoa sharti kuwa binti yao hawezi kuolewa hadi pale watakapo pima afya wote wawili kwa pamoja. Kijana hakuwa tayari, pengine kutokana na mienendo yake kuwa ya ovyo, lkn wazazi wa binti wakaforce kwa kuamini kwamba binti yao ni virgin, hivyo hana tatizo lolote! Baada ya mjadala mrefu, jana wakaamua kupima, majibu yakaonyesha binti ambaye wazazi wake wanaamini ni virgin ana HIV + na kijana yupo safi, tena baada ya kupima mara mbili ktk hospitali tofauti ikiwemo ya mkoa!!!!!!

Ndoa ilikuwa ifungwe jumamosi tarehe 12/02/2011. Sasa kijana ameamua kuachana na binti, na binti ameamua kunywa dawa za kutoa uhai, lkn hadi naandika hapa, bado kalazwa hosp. na hali yake sio nzuri, drip sita kesha maliza. Hapo nani alaumiwe? Wazazi wa binti au kijana? Je ni vizuri wazazi kumwamini binti kupita kiasi? Binti anamiaka 26, eti bado wazazi wanaamini kuwa bado hajawahi ku-do, ktk ulimwengu wa sasa lnawezekana hiyo? Nawakilisha!:msela::msela:
 
mnh na ndoa za siku hizi zinavyofungwa baada ya watu kuridhishana kitandani vya kutosha??? mie siamini huyo kaka haku-do na huyo dada!!! akapime tena HIV lol,afu kama ya kutunga vile....:laugh::laugh::laugh:
 
mnh na ndoa za siku hizi zinavyofungwa baada ya watu kuridhishana kitandani vya kutosha??? mie siamini huyo kaka haku-do na huyo dada!!! akapime tena HIV lol,afu kama ya kutunga vile....:laugh::laugh::laugh:
hata kama ali kudo na huyo bindti kama alitake precautions, chanses za kuambukizwa kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume ni ndogo ikiwa michubuko kwa upande wa mwanaume haikutokea.
 
:clap2::clap2:Hiyo ni true issue! Tena ni jana tu imetokea wala sio ya kutunga! Sijajua kama jamaa haku-do au la!! :clap2::clap2:
 
Sio suala la nani alaumiwe.. kwa siku hizi kabla ya ndoa ni lazima kupima HIV. na kukutwa na HIV si kusema si bikira pengine kaupata kwa njia nyingine, tunamuombea apone Mungu amsamehe.
 
Huenda kweli walishawahi kufanya mapenzi,lakini siku hizi kesi za discordant couples zimesheheni yaani kati ya wenza wawili kwenye mahusiano mmoja anakua +ve mwingine anakuwa negativ,actually tafiti nyingi zinaendelea duniani kujaribu kujua kwa nini inatokea hivi ili labda jibu lake litoe ufunguo wa kupata dawa ya kuzuia maambukizi ya HIV. Yote kwa yote inawezekana pia hawajawahi kulalana.Swali langu hapa ni je kwa nini kijana na binti walipinwa HIV bila kufanyiwa counselling kwanza,ethics zinakataza kumpima au kumpa mtu majibu bila counselling na no wonder binti kabugia sumu,Mungu amsaidie apone apewe ushauri nasaha na ataishi vizuri na who knows mbele ya safari anaweza kumpata mwenza tena mwenye HIV na bado wakaoana na kupata mtoto ambaye ni HIV free.
 
Ndio wakati wa kuonesha mapenzi ya dhati kwa kufunga ndoa na waishi pamoja,nachoka kusikia mapenzi ya kubeep yaani watu siku hizi wanapendana kwenye raha tu,ikitokea shida basi mapenzi yanapotea
 
da! Umenikumbusha mwalimu wangu wa kiswahili forodhani mwaka 2000,,,,,,,,,,, umdhaniye ndiye kumbe.......
 
Duh hii imekaa vibaya ila kwa hawa watu ambao ni wahuni kama huyo kaka always wanatumia kinga hawamwamini mtu. so ni wazi huyo kaka ni mtumiaji mzuri wa kinga.
 
Sijaelewa sababu za kunywa sumu, ni kuwa na ukimwi au aibu kwa mchumba? mbona yuko kizamani hivyo
 
Stori ya kutunga hii !
Kwanza huwezi kuiita ni ndoa wakati ndo kwanza walikuwa wanataraji kufunga ndoa.. ungesema Uchumba wasambaratika few days before ungeeleweka...

Halafu kwa system ya sasa asilimia 75 watu wanafunga ndoa wenzi wao wakiwa tayari wana ujauzito na kwa jinsi ulivyomtaja jamaa kwamba ni mutu ya totoz haiwezekani asichakachue...

Hizi hadith mconsult Shingongo kwanza kabla hujazileta huku..
 
Ndio wakati wa kuonesha mapenzi ya dhati kwa kufunga ndoa na waishi pamoja,nachoka kusikia mapenzi ya kubeep yaani watu siku hizi wanapendana kwenye raha tu,ikitokea shida basi mapenzi yanapotea

Joseph!!! to honest ingekuwa wewe ungekubali kumuoa?? ama kwa kuwa limetokea kwa mwenzio???
 
Back
Top Bottom