Ndoa ya Obama

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,833
155,780
'Ndoa ya Obama Ilikuwa Chupu Chupu Kuvunjika Mwaka 2000'
2197922.jpg

Rais Obama na Mkewe enzi zao za ujana

Imegundulika kuwa ndoa ya rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle ilikuwa kwenye mashaka ya kuvunjika mwaka 2000 baada ya Obama kupigwa mwereka kwenye uchaguzi wa kongresi. Kwa mujibu kitabu cha "Renegade: The Making of a President" cha mwandishi wa Marekani Richard Wolffe, rais Obama mnapo mwaka 2000 ilimbidi atenge muda wa kuokoa ndoa yake baada ya mashaka makubwa kuingia kwenye ndoa hiyo kufuatia Obama kupigwa mwereka kwenye uchaguzi wa Kongresi.

Michelle alikuwa akimlaumu Obama kwa ubinafsi kwa kujali sana mambo ya siasa na kutumia muda wake mwingi kwenye siasa badala ya familia yake.

Obama naye alikuwa akimlaumu Michelle kwa kuwa mtu baridi na kutokuwa karibu naye kwenye mambo yake.

"Katika kipindi hicho mapenzi yalipungua na kulikuwa hakuna maelewano mazuri" kilisema kitabu hicho. Inasemekana kwamba wapenzi hao walikuwa hawakai pamoja kupiga stori karibia mwaka mzima kutokana na mgogoro huo.

Uchachu huo katika ndoa hiyo ulitokea kipindi ambacho mtoto wao wa mwisho Sasha alizaliwa.

"Michelle alikuwa akiona siasa ni kama mchezo wa kupoteza muda tu" kilisema kitabu hicho.

Utulivu ulirudi katika ndoa yao baada ya Obama kuchaguliwa kuwa seneta mwaka 2004.
 
ndivyo walivyo wanawake wengi.''aliona siasa ni mchezo wa kupoteza mda''

sasa anajisikiaje kuwa white house!!!

hali hii hutokea sana ktk familia nyingi.
 
Inataka uvumilivu ili kupata mafanikio mkubwa in life.Lakini mara nyingi kina mama wanataka mambo fastafasta. Kwa mfani hapo bongo, wengi wa kina dada zetu wanataka ukioa tu hapohapo uwe na gari la kifahari, nyumba kubwa, bia unakunywa savana au level 8 etc etc, then you are the man..Kwikwikwi..I just joke
 
Hakuna ndoa isiyokuwa na highs and lows jamani.Sababu za lows zinaweza kuwa nyingi tu - kuanzia kutokuwa na muda na familia kwa sababu yeyote ile, kukosa uaminifu,kukosekana kipato cha kutosha, maradhi,migogoro ya ndugu, mitafaruku isababishwayo na malezi ya watoto, n.k. Sasa nani kasema akina Obama ni Malaika?
Let them live their life as any other married couple with their highs and lows!
 
bravo sis, umenena sawia! cdhani kama kuna mtu anaeweza kusema kwenye ndoa yake hakuna hizo highs na lows, zinatokea sana na ndio hapo wanandoa msipokuwa makini/wavumilivu ndoa inajifia.
 
Hakuna ndoa isiyokuwa na highs and lows jamani.Sababu za lows zinaweza kuwa nyingi tu - kuanzia kutokuwa na muda na familia kwa sababu yeyote ile, kukosa uaminifu,kukosekana kipato cha kutosha, maradhi,migogoro ya ndugu, mitafaruku isababishwayo na malezi ya watoto, n.k. Sasa nani kasema akina Obama ni Malaika?
Let them live their life as any other married couple with their highs and lows!

Asante mkuu, maisha ndivyo yalivyo, sina la kuongeza!
 
...Sasa hivi wifey anauza tu sura duniani bila kokoro wala nini, hakuna cha complain wala baba yake complain. Du kweli black women wana mambo wakiridhika.
 
Michelle inawezekana kabisa hakuwa ameelewa siasa ina ulaji ila kushinda kunahitaji kusaidiana mbona urais alisaidia na wakawa wanapambania ikulu kwa umoja
 
Siasa ni mbaya sana maana unaweza ukajitenga na familia kama Hii kampeni yake obama kama si alikuwa nae Michelle full time duuu balaa maana almost 2 yrs jamaa anazunguka tuu.....hakujua nini maana ya siasa na jinsi gani unatakiwa ku saidia mumeo kwenye kampeni labda.........
 
Hakuna ndoa isiyokuwa na highs and lows jamani.Sababu za lows zinaweza kuwa nyingi tu - kuanzia kutokuwa na muda na familia kwa sababu yeyote ile, kukosa uaminifu,kukosekana kipato cha kutosha, maradhi,migogoro ya ndugu, mitafaruku isababishwayo na malezi ya watoto, n.k. Sasa nani kasema akina Obama ni Malaika?
Let them live their life as any other married couple with their highs and lows!

WoS, you said it all. You always inspire me with your substances!!! Asante.

Wakuu kwa maisha ya ndoa kila siku ijayo na kupita ni kumshukuru Mungu kwani siku hiyo na tarehe hiyo hutakaa uione tena,, itabaki kuwa kumbukumbu. Kinachotakiwa ni kujaribu kwa pande zote kuweka historia nzuri (your marriage past)!! Ndoa si lelemama!! Ni kazi nzito!!! I pray for my 50th Marriage aniversary(kwa mtiririko wa Bronze, Silver, Golden and Diamond jubilees) !!!!! Ni kazi kubwa hapo wakuu!!
 
Mkuu Maane,
hii post yako imejaa maneno ya hekima na busara za kutosha.... laiti ambao hawajaingia au wanaotarajia kuingia kwenye ndoa wangepata fursa kupita humu na kujichotea hazina hii isiyooza ikawasaidie huko mbele ya safari.KWELI! NDOA NI NDOANO - yahitaji subira vinginevyo ukijaribu kujinasua kwa hamaki na papara utararuka vipande vipande!
 
wanawake bana........ukiishiwa nao wanasepa.........

wewe YY!
tusihukumu jumlajumla... hata hapahapa JF ingekuwa inawezekana kupata shuhuda za wanawake walioshikana na waume zao kwenye shida ungeona kuwa sio wote wanasepa kama unavyosema.Hata Michele alichokuwa analalamikia ni kumkosa mume na baba wa watoto wake na siyo kuishiwa.
 
...simlaumu Michelle Obama, mwaka 2007 tu hapo wengi wetu hatukuwahi kufikiria mwaka mmoja baadae Marekani ingepata rais mwenye asili ya Africa.
 
wewe YY!
tusihukumu jumlajumla... hata hapahapa JF ingekuwa inawezekana kupata shuhuda za wanawake walioshikana na waume zao kwenye shida ungeona kuwa sio wote wanasepa kama unavyosema.Hata Michele alichokuwa analalamikia ni kumkosa mume na baba wa watoto wake na siyo kuishiwa.

WoS:

Wakati mwingine Wamarekani weusi wameshaweka limitation zao. Inawezekana Michelle was content na walivyonavyo.
Na wakati Obama aliona sky is the limit.
 
wewe YY!
tusihukumu jumlajumla... hata hapahapa JF ingekuwa inawezekana kupata shuhuda za wanawake walioshikana na waume zao kwenye shida ungeona kuwa sio wote wanasepa kama unavyosema.Hata Michele alichokuwa analalamikia ni kumkosa mume na baba wa watoto wake na siyo kuishiwa.
iam sorry....labda kosa langu ni kuishi katika ki statistics sana.....too much approximation lakini ukweli unabaki pale pale.....more than 60 ya wanawake ukiishiwa wananuna na kusepa ukizubaa masela wanakusaidia.....
 
Yo Yo...[B said:
more than 60 ya wanawake ukiishiwa wananuna na kusepa[/B] ukizubaa masela wanakusaidia.....

What is the source of this info/data ndugu yangu....hata kama ni kukisia, why 60 and not 80 or 10? or even 2?
 
What is the source of this info/data ndugu yangu....hata kama ni kukisia, why 60 and not 80 or 10? or even 2?
Naishi mtaani bibie,nakaa na wanawake,nafanya nao kazi kila mahali niko nao...nina dada pia,mama wadogo na shangazi......unahitaji data zaidi?
 
Hakuna cha ajabu hapa. Ndoa nyingi zinapitia katika majaribu mbali mbali na nyingi zinadumu. Wanandoa wengi hupeana ushauri mbali mbali ikiwemo ajira n.k.. Labda wakati huo Michelle kwa kuona hali halisi ya mumewe na kujua siasa ilivyo mchezo mchafu hakuona bright future ya wao kama family hivyo alikuwa na kila sababu ya kutoa opinion yake kama mke.

Michelle hata kama ni kweli aliona 'Siasa ni kupoteza muda' lakini hakufile divorce bali aliendelea kuwemo ndani ya ndoa na leo hii anafaidi matunda ya uvumilivu wake.

Wanandoa hupeana ushauri mbali katika maisha yao, wakati mwingine wanaweza huwa wako very accurate na wakati mwingine wanakuwa hawako accurate, lakini hawatoi ushauri huo kwa nia mbaya bali kwa nia nzuri ya kuijenga na kuiendeleza familia yao katika siku za usoni.
 
Back
Top Bottom