Ndoa ya Miaka Mitano Yavunjika na Mke Kulipwa dola Milioni 50

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
2553638.jpg

George David na mkewe enzi za furaha ya ndoa yao Sunday, July 19, 2009 5:33 AM
Mwenyekiti wa kampuni ya United Technologies Corp ya Marekani milionea George David ameachana na mkewe aliyeoana naye mwaka 2002 na atamlipa jumla ya dola milioni 50 kama fidia ya kuvunjika kwa ndoa yao. Ndoa ya milionea George David na mkewe Marie Douglas-David raia wa Uswizi ilivunjika mwaka 2007 ikiwa ni miaka mitano tu toka walipooana mwaka 2002.

George David ni mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya United Technologies Corp (UTC) ambayo huhusika na utengenezaji wa mitambo ya viwandani, injini za ndege na helikopta pamoja na silaha za kivita.

George David ana umri wa miaka 67 wakati mkewe ana umri wa miaka 36. Tofauti ya umri kati yao ni miaka 31.

Taarifa zilisema kuwa wapenzi hao baada ya kuoana mwaka 2005 waliandikishiana kuwa ndoa yao itakapovunjika basi George amlipe Marie dola milioni 42.5 kama fidia ya ndoa.

Lakini mwaka 2007 ndoa yao ilipovunjika Marie aligeuza kibao na kudai alipwe dola milioni 99 kutoka kwenye utajiri wa George David wa dola milioni 329.

Baada ya kufikishana mahakamani na mzozo huo wa fidia kudumu miaka miwili tangia mwaka 2007 hatimaye wapenzi hao walifikia muafaka ijumaa.

Kwa mujibu wa muafaka huo George David atamwongezea mkewe dola milioni 6.5 zaidi katika dola milioni 42.5 walizokubaliana awali.

Marie pia mbali ya kulipwa mamilioni hayo ya dola za kimarekani, atapewa pia baadhi ya mali za mumewe huyo.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2553638&&Cat=7
 
Back
Top Bottom