Ndoa ya Kiserikali+ndoa ya Kanisani

rakeyescarl

JF-Expert Member
Dec 9, 2007
481
145
Wanasheria naomba msaada wenu.
Hivi kama mtu ana ndoa ya kanisani(RC) na baadae akaenda akafunga ndoa kiserikali(civil) je
1)kote huko anapata vyeti?Maana nasikia kote huko vyeti vinavyotolewa ni vya serikali na je is it illegal
2)Je mpaka sasa hatujawa na uwezo wa kujua kuwa mtu huyu mwenye jina lile lile anaoa au kuolewa tena?
ASANTENI.
RE.
 
Ninaishi mtaa mmoja na jamaa ambaye alianza na ndoa ya serikali, akapata cheti,
Akaoa kiislamu, akapata cheti,
Na sasa Mkesha wa Pasaka juzi ameoa Kikatoliki, na amepata cheti!

Ukiongelea mambo ya kujulikana kwa kutumia majina broda hapo unaongelea kompyuta, , huenda hujatembelea ofisi za serikali kwa mfano kabidhi-wasii, ambako mafaili yamelundikana toka miaka ya 1950, na hakuna mfuatano wa kumbukumbu.

Ofcourse ni makosa kuwa na vyeti zaidi ya kimoja kwa wakati mmoja, maana holder anaweza kuvitumia vyote kwa malengo fulani mabaya!
 
sheria inatambua ndoa za aina tatu
1. kidini
2. kimila
3. kiserikali

mchungaji au sheikh anapotoa cheti cha serikali hutoa kama wakala wa serikali katika ufugishaji wa hiyo ndoa na hata yale mashartu ya kutangaza siku 21 ni ya serikali na sio ya dini

kama ilivyo kwa ubatizo, kipaimara nk, mtu akifunga ndoa kanisani anapewa cheti cha kanisa (kwani ndoa ni koja ya sakramenti za kanisa) pamoja na cha serikali. ukifunga ndoa serikalini pekee, utapata cheti kimoja cha serikali pekee na siku ukitaka "kuibariki" ndoa yako (kama wafanyavyo wakatoliki wengi) kwa kuongeza na rites za kidini, basi kanisa/msikiti wako utakupa cheti kingine ambacho ni cha kidini na hakikomeshi wala kuharamisha (don't render void) cheti ulichopata mwanzo cha serikali

lakini kisheria, ndoa iliyofungwa kwa aina yoyote kati ya hizo tatu hapo juu inatambulika
 
Kote huko anafunga ndoa na mtu huyo huyo ama watu tofauti?
 
Kwa maelezo ya mtoa mada nahisi ni watu tofauti, kwa kuwa mie sio mwanasheria nasubiri waje wataalamu wa sheria watoe darasa.
 
Ninaishi mtaa mmoja na jamaa ambaye alianza na ndoa ya serikali, akapata cheti,
Akaoa kiislamu, akapata cheti,
Na sasa Mkesha wa Pasaka juzi ameoa Kikatoliki, na amepata cheti!

Ukiongelea mambo ya kujulikana kwa kutumia majina broda hapo unaongelea kompyuta, , huenda hujatembelea ofisi za serikali kwa mfano kabidhi-wasii, ambako mafaili yamelundikana toka miaka ya 1950, na hakuna mfuatano wa kumbukumbu.

Ofcourse ni makosa kuwa na vyeti zaidi ya kimoja kwa wakati mmoja, maana holder anaweza kuvitumia vyote kwa malengo fulani mabaya!

Dah PJ huyo mtu ni noma. Wake wengine walikuwa anawaacha kila anapooa tena au?
 
Mh. Judith nakushukuru sana lakini ni kweli kuwa kanisani wanatoa vyeti 2? au una maana cha mke na cha mme i.e kila mtu na chake?
Asante sana.
sheria inatambua ndoa za aina tatu
1. kidini
2. kimila
3. kiserikali

mchungaji au sheikh anapotoa cheti cha serikali hutoa kama wakala wa serikali katika ufugishaji wa hiyo ndoa na hata yale mashartu ya kutangaza siku 21 ni ya serikali na sio ya dini

kama ilivyo kwa ubatizo, kipaimara nk, mtu akifunga ndoa kanisani anapewa cheti cha kanisa (kwani ndoa ni koja ya sakramenti za kanisa) pamoja na cha serikali. ukifunga ndoa serikalini pekee, utapata cheti kimoja cha serikali pekee na siku ukitaka "kuibariki" ndoa yako (kama wafanyavyo wakatoliki wengi) kwa kuongeza na rites za kidini, basi kanisa/msikiti wako utakupa cheti kingine ambacho ni cha kidini na hakikomeshi wala kuharamisha (don't render void) cheti ulichopata mwanzo cha serikali

lakini kisheria, ndoa iliyofungwa kwa aina yoyote kati ya hizo tatu hapo juu inatambulika
 
Ndio Mheshimiwa,
Yaani kama ni mke basi anafunga na wanaume tofauti kote na kama ni mwanaume basi huko kote anafunga na wanawake tofauti.
Asante,

Maelezo yako ni ya kweli na Hakika

Pia kwenye ndoa ya Bomani {Serikali} Siku mnaenda kuandikisha ndoa kuna maswali ambayo unaulizwa na ofisa wa ndoa ambayo anayajaza kwenye form ya maelezo mfano. Je ndoa yenu ni ya wake wengi au mmoja? Je ulisha wahi kuoa au kuolewa na ukaachana na mtu mwingine na ikionekana mliachana basi unaulizwa ilikuwa kisheria au? kama ilikuwa kisheria kuna hati ambayo unapaswa kuja nayo ( sina hakika sana unatoa maelezo au hati ya kuachana unakuja nayo) na ikiwa ulidanganya kwenye maelezo basi ukibaika mkondo wa sheria unaweza ukafuata mkondowake
 
PJ, Hao watu ni wapuuzi na wanajitafutia matatizo.
Kwanza ikitokea one of the anafariki let say ndugu zake ni waislamu watasema mazishi na utaratibu wa mgawanyo wa mali vifuate dini ya kiislam hapo hapo aliyebaki kama utaratibu huo haumpi favour atasema hapana ndoa yetu ni ya kiserikali hatufuati mfumo wa dini yoyote, au atatokea ndugu mwingine anayefahamu akaleta cheti kile cha ndoa ya kikiristu akasema hawa walikuwa wakiristu itakuwaje?

Na kama hivyo vyeti wanavitumia kwa michezo michafu either kibiashara, kusafiri nchi za nje e.t.c inabidi waaminiane sana kwani siku mmoja akiudhiwa atatoa siri ili wote waangamie lakini pia wanaweza kuishia jela huko kwenye mataifa ya watu wapovitumia. wawe makini sana.

Ninaishi mtaa mmoja na jamaa ambaye alianza na ndoa ya serikali, akapata cheti,
Akaoa kiislamu, akapata cheti,
Na sasa Mkesha wa Pasaka juzi ameoa Kikatoliki, na amepata cheti!

Ukiongelea mambo ya kujulikana kwa kutumia majina broda hapo unaongelea kompyuta, , huenda hujatembelea ofisi za serikali kwa mfano kabidhi-wasii, ambako mafaili yamelundikana toka miaka ya 1950, na hakuna mfuatano wa kumbukumbu.

Ofcourse ni makosa kuwa na vyeti zaidi ya kimoja kwa wakati mmoja, maana holder anaweza kuvitumia vyote kwa malengo fulani mabaya!
 
Kimsingi na kisheria mtu 1 huwezi kuwa na vyeti 2 vya ndoa kwa wakati mmoja.

ninavyofahamu watu wengi huwa wanaanza na ya serikali then wakishakubaliana kimsingi ni imani gani wafuate ndio wanaenda kanisani au msikitini.
Tatitzo ni nini cha kufanya na kile cheti cha kwanza, it is supposed to be returned to the registrar of marriages ili wakati anasajili hiyo ndoa ya pili ajue kuwa ni same parties, badala ya kusajili as if ni wanandoa wapya kabisa.

Nakubaliana na PJ kuwa mfumo wa utunzaji wa kumbukumbu ofisi ya kabidhi-wasii mkuu unaweza kuwa na mapungufu ndio maana watu haohao wanaweza funga ndoa 3 na kuwa na vyeti 3 vya ndoa!!!!!!!!!!! mbaya sana.
 
Ndio Mheshimiwa,
Yaani kama ni mke basi anafunga na wanaume tofauti kote na kama ni mwanaume basi huko kote anafunga na wanawake tofauti.
Asante,
Kote huko anafunga ndoa na mtu huyo huyo ama watu tofauti?
 
sheria inatambua ndoa za aina tatu
1. kidini
2. kimila
3. kiserikali

mchungaji au sheikh anapotoa cheti cha serikali hutoa kama wakala wa serikali katika ufugishaji wa hiyo ndoa na hata yale mashartu ya kutangaza siku 21 ni ya serikali na sio ya dini

kama ilivyo kwa ubatizo, kipaimara nk, mtu akifunga ndoa kanisani anapewa cheti cha kanisa (kwani ndoa ni koja ya sakramenti za kanisa) pamoja na cha serikali. ukifunga ndoa serikalini pekee, utapata cheti kimoja cha serikali pekee na siku ukitaka "kuibariki" ndoa yako (kama wafanyavyo wakatoliki wengi) kwa kuongeza na rites za kidini, basi kanisa/msikiti wako utakupa cheti kingine ambacho ni cha kidini na hakikomeshi wala kuharamisha (don't render void) cheti ulichopata mwanzo cha serikali

lakini kisheria, ndoa iliyofungwa kwa aina yoyote kati ya hizo tatu hapo juu inatambulika

Kwa maelezo haya kwenye red inaonyesha kuna ndoa ya aina moja tu nayo ni ya serikali. Ila sasa serikali hiyo hiyo ina namna tofauti ya utekelezaji wa jambo hili kwa kutumia mawakala tofauti ambao ni viongozi wa dini walio sajiliwa na wa mila kama wapo walio sajiliwa na serikali yenyewe moja kwa moja.
 
Wanasheria naomba msaada wenu.
Hivi kama mtu ana ndoa ya kanisani(RC) na baadae akaenda akafunga ndoa kiserikali(civil) je
1)kote huko anapata vyeti?Maana nasikia kote huko vyeti vinavyotolewa ni vya serikali na je is it illegal
2)Je mpaka sasa hatujawa na uwezo wa kujua kuwa mtu huyu mwenye jina lile lile anaoa au kuolewa tena?
ASANTENI.
RE.
Ni kwamba kama ulioa kisheria na kupewa marriage certificate whether kanisani, msikitini au kwa mkuu wa Wilaya, unaruhusiwa kisheria iwapo huyo mkeo wa kwanza mmeachana kisheria Mahakamani (divorce) na si kwamba leo umeoa, kabla ya divorce unaoa tena na kupewa cheti cha ndoa! hiyo hairuhusiwi labda muhusika asiweke wazi na awe hajulikana katika eneo hilo na ukigundulika unshtakiwa
 
ukioa ya kimila ntafute nikupe cheti free of charge achana na vykina yoyoyo 30,000
 
Ok ngoja niwape sheria ya ndo muuisome naipost jukwaa la sheria ...........back
 
Back
Top Bottom