Ndoa ya Dr. Slaa na Josephine ni ruksa, hakuna pingamizi tena dhidi yao

muwamba ngoma, ngozi huvutia kwake? Chadema tunapenda sana Dr. Slaa kiasi cha kusahau mapungufu yake kama binadamu mwingine. Kitendo cha kuzaa watoto wawili na kama kweli walikuwa wanakaa pamoja zaidi ya miezi 6 chini ya paa moja na majirani wa kuprove hilo wapo Rose anakuwa mke wa Dr. Slaa by default so she is a legal wife. Hatuingilii mahakama ni maoni tu
 
wakuu ndoa Jmosi sasa nikitaka kuchangia inakuwaje? dada Josephine usitunyime pilau tafadhali.
 
Chadema bana kwa kuchagua mambo leo mahakama imetenda haki lakini linapokuja suala la Lema mahakama imetumwa na Ikulu...

Vipi kuhusu madai ya Rose Kamili, ya Dr Slaa kutelekeza familia yake.

Na wewe una hamu ya kuoalewa. Nenda kwenye page za mambo hayo.
 
muwamba ngoma, ngozi huvutia kwake? Chadema tunapenda sana Dr. Slaa kiasi cha kusahau mapungufu yake kama binadamu mwingine. Kitendo cha kuzaa watoto wawili na kama kweli walikuwa wanakaa pamoja zaidi ya miezi 6 chini ya paa moja na majirani wa kuprove hilo wapo Rose anakuwa mke wa Dr. Slaa by default so she is a legal wife. Hatuingilii mahakama ni maoni tu

Mkuu kuna mambo kadhaa kwenye post yako:-

(i) Hapo kwenye
green: kuzaa hata watoto mia nje ya ndoa haku-justify ndoa na yule uliyezaa naye. So, that is pointless.

(ii) Hapo kwenye
red: Inawezekana lakini umeangalia upande mmoja tu in favor of Rose. Hebu angalia upande wa pili wa coin, suppose Rose ndiye aliyemtelekeza Dr. Slaa? Au kwa kuwa ni yeye (Rose) ndiye anayelalamika unadhani hawezi akawa ndiye chanzo cha mgogoro?

(iii) Hapo kwenye
red: Umezingatia dhana iitwayo "UTORO KWENYE NDOA"? Umezingatia pia kwamba mume n mke wasipokuwa pamoja kwa muda fulani ndoa inakuwa VOID? Katika shauri hili inawezekana Rose au Dr. Slaa au wote wamekuwa watoro kwenye "ndoa" yao kwa muda unaotambulika kisheria hivyo dhana ya ndoa haipo. Usiangalie upande mmoja tu wa kuungana hata kutengana pia kunatambulikana kisheria.

(iv) Huyu Rose kama si kutumiwa, angeibuka mapema kabla muda unaotambuliwa kisheria wa UTORO KWENYE NDOA haujakamilika. Mtu hawako pamoja kwa zaidi ya miaka sijui mingapi halafu leo unaibuka eti ni mume wangu hana hata aibu? Anachopaswa kudai ni MALI WALIYOCHUMA PAMOJA (kama ipo) na sio HAKI YA MUME.

(v) Ndoa tarajiwa ya Dr. Slaa na Josephine: Sijui ndoa ya Dr. Slaa inatarajiwa kufungwa kwa madhehebu gani ila kama ni madhehebu ya kikristo; ndoa huwa ndoa halali pale inapofungwa kiimani. Hivyo, dhana yako uliyoitaja hapo kwenye
red haitambuliki na kanisa hivyo Dr. Slaa hakuwahi kuwa na ndoa hapo kabla.



Otherwise, binafsi nampongeza sana Dr. W. Slaa na Mkewe Mtarajiwa, Josephine Mushumbusi, kwa kuachana na maisha ya ukapera na kuanza maisha mapya ya ndoa. Hongereni sana Maharusi wetu. Mwenyezi Mungu awajalie maisha marefu yenye baraka na fanaka kwa familia yenu.
 
dudus Mkuu kwa kiasi nakubaliana na uchambuzi wako ila hapa mwisho ni kwamba anakuwa mke wake kisheria endapo wamekaa pamoja kwa zaidi ya miezi sita. Hiyo default status inatambuliwa na sheria na sio kanisa wala msikiti. Na rose kwa hiilo hawezi kuihakikishia mahakama kuwa ilikuwa ndoa ya aina gani. Ya mke mmoja au wengi maana hawana cheti cha ndoa. Ila kuna kila dalili kuwa kuna mtu nyuma ya rose ambaye anamsukuma kufanya hivi. Kwani mara baada ya kutoka CCM na kujiunga Chadema kauli za rose huyu huyu aliyepongezwa na Sophia Simba ni tofauti na hatua aliyochukua. Lengo hapa ni kujaribu kuchafua jina la Dr. Slaa kwenye mchakato wa kwenda Ikulu
 
Last edited by a moderator:
Hongera Dr. This time mfanye kweli ili tusipoteze muda humu kwenye mijadala isiyo na manufaa kwa Taifa.
 
Watanzania tuache udini,kabisaa hasa sisi waislam ni wadini sana,tuaache upumbavu huo kwasababu hata aliyeleta dini hatumjui.
 
Jamani wenye picha tumuone huyo bibi harusi mtarajiwa kama kitu au galasha
 
fmpiganaji Attention Sophia Simba na Ester Bulaya, in future they should do their home work first kabla ya kushangilia masahibu ya wenzao!! (front page Mwananchi julai 13, 2012; wakimpongeza Rose kamili kwa kuweka pingamizi dhidi ya wanandoa watarajiwa) Next time do not play CCM politics on matters holy!
 
Last edited by a moderator:
Chadema bana kwa kuchagua mambo leo mahakama imetenda haki lakini linapokuja suala la Lema mahakama imetumwa na Ikulu...

Vipi kuhusu madai ya Rose Kamili, ya Dr Slaa kutelekeza familia yake.

Kila jambo limekuwa siasa tu,iliwahi kutokea siku moja baba m1 alimtuma mtoto wake dukani,alipochelewa kurudi yule mzee akasema naona sasa umekuwa CHADEMA,kila nikikutuma unakuwa mbishi.Sasa leo ni suala la kijamii lakini siasa inaingizwa wapi tunaelekea?
 
Tunakoelekea itabidi uweke mezani hoja ya kutafuta mchumba wadau wajadili kama anafaa au la!
 
Back
Top Bottom