Ndoa ya chadema na sabodo si mtihani tosha kwa upinzani?

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
source: mpayukaji.blogspot.com

Hakuna ubishi kuwa ndoa ya anayeitwa mfanyabiashara maarufu kwa jina la Mustafa Sabodo imeshika kasi. Kwa wanaojua jamaa zetu hawa walivyoletwa na kuchuma, anahofia usafi wa huyu jamaa anayesifika kutumia jina la marehem Mwalimu Julius Nyerere kujinufaisha. Anajiita mpenzi wa Mwalimu ambaye wakati wa uhai wake hata hivyo hatukuwahi kumsikia.

Je hii ni janja ya wahindi kuanza kutafuta pa kushika baada ya kuona CCM ikiyoyoma? Je kama wameitosa CCM iliyowalea na kuwakumbatia hadi wengine kuzawadiwa ubunge, CHADEMA ni nani wasiifanyie hivyo?

Je nao falsafa yao ni ya 'Sina adui au rafiki wa kudumu bali maslahi'?

Mwanzoni Sabodo aliahidi kuwapa CHADEMA jengo lake la Mwenge. Ghafla amepiga U-turn na kusema eti atawajengea ofisi. Tusije tukaruka mkojo tukaishia kukalia manonihino. Ndoa ya Sabodo na CHADEMA inabidi iangaliwe isijekuwa ni mtego wa CCM kumtuma kada wake kuwachafua. Kama Sabodo anaipenda CHADEMA anangoja nini CCM? Kimsingi anataka kuweka vyama vyote mfukoni mwake.

Sabodo alikaririwa akisema, "Kwa kweli nimefurahi sana kunialika kwenye mkutano wenu, nimeshawahi kuisaidia CCM, lakini hawajawahi kunishukuru kama mlivyofanya ninyi."Je hii ni sababu yenye mashiko kumfanya aipende CHADEMA hivyo au anaandaa pa kushika baada ya CCM kujiishia?

My take: Nimeshindwa kuipuuza habari hii
 
MAMA POROJO,
Kuna romous zimezagaa mitaani kwamba wafanyakazi wengi wa hapo Lumumba hamjalipwa mshahara. Je ni kweli? Msalimie Nape na Mzee Msekwa. Waambie e-Politics haiendeshwi kwa staili hii.

TUMBIRI wa JF,
P.O BOX - PM JF.
 
Hoja yako haina mashiko,,ktk mchango wako leo hapa umeona hilo 2? Fuata ya magamba
 
Mama Masaburi umefikiria tokea wiki iliyopita ndio unatuletea huu uchafu changia thread za wenzako inatosha. Halafu naona Vibarua kutoka kwa nape vimeota majani mmepungua sana humu jamvini
 
Ninaandika kutoa masikitiko yangu hapa jf,mashabiki wa ccm wamepungua sana kama sio kwisha kuna post zingine hutawaona kabisa.mmekwiba sana pesa zetu for 50yrs hata kutetea chama chenu mnashidwa hata nape ndio usiseme,mbona kipindi cha uchaguzi kule arumeru mlikuwa wengi hadi mkaweka rehani uhai wenu endapo dm ingeshida? Njooni tuwavue hizo gamba!
 
MAMA POROJO,
Kuna romous zimezagaa mitaani kwamba wafanyakazi wengi wa hapo Lumumba hamjalipwa mshahara. Je ni kweli? Msalimie Nape na Mzee Msekwa. Waambie e-Politics haiendeshwi kwa staili hii.

TUMBIRI wa JF,
P.O BOX - PM JF.

hata kama ningekuwa Lumumba na wewe ukawa Makao Makuu ya chama chako bado tunahitaji kujadili hoja kwa manufaa ya taifa letu badala ya kunijadili mimi
 
Sabodo nilmwona kwenye TV akiwa Ikulu kuwaapisha Mawaziri kumbe bado yuko CCM
 
CHADEMA na wanachama wake ni full madigiriii. Kama unafikiri tunaingizwa mkenge basi acha nikwambie tabia zetu. Kwa mfano mimi, nina kadi ya CCM lkn mimi ni CHADEMA dam dam. Hii kadi inaniwezesha kutafuna fedha za Hawa Nghumbi kwenye uchaguzi, lkn moyo wangu nao unaniongoza kumpigia kura Mnyika John Maakili.

Kama hiyo ndio nia ya Sabodo, rest in peace assured kuwa senti zake tutatafuna na siku ya kuwajibishwa atawajibishwa kama tulivyomwajibisha mama yenu Hawa kule Ubungo.

Sijui uchaguzi utakuja lini tena nile visenti vya CCM mie. Sio vingi, lkn kwa kweli vinanisaidia kupata maji ya kulainishia koo niwe na pumzi ya kuwaeleza vijana uzuri wa CDM.

M4C, mpk kieleweke. Pole mama blah blah!

Nimesikia Sabodo anataka kuinunua Lumumba aipe CDM, mtahamia wapi?
 
Degree ya wapi inayotoa majibu mepesi hivi??????????? tena nje ya swali.
 
Back
Top Bottom