Ndoa na Mirathi: Nafasi ya Mahakama ya Kadhi kwa Wanawake

Status
Not open for further replies.
Waislamu cha msingi kwao ni Mahakama ya Kadhi tu hakuna kingine? Hivi huyo Kadhi atatuondolea umaskini tulio nao au atatusaidiaje?

Hivi ikiwa unashindwa kujiondoa wewe mwenyewe kwenye umaskini unategemea nani akuondoe? Kanisa limeshakutoa kwenye umaskini?

Umaskini hauko kwenye mali au kipato chako umaskini upo ndani ya damu yako. Hata uletewe Papa hatokuondolea umaskini uliokuwa nao.

Uwepo wa kadhi ni kuhakikisha kuwa Muislaam ana haki kama yule asie na dini. Au mwenye haki nchi hii ni yule ambae hana dini?

Kodi za Waislaam na wasio Waislaam zinalipia Mahakama za wasio na dini. Jee hiyo ni haki? Ambae ana dini yake hana haki? Mnanshangaza.
 
Kwa kweli nimependa hoja ambayo imedokezwa na kuletwa na na BR. Mara nyingi ukiwasikia watu wanazungumzia mahakama ya kadhi na suala la mirathi na ndoa utaona ni hoja za Wanaume Waislamu ambao hupewa kipaumbele. Yaani, jambo hili linaangaliwa kwa mwanga wa mwanamme Muislamu na sikumbuki kama mawazo ya wanawake wa Kiislamu kuhusu suala hili yamewahi kuwekwa bayana kama alivyofanya BR. Ametupa mwanga na kulazimisha watu wafikirie vizuri maana watu wanaposema jambo hili ni zuri kwa Waislamu wanahitaji kujibu baadhi ya maswali ambayo yanaibuliwa na BR. Ni maswali ambayo yanahusiana ni nani ambaye ataguswa sana na uwepo wa mahakama hiyo - Mwanamke wa Kiislamu.

BR tupe darasa.
 
Kwanza napenda kusema mimi ni mmoja wa wanaokubali kuwa mahakama za kadhi ni muhimu kwa maswala yanahohusu ibada na maisha ya muislam, hususan ndoa, talaka na mirathi.Hili halina ubishi. Ninachokipigania ni kwanza kuwa na mwanzo mzuri kwetu sisi wenyewe kufuata maamrisho ya Kuraan, kuanzia kufunga ndoa, maisha ya ndoa kwa maana ya matunzo, maridhiano ya unyumba na mengineyo na stahili nyingine, ikiwemo kuachana kwa talaka pale inapobidi na pia mirathi. Huu ndio msingi utakaoleta maana pale mahakama za kadhi zitakapoanza kazi endapo zitaundwa.Hii ndio hoja yangu ya msingi na labda tungeanzia hapo. Utaona hata michango yangu hapo juu, nimesisitiza sana huu msingi.
 
Usinchekeshe!
Ina maana waislam watanzania wao hawajiwezi hadi kuchangiwa? Hebu usituangushe.
Mtumai cha ndugu si hufa maskini?Mahakama ya kadhi tunachoionea mashaka ni kama itaweza kumaliza matatizo ya "kifikra' kwa wanaume wa kiislam hasa kwenye Ndoa.Huu umaskini uliokithiri utamalizwa vipi na hii mahakama? Tatizo ni umaskini wa fikra na mapato unaochangia wanawake wa kiislam kunyanyasika.Salma2015 kauliza maswali ya msingi na hakuna hata mmoja kaweza kujibu hizo hoja.Wanawake wa kiislam hawana tatizo na maagizo ya Kuran au ya Mtume.Wasiwasi ni utendaji kuanzia waumin wenyewe hadi watakaosimamia hizo mahakama.Enyi wanaume, mjue mnatuharibia ibada zetu kwa tabia zenu.Mnalazimisha wanawake wawe na tabia zisizoendana na Uislam kwa vile nyie hamtimizi maagizo.Mnabebesha wanawake mizigo mizito ya "hasira, wivu, chuki" ukiacha mingine ya familia . For you the intellectuals I would confidently say that
Ndoa kwenye uislam ni ibada.Allah kamuumba "mwanamke" kwa "mwanaume" waishi kwenye ndoa kwa lengo la kuwepo amani, utulivu, raha na faraja.Hivyo basi ndoa inatakiwa izae AMANI NA RAHA.Hii itawezekana kupatikana kama tu wote wanatimiziana wajibu unaowapasa vinginevyo kutakuwa na magomvi yatakayoharibu amani, utulivuna hatimaye kuharibu ndoa (Rejea Kur.30.21).Wanaume mmepewa onyo mkaambia Muogopeni Allah kwa jinsi mtakavyoshi na wake zenu, kwa sababu mumewaoa kwa trust ya Allah! Sasa kama nyie hata hili Onyo hamlizingatii, mnaweza kuwa na uhalali kudai mahakama ya Kadhi ili ati iwaamulie mambo ya ndoa?

Haya hili la Polygamy nalo ni suala lenye utata.
Uislam umeweka msisistizo mkubwa kwa haki za watu - mume –mke, na pia zile za Muumba.Kufuatana na Uislam,mke ni life partner and not a robot or husband’s property that can be put out of commission or replaced at any time without any consideration, concern, shame or feelings!Uislam haumpi mwanaume yeyote yule a right to have more than one wife nor considers it is an act of piety.
Mtume mwenyewe alikuwa na mke mmoja tu for about twenty five years kabla ya kuoa wengine,na alimuoa huyu mke akimzidi mtume kwa miaka 15 years.Pigeni mahesabu ndipo mtambue "tamaa" haikuwa sababu ya msingi ya Mtume kuoa zaidi ya Bi Khadija. Hivyo basi kinyume na wanavyodhania wanaume wengi wa kiislam, monogamy is a norm and polygamy a rare exception in Islam. Kuhusisha dini na polygamy ni upotoshaji wa makusudi wa wale wenye kueneza huo utaratibu wa kuoa wake wengi.

Dini ya Kiislam ni dini ya haki kwa wote na siyo a smoke screen to deceive anyone and or hide behind it to protect personal desires or lust. Wanaume wengi wa Kiislam wanajitafutia uhalali wa vitendo vyao kwa kutumia verses za Kuraan conveniently and selectively bila kusoma ayah kamili na kuwa na uelewa wa kutosha. Ayah inayozungumzia kuoa zaidi ya mke mmoja ina context na imeelezwa uzuri kabisa: Marrying more than one wife was revealed after a battle in which many Muslim men were killed leaving behind helpless widows and orphans. The entire ayah (verse) of Surah (chapter) An-Nisa (The women 4:3), where Allaah The Almighty says; “And if you fear that you shall not be able to deal justly with the orphan-girls, then marry other women of your choice, two or three, or four, but if you fear that you shall not be able to deal justly with them, then (marry) only one…….”

Sasa nyie wanaume wa Tanzania, miaka hii mna sababu gani zaidi ya tamaa zenu kuoa zaidi ya mke mmoja?

Kwanza, Mtazamo wako kuwa kuna jamii ya wanaume waislamu hawawatendee haki wanawake wao ni sahihi kabisa, lakini napenda nikufahamishe kuwa hayo ni makosa yao wanaume wa kiislam na si makosa ya uislamu na mahakama ya kadhi haiwezi kunyimwa kwasababu kuna wanaume wa kiislamu wanawatesa wanawake kinyume cha mafundisho ya dini.

Pili nafikiri mahakama ya kadhi iliyo na waadilifu itasaidia kutoa hukumu kama hizo ulizosema, sidhani kama ni sawa kidini kwa mwanaume asiye na uwezo kuoa wake zaidi ya moja mfano kuwalaza wake zake kwenye chumba kimoja kama ulivyosema. sharia inaufafanuzi wa kutosha kuhusu nani anaruhusiwa kuoa, sababu za kuoa nk. imetoa mfano mzuri ni kwanini mtume alioa hizo sababu za mwanamume muislamu kuoa na si vinginevyo..

Tatu, sisi tunaotaka mahakama ya kadhi si kwa ajili ya kunyanyasa wanawake bali kwa ajili ya kufanya ibada zetu, kuona kuwa mali zetu na maisha yetu yanakuwa katika hukumu ya Allah, mahakama itasaidia kutoa ufumbuzi wa mirathi za mali zetu ..above all ni choice kwako kama unaona bado uzito kufuata hukumu hiyo unaweza kutumia sheria za nchi..

Nafikiri swala hili ni la imani hakuna kulazimishana katika imani
 
Hii waje wabishe! Wanawasukuma wake zao kwenye zinaa tu halafu wanadai Kadhi courts.Wasafishe kwanza nyumba zao, watii maamrisho ya Uislam ndipo wadai Kadhi Courts.Wanafiki wakubwa! Kwanza wanaaibisha Uislam kwa maana Uislam unampa mwanamke staha kwa mapana yote.Uislam hautaki mwanamke aaibike kwa kujitembeza ovyo mitaani, sokoni na madukani kuombaomba.Mume apaswa kumtimizia mkewe na watoto.Fikiria mwanaume unamlazimisha mkeo kuvaa hijab, kisha unamuachoa buku afanyefanye! Hiyo fanyafanya maana yake nini? Huko sokoni unakotaka aende akajichekeshechekeshe kwa wauza nyanya, vitunguu na mchicha ili tu wewe ule ndio uislam?Halafu unataka kuoa rundo la wanawake - niliuliza utawalisha nini? Au ndio utumwa mamboleo?

Bibie,

Hichi ulichoandika hapa hakina uhusiano na mahakama ya kadhi
 
Kwanza napenda kusema mimi ni mmoja wa wanaokubali kuwa mahakama za kadhi ni muhimu kwa maswala yanahohusu ibada na maisha ya muislam, hususan ndoa, talaka na mirathi.Hili halina ubishi. Ninachokipigania ni kwanza kuwa na mwanzo mzuri kwetu sisi wenyewe kufuata maamrisho ya Kuraan, kuanzia kufunga ndoa, maisha ya ndoa kwa maana ya matunzo, maridhiano ya unyumba na mengineyo na stahili nyingine, ikiwemo kuachana kwa talaka pale inapobidi na pia mirathi. Huu ndio msingi utakaoleta maana pale mahakama za kadhi zitakapoanza kazi endapo zitaundwa.Hii ndio hoja yangu ya msingi na labda tungeanzia hapo. Utaona hata michango yangu hapo juu, nimesisitiza sana huu msingi.

Bibie, ni kweli kabisa unachosema je unafikir watu wote watakuwa waislamu wazuri kama upendavyo? haiwezekani ndio maana kunatakiwa kuwe na choice, asiyetaka mahakama ya kadhi aende state courts

Naomba nikuulize, je sisi ambao tumefuata, tunataka kuhukumiwa na mali zetu (alhamudililah tuna uwezo na mali nyingi kiasi) tukifa tunataka mahakama ya kadhi itumike kugawa mali zetu kuna shida gani??
 
Mimi hii kitu ya watoto nje ya ndoa kutotambulika kwenye mirathi inanitia huzuni maana ndiyo inasababisha sana uduni wa maisha ya watu wengi. Lakini mwisho wa siku utasikia ni 'mfumo kristo' ndiyo unaleta ufukara ...kumbe ukweli ni kuwa ufukara unasababishwa na viidume vingi vilivyokosa maadili na kujaa zinaa.

Watoto nje ya ndoa wakiwemo kwenye mirathi wataleta matatizo zaidi. Kumbuka Uislaam unasisitiza ndoa na hausisitizi zinaa na kama mtu aliteleza na kuzaa nje ya ndoa basi ampe mali (kama anayo) huyo mtoto nje ya ndoa na kabla hajafa na si kuleta rabsha baada ya kufa.
 
Bibie, ni kweli kabisa unachosema je unafikir watu wote watakuwa waislamu wazuri kama upendavyo? haiwezekani ndio maana kunatakiwa kuwe na choice, asiyetaka mahakama ya kadhi aende state courts

Naomba nikuulize, je sisi ambao tumefuata, tunataka kuhukumiwa na mali zetu (alhamudililah tuna uwezo na mali nyingi kiasi) tukifa tunataka mahakama ya kadhi itumike kugawa mali zetu kuna shida gani??

Ndugu yangu,Ninakuelewa unachokisema.Hapo kwenye bold, mko wangapi hadi mqualify kuwa na hiyo mahakama na itoe haki bila kuumiza wengine?Nakupata vizuri sana.Sijui ushajaribu kujishughulisha kujua nini kinatokea huko Kenya ambapo kuna mahakama ya Kadhi tena kikatiba?
Kenya , Mahakama ya Kadhi ilianzishwa kwa makubaliano baina ya late Kenyatta, rais wa Kwanza wa Kenya, na Sultan wa Zanzibar for a 10 mile coastal strip ambayo ilikuwa incorporated kwa Republic of Kenya at independence.Utaona dhahiri hii ilikuwa ni "biashara" na siyo utashi wa kisiasa ( political will and commitment).Moja ya central arguments kwa waliokuwa wana advocate for Kadhi courts ziingizwe kwenye hii Katiba yao mpya ni kwamba hizi mahakama zilikuwepo kwenye Katiba ya Kenya since independence.Nadhan hata Waislam wa Tanzania wanatumia hii argument bila hata kujua chanzo cha hizo mahakama kuwemo kwenye mfumo wa Kenya.Basi mngejibidisha kujua hizo mahakama zimekuwa zinafanyaje kazi huko Kenya kabla ya kudai ziingie kwenye mfumo huku Tanzania.

Mwaka jana 2010 December, League of Muslim Women of Kenya (LMWK) lilifanya tathmini kwa kuwaita kwenye dialogue wanawake wa Kiiislam, waje watoe uzoefu wao katika kuzitumia mahakama za Kadhi courts, na pia kujifunza kutoka kwa administrators wa hizo mahakama kuhusu role and mamlaka (jurisdiction) ya hizi mahakama. Mkutano huo ulihudhuriwa na panel ya makadhi wanne, walioongozwa na Sheikh Ahmed Mohdhar, ambaye alikuwa Acting Chief Kadhi na Kadhi wa Nairobi.Nitawanukulia yaliyojiri kwenye ule mkutano kama ifuatavyo:

The Kadhis took time to explain to the women the workings of the Kadhis' courts and responded to concerns and questions raised by the women. The participants shared their experiences using the courts including challenges they encountered in attempting to access justice. A number of critical issues emerged on the problems that women encounter in accessing justice through the Kadhis' courts. Among the challenges identified by the women were :

  • lack of information about the location of the Kadhis' courts,
  • discriminatory practices and lack of public relation skills among some court clerks, and
  • lack of finances to pay court fees.
  • The women also cited the shortage of court process servers which often resulted in them (women) having to personally effect service on the defendants who in most cases would be their estranged husbands. As one participant observed: "The idea of having to ask a woman who has filed a case to go and serve papers to a person they are accusing makes it difficult for the case to commence, for in most cases it is hard to serve the papers."
  • The women further mentioned the lack of female Kadhis and courts clerks as another barrier to access to justice.
  • They mentioned that discussing matters involving pertinent personal issues was difficult and at times embarrassing as all the officers in the Kadhis courts were male.
Sasa nyie mnataka haya matatizo nayo yaje Tanzania kwanini?
Umesema vema kwamba wanawake wanaotaka kutumia mahakama za State wawe huru. Kuna point hujaizungumzia.UWEPO WA OPTIONS NYINGI ndani ya mfumo wa utoaji haki.Tanzania kama nchi nyingi za Kiafrika zenye Waislamzilivyo, bado zina tatizo hili na ndio maana hata zikiwepo Kadhi Courts hazileti maana kama ilivyokusudiwa.Watu bado wanakimbilia jadi/mila zao katika mambo yao ya maisha hata kama ni waislam.Sasa hivi Tanzania hali ndiyo ilivyo.Utafiti wangu umenionyesha kwamba, mahakama hizo za State nazo zinatoa option - kutumia sheria za dini, mila au state. Kwa waislam, huenda tatizo ni kukosekana waamuzi huko mahakama walio na ueledi wa sheria za kiislam.Nadhani tungeanzia hapo kuimarisha weledi.
Wakatabahu,Blackie
 
Suala la Mahakama ya kadhi ni haki ya kila Muislaam kama vile mahakama zisizokuwa za dini.

Kumbuka kuwa hata hii leo, kesi nyingi za Waislaam hupelekwa mahakama hizi zisizokuwa na dini, lakini huko hata Mahakimu wanaposhindwa kuziamuwa huzitafutia ushauri kwa Kabidhi wasihi ambapo kuna wataalamu wa Kiislaam wana ajariwa kuhusu haya masuala.

Sioni tatizo la kuwepo mahakama ya kadhi, nnachokiona ni haki ya kila mtanzania kutendeka ipasavyo awe na au asiwe na dini na kuwanyima Waislaam mahakama ya kusimamia mambo yao ya haki zao za msingi ni kuwanyima haki. Hususan wanawake ndio wa mwanzo kunyimwa haki zao za msingi, uwepo wa mahakama za kadhi zinazotambulika kisheria ni kumpa kila mtu haki yake ya msingi.

Kwanini wasio na dini wawe na mahakama na wenye dini wasiwe na mahakama na wote ni walipa kodi?
 
HIZO ISHU ZAKO NAONA Blackie amezisemea vizuri tu.Ila kuna mambo kayaibua na huenda nyinyi wanawake wa kiislam mngevisemea:

Kenya , Mahakama ya Kadhi ilianzishwa kwa makubaliano baina ya late Kenyatta, rais wa Kwanza wa Kenya, na Sultan wa Zanzibar for a 10 mile coastal strip ambayo ilikuwa incorporated kwa Republic of Kenya at independence.Utaona dhahiri hii ilikuwa ni "biashara" na siyo utashi wa kisiasa ( political will and commitment).Moja ya central arguments kwa waliokuwa wana advocate for Kadhi courts ziingizwe kwenye hii Katiba yao mpya ni kwamba hizi mahakama zilikuwepo kwenye Katiba ya Kenya since independence.Nadhan hata Waislam wa Tanzania wanatumia hii argument bila hata kujua chanzo cha hizo mahakama kuwemo kwenye mfumo wa Kenya.

Huenda hapa pakahitajika debate ili kupata "political will and commitment" na mpaka sasa JK keshakataa kuwaanzishieni kwa hiyo mjue hakuna political will and commitment. Kilichpbaki ni nyie wenyewe kupambana na kuzianzisha

Kuna point hujaizungumzia.UWEPO WA OPTIONS NYINGI ndani ya mfumo wa utoaji haki.Tanzania kama nchi nyingi za Kiafrika zenye Waislamzilivyo, bado zina tatizo hili na ndio maana hata zikiwepo Kadhi Courts hazileti maana kama ilivyokusudiwa.Watu bado wanakimbilia jadi/mila zao katika mambo yao ya maisha hata kama ni waislam.Sasa hivi Tanzania hali ndiyo ilivyo.Utafiti wangu umenionyesha kwamba, mahakama hizo za State nazo zinatoa option - kutumia sheria za dini, mila au state. Kwa waislam, huenda tatizo ni kukosekana waamuzi huko mahakama walio na ueledi wa sheria za kiislam.Nadhani tungeanzia hapo kuimarisha weledi.

Nadhani hapa napo kuna ishu kuntu.Mnazo options tayari ndani ya mfumo uliopo maana mfumo huu unajali wote wenye dini na wasio na dini.Uchaguzi ni wenu.

Wakatabahu,Blackie

Blackie endelea kutoa darasa hadi kieleweke
 
Sioni tatizo la kuwepo mahakama ya kadhi, nnachokiona ni haki ya kila mtanzania kutendeka ipasavyo awe na au asiwe na dini na kuwanyima Waislaam mahakama ya kusimamia mambo yao ya haki zao za msingi ni kuwanyima haki. Hususan wanawake ndio wa mwanzo kunyimwa haki zao za msingi, uwepo wa mahakama za kadhi zinazotambulika kisheria ni kumpa kila mtu haki yake ya msingi.

Kwanini wasio na dini wawe na mahakama na wenye dini wasiwe na mahakama na wote ni walipa kodi?

Waislamu hawajakatwa kuwa na mahakama ya kadhi. Binafsi ningependa kuona wanafanya hata ya majaribio tu kwa jiji la Dar peke yake kwanza.
 
  • The women further mentioned the lack of female Kadhis and courts clerks as another barrier to access to justice.
Duh.. unajua siku hizi mbili umenifanya nifikirie kweli. Maana muda wote ambao tumekuwa tunazungumzia "kadhi" miye mawazoni namuona mbaba fulani akiwa hivyo. Swali ni je, wanawake Waislamu wa Tanzania wanajua wanayo haki ya kuwa kadhi?
 
Mie siungi mkono kuanzishwa mahakama ya kadhi kwakua sina shida nayo na nimeishi vizuri bila kuwepo.lkn naona wanayoitaka ianzishwe chini ya mfumo wa serikali wana hoja.

wanaweza kuiendesha kwa pesa zao n tartibu zao kama mbavyo wanavyosuluhisha ndoa sasa makanisa na bakwata nje ya mfumo wa mahakama.

tabu itakuja pale mtu anapokaidi wito au maamuzi ya mahakama halali nje ya mfumo wa kiserikali atajibishwa je. sheria zetu mtu anaweza kufugwa akishidwa kulipa deni je waislamu watamfunga wapi mtu aliyekula mali za yatima kama serkali haitambui mahakama ilosema kama kala mali za yatima .

MIE NAONA KODI ZA UENDESHAJI SIO ISHU ILA NI NGUMU KUTEKELEZA SHERIA NJE YA MFUMO WA SERIKALI KWANI, MTU HATAFUATA MAAMUZI YA MAHAKAMA NA HAKUNA WA KUMFANYA KITU LBD SIKU YAKUKUTANA NA MUUMBA.
 
mie siungi mkono kuanzishwa mahakama ya kadhi kwakua sina shida nayo na nimeishi vizuri bila kuwepo.lkn naona wanayoitaka ianzishwe chini ya mfumo wa serikali wanahoja.
Wanaweza kuiendesha kwa pesa zao n tartibu zao kama mbavyo wanavyosuluhisha ndoa sasa makanisa na bakwata nje ya mfumo wa mahakama.tabu itakuja pale mtu anapokaidi wito au maamuzi ya mahakama halali nje ya mfumo wa kiserikali atwajibishwaje.sheria zetu mtu anaweza kufugwa akishidwa kulipa deni je waislamu watamfunga wapi mtu aliyekula mali za yatima kama serkali haitambui mahakama ilosema kama kala mali za yatima .mie naona kodi za uendeshaji sio ishu ila ni ngumu kutekeleza sheria nje ya mfumo wa serikali kwani ,mtu hatafuata maamuzi ya mahakama na hakuna wa kumfanya kitu lbd siku yakukutana na muumba.
upuzi wa kisilamu tena!!!
 
Mie siungi mkono kuanzishwa mahakama ya kadhi kwakua sina shida nayo na nimeishi vizuri bila kuwepo.lkn naona wanayoitaka ianzishwe chini ya mfumo wa serikali wana hoja.

wanaweza kuiendesha kwa pesa zao n tartibu zao kama mbavyo wanavyosuluhisha ndoa sasa makanisa na bakwata nje ya mfumo wa mahakama.

tabu itakuja pale mtu anapokaidi wito au maamuzi ya mahakama halali nje ya mfumo wa kiserikali atajibishwa je. sheria zetu mtu anaweza kufugwa akishidwa kulipa deni je waislamu watamfunga wapi mtu aliyekula mali za yatima kama serkali haitambui mahakama ilosema kama kala mali za yatima .

MIE NAONA KODI ZA UENDESHAJI SIO ISHU ILA NI NGUMU KUTEKELEZA SHERIA NJE YA MFUMO WA SERIKALI KWANI, MTU HATAFUATA MAAMUZI YA MAHAKAMA NA HAKUNA WA KUMFANYA KITU LBD SIKU YAKUKUTANA NA MUUMBA.

Tuwekee full stop na vituo basi ili mada ieleweke.
 
[/LIST]
Duh.. unajua siku hizi mbili umenifanya nifikirie kweli. Maana muda wote ambao tumekuwa tunazungumzia "kadhi" miye mawazoni namuona mbaba fulani akiwa hivyo. Swali ni je, wanawake Waislamu wa Tanzania wanajua wanayo haki ya kuwa kadhi?

Kwamba wanawake Tanzania wanajua kama wanaweza kushika nafasi ya Kadhi ama la, siwezi kujibu ila yatosha kusema kuwa Shari`ah haikatazi mwanamke kuwa kadhi. In fact, Shari`ah iko silent on this issue. Kwa hiyo basi jambo hili limeachwa kushughulikiwa ndani ya jamii husika ya Waislam kwa ujumla wao .Ujumla huu ndio utaamua kwa kuzingatia maslahi ya jamii kwa ujumla, na na pia katika kuendeleza haki. Kwa msingi huo, hakuna sababu mwanamke asiweze kuwa Kadhi. Maadam meritocrity itatumika,hakuna haja ya kutokuzingatia uwezo katika kujaza nafasi hizi .Haitakuwa kwa manufaa ya Waislam kuzingatia "jinsia" au "nafasi maalum" za wanawake! Kigezo siyo usawa wa jinsia bali uwezo na weledi.

Kwa maana hiyo hapo juu, basi huyo anayetaka kubisha kuwa wanawake wasipate fursa ya kuwa Kadhi, itakuwa jukumu lao kuonyesha the basis of their opinion from the Qur'an and the Sunnah. Bila such bases yatosha kusema Wanawake wanayo haki kuwa Kadhi.

Watoto nje ya ndoa wakiwemo kwenye mirathi wataleta matatizo zaidi. Kumbuka Uislaam unasisitiza ndoa na hausisitizi zinaa na kama mtu aliteleza na kuzaa nje ya ndoa basi ampe mali (kama anayo) huyo mtoto nje ya ndoa na kabla hajafa na si kuleta rabsha baada ya kufa.

Two wrongs dont make a right.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom