Boney E.M.
JF-Expert Member
- Jan 22, 2007
- 425
- 35
Hali ya sasa kiuchumi sio nzuri hata katika vipato vyetu hapa Tz. Mara nyingi matumizi yanazidi uwezo wetu wa kipato. Inajitokeza kuwa kuna kisa 'live' cha wanandoa fulani wana tatizo kwani mahitaji ya mwanamke bado yako juu ilhali kipato kimepungua. Mke anamwambia mumewe sijui utapata wapi pesa sie tunachotaka ni maisha mazuri. Hili limepelekea hata mwanamume kunyimwa unyumba na kuleta mifadhaiko ndani ya nyumba hiyo. Je tuwashauri nini hawa wanandoa waendelee kuishi kwa amani? Mke hataki kupunguza matumizi na mume hana vyanzo mbadala vya kipato. je madai ya mwanamke ni halali?