Ndoa mbili ni ndoa au doa??? Ushauri

PMNBuko

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
967
154
Kuna mama mmoja ameolewa kwa ndoa ya kiislamu. Ana watoto wawili. Mtoto mmoja wa kwanza kamzaa na mume wake wa Kwanza, mtoto wa pili kamzaa na mume wake wa Pili. Huyu mwanamke anafahamika kabisa katika familia zote za wanaume hao. Na anaheshimika kama mke halali. Wazazi wa familia ya mume wa Pili wanamfahamu lakini hawafahamu kuwa ameolewa sehemu nyingine. Mume wa pili anajua ameoa mke wa mtu na yuko comfortable lakini mume wa kwanza hajui lolote. Huyu mwanamke anaamua wiki hii aende kwa mume mmoja. Sehemu moja anadanganya kuwa, mfano: Nasafiri kikazi, mara leo nimefanya kazi hadi asubuhi n.k. Lakini hasa mume wa kwanza ndiye anadanganywa make hajui kuwa mkewe amelowa kwa mume mwingine. Binafsi nimemshauri amwache huyo mume wa Pili na kama ikibidi amweleze mume wake wa Kwanza kuwa mtoto wao wa Pili siyo wa mume huyo wa Kwanza, ili apelekwe kwa mume huyo wa Pili na ikibidi aachane naye kabisa lakini amegoma kabisa kusikiliza ushauri wangu. Jamani wanaJF (hasa akina dada)mnatoa ushauri gani kwa huyo mwanamke mwenzenu??? Toeni ushauri wenu nitaufikisha sasa hivi kwake. Ahsanteni!!
 
Kuna sheria ya ndoa, nimesahau ya mwaka gani - Itafute umkabidhi huyo mama! ( Mimi dume though)
 
ipo siku huyo m.me atashtuka tu,huwezi kumdanganya m.me kwa muda mrefu hivyo.hata awe zoba kiasi gani.za mwizi arobaini,au huyo mwanamke ndio mlishaji kwa huyo mume ambae hajui?na hiyo si ndoa,huyo mwanamke anaidanganya nafsi yake
 
Asante. Nitajaribu kutafuta.
 
ipo siku huyo m.me atashtuka tu,huwezi kumdanganya m.me kwa muda mrefu hivyo.hata awe zoba kiasi gani.za mwizi arobaini,au huyo mwanamke ndio mlishaji kwa huyo mume ambae hajui?na hiyo si ndoa,huyo mwanamke anaidanganya nafsi yake

Thanks. Kusema "Mlishaji" una maana gani?? Sidhani kama atabanwa na huyo mume>>> alishatengeneza mazingira ambayo mume wake wa kwanza anamwamini tu.
 
Kama hataki ushauri mwache aendelee na tabia yake siku maji yakiwa shingoni atakuja kuomba ushauri manake kwasasa hayuko tayari kushauriwa!
 
aaaah ana hatari,ndoa kabisaaa ndoa ya pili juu ya nyingine???
mi naona achague tu sehem moja aachike.ikija kugundulika ni aibu sana.
 
Mwambie asijilinganishe na wanaume, mwanamke gani anakuwa na waume wawili? ingekuwa bwana tu angeeleweka ,mume kweli jaman?
 
mnh mie siamini kwa mwanamke unaweza olewa mara mbili,na waume zako wasijue kama wako wawili....acha kutupima bana.:twitch::sick:
 
huo ni uasherati kama mwingine.awe mkweli kwa mumewe wa kwanza.siku za mwizi arobaini.sheria ya ndoa inazungumzia kuhusu ndoa za wake wengi au mmoja lakini haisemi ndoa ya mke moja wanaume wawili,hii hatari kabisa.
 
mnh mie siamini kwa mwanamke unaweza olewa mara mbili,na waume zako wasijue kama wako wawili....acha kutupima bana.:twitch::sick:

Huo ni ukweli na mambo hayo anayafanya kweli. Tena juzi Jumamosi alikuwa kwa mume wa pili. Anamcare kwa kila kitu. Inatosha kusema tu kwamba. Ana wanaume wawili and that's all. Kama unavyofahamu mke na mume. Basi, na huyu dada anaishi vivyohivyo, iula tofauti tu, waume wawili, yeye (mke) mmoja. Lakin game linachezwa dhidi ya mume wa kwanza.
 
Mimi bado haijaingia akilini vipi aweze kumudu ndoa mbili bila mmoja wa kwanza kushtuka.
Kama ni kweli nadhani pamoja na makosa ya huyo mama mume wa kwanza naye anamatatizo ya kimaono juu ya mkewe, pia mme wa pili ndio hamna kitu kabisa yaani unaoa mke na unajua ameolewa na unakubali kuwa atawafanyia zamu za kulala, na hapo yeye wapili ndio atanyanyasika zaidi maana anajua anaiba hata akiambiwa tulia mwezi huu siji maana naona kama anastuka itabidi akubali.
Hapa tutamlaumu sana huyu mama lakini stori hii inaonyesha udhaifu mkubwa kwa sisi wanaume, na katika hili ntasimamia kuwa wanaume ndio chanxo cha kupelekea huyo mama kufanya hivyo maana kama mmojawapo angekuwa strong naamini yasingetokea hayo yote
 
Asante mkuu. So tumshauri je? kwa mwonekano wa nje naona mwanaume wa kwanza yuko fiti, ila sisi watu wa nje hatujui kama yuko strong au vipi! Lakini hivi ni sababu kama zipi zinamfanya mke aamue kuolewa nje??????? Tamaa?? Kukosa huduma ya kimapenzi kwa mumewe?? Au ni nini??
 
Mkuu sikumaanisha kuwa mme wa kwanza labda hamtimizii ndio maana akaolewa tena(ingawa pia inawezekana)
 
Mkuu ndio maana nikasema mimi haiingi akilini kabisa KAMA NI KWELI IPO HIVYO.
Kabla sija mnyooshea kidole huyo mama mimi nalia na hao "waume" zake kama kweli wako timamu.
Kwanini tunaoa? inawezekana vipi wewe mwanaume unakaa mji mmoja na mkeo wiki hii analala wapi siju wiki ijayo kwako inayofuata tena na tena na tena hadi anazaa na mtoto inamaana wanamuda mrefu hata ktk hali hiyo na wewe mume unaona its ok.
Je watoto wanakaa kwa mume yupi au kila mtu anakaa na wake impossible!!!.
Ndoa yapili inatimiza matakwa gani? kidini, kisheria au kitamaduni zetu? none of them!!!!!!.
Mume wa kwanza ni mzembe wa kusimamia ndoa yake, wapili ni lofa nadhani hata mtoto atakuwa anatunziwa na mwenzie nahisi labda inawezekana jimama liko fiti kimavumba linamuweka town na hana say yoyote bali kufuata matakwa ya mama ili aishi mjini.
Mume wa pili ashauriwe pia
 
Kama hasikii muache....life is a teacher....subiri kidogo....nawahurumia waume watakaoumia.....:coffee:
 
Kuna mama mmoja ameolewa kwa ndoa ya kiislamu. Ana watoto wawili. Mtoto mmoja wa kwanza kamzaa na mume wake wa Kwanza, mtoto wa pili kamzaa na mume wake wa Pili. Huyu mwanamke anafahamika kabisa katika familia zote za wanaume hao. Na anaheshimika kama mke halali. Wazazi wa familia ya mume wa Pili wanamfahamu lakini hawafahamu kuwa ameolewa sehemu nyingine. Mume wa pili anajua ameoa mke wa mtu na yuko comfortable lakini mume wa kwanza hajui lolote. Huyu mwanamke anaamua wiki hii aende kwa mume mmoja. Sehemu moja anadanganya kuwa, mfano: Nasafiri kikazi, mara leo nimefanya kazi hadi asubuhi n.k. Lakini hasa mume wa kwanza ndiye anadanganywa make hajui kuwa mkewe amelowa kwa mume mwingine. Binafsi nimemshauri amwache huyo mume wa Pili na kama ikibidi amweleze mume wake wa Kwanza kuwa mtoto wao wa Pili siyo wa mume huyo wa Kwanza, ili apelekwe kwa mume huyo wa Pili na ikibidi aachane naye kabisa lakini amegoma kabisa kusikiliza ushauri wangu. Jamani wanaJF (hasa akina dada)mnatoa ushauri gani kwa huyo mwanamke mwenzenu??? Toeni ushauri wenu nitaufikisha sasa hivi kwake. Ahsanteni!!

Mke kuolewa na mume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja yaani kuwa na waume wawili na kuendelea haruhusiwi.

Sheria inakataza mke kuolewa na waume wengi kwa wakati mmoja kwani ni kinyume na fitrah- maumbile ya asli, huyo mwanamke ajuwe kabisa anafanya hiyana na ni uzinifu. Na huyo mume wa pili anaingia kwenye kundi la wazinifu vile vile, sheria ya dini na hata ya serikali haitambui ndoa yao.
 
Back
Top Bottom