ndoa/mapenzi thru mitandao ya kijamii

Wewe si unaona watu humu wanasema eti wako kwenye ndoa lakini kutwa kucha humu wanaitana majina ya kimahaba na wenza wao wa kimtandao....halafu ukiwauliza kama wenza wao wa kikweli wanajua kama wamo humu wanasema hawajui!

Sasa hapo ukiongeza na mambo ya multiple IDs ndo inakuwa vurugu mechi tupu.

Utaona mtu kishaandika hapa kwamba ni mke/mume wa mtu halafu anakutana na mtu hapa wanaanza kuitana darling, la azizi, sweetie, mpenzi bila hata ya kuwa na staha ya ndoa zao! labda ndio katika juhudi za kutafuta umaarufu kwa nguvu. Halafu mashabiki wa uzinzi wanashangilia kwa kuwaita wahusika shemeji, wifi na uozo mwingine! Cha kushangaza wamiliki wa huu mtandao wanafumbia macho uchafu huu wasipokuwa makini patageuzwa hapa na kuwa the "great danguro of JF."
 
Back
Top Bottom