Ndoa-je ni kawaida kuhisi hivi kuhusu ndoa?

sweetdada

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
517
169
Natumai wote mu wazima wanaJF.

Jamani kuna kitu chaniogopesha bado niko njia panda nahitaji kujua kwa kina.

Nakaribia kuingia kwenye ndoa,ninampenda huyu husband to be ila kila nisomapo,nionapo ndoa za ndugu jamaa na marafiki kwa kweli naogopa mnoo,nimechengachenga mara mbili ila safari hii sina ujanja.

Nachotaka kujua ni je maisha ya ndoa yakoje,mazuri,mabaya,kama uchumba au tofauti ni ipi na maisha ya boyfriend girlfriend?I wish kungekuwa na ndoa za mikataba hapa kwetu yani tumbo linauma kwa uoga. Je hii ni kawaida au nina tatizo la kisaikolojia?

Nahitaji michango yenu yenye busara.

Sweetdada.
 
Huna ujanja?Unataka ndoa ya mkataba?
Ukishaingia kwenye ndoa na mawazo ya aina hiyo tegemea sana kuhisi uko trapped utakapokuwa ndani.Kwahiyo jitahidi uondoe hizo fikra kichwani.

Kuhusu swali lako, pamoja na kwamba ndoa nyingi zinaonekana kuwa na matatizo usizitumie hizo.kama reference kwasababu tatizo halipo kwenye ndoa bali lipo kwa wanandoa.Wao ndio wenye matatizo. Hivyo wewe na mwenzako mkiingia kwa malengo, mkiwa tayari kusaidiana na kuongozana mtafurahia ndoa yenu. Jiandae tu kwa majukumu ambayo hukua nayo kipindi cha uchumba (kudeal na wakwe, mawifi na mashemeji, kuishi na mtu mwingine ambae anaweza akawa tofauti na wewe full time, kuwa msaada kwa mumeo n.k).

Alafu kama mlikua na uchumba mzuri na wote mlikua genuine mnaweza mkaendelea hivyo hivyo kwenye ndoa, plus majukumu zaidi. Kuweni marafiki, boresheni mawasiliano kila siku , heshimianeni maisha yatasonga.
 
dah ni ngumu sana kutell apart pre wedding jitters na general negativve view ya ndoa

mie naona wewe unna negative view ya ndoa na nisinge kushauri uolewe kwa sasa.
 
Natumai wote mu wazima wanaJF.

Jamani kuna kitu chaniogopesha bado niko njia panda nahitaji kujua kwa kina.

Nakaribia kuingia kwenye ndoa,ninampenda huyu husband to be ila kila nisomapo,nionapo ndoa za ndugu jamaa na marafiki kwa kweli naogopa mnoo,nimechengachenga mara mbili ila safari hii sina ujanja.

Nachotaka kujua ni je maisha ya ndoa yakoje,mazuri,mabaya,kama uchumba au tofauti ni ipi na maisha ya boyfriend girlfriend?I wish kungekuwa na ndoa za mikataba hapa kwetu yani tumbo linauma kwa uoga. Je hii ni kawaida au nina tatizo la kisaikolojia?

Nahitaji michango yenu yenye busara.

Sweetdada.

Kwani Unaolewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki? Ndo utakuwa Mke wao?
 
Ipo kazi, kama tu ukiwaza kuolewa wachanganyikiwa, sasa waolewa nini?

Hadi unamchenga?
Eti huna ujanja?
Wataka mkataba?
 
Matatizo nyie wanawake wnegine mnavamia wavuta bangi ndo mana mnaogopa kuolewa.
 
Huna ujanja?Unataka ndoa ya mkataba?
Ukishaingia kwenye ndoa na mawazo ya aina hiyo tegemea sana kuhisi uko trapped utakapokuwa ndani.Kwahiyo jitahidi uondoe hizo fikra kichwani.

Kuhusu swali lako, pamoja na kwamba ndoa nyingi zinaonekana kuwa na matatizo usizitumie hizo.kama reference kwasababu tatizo halipo kwenye ndoa bali lipo kwa wanandoa.Wao ndio wenye matatizo. Hivyo wewe na mwenzako mkiingia kwa malengo, mkiwa tayari kusaidiana na kuongozana mtafurahia ndoa yenu. Jiandae tu kwa majukumu ambayo hukua nayo kipindi cha uchumba (kudeal na wakwe, mawifi na mashemeji, kuishi na mtu mwingine ambae anaweza akawa tofauti na wewe full time, kuwa msaada kwa mumeo n.k).

Alafu kama mlikua na uchumba mzuri na wote mlikua genuine mnaweza mkaendelea hivyo hivyo kwenye ndoa, plus majukumu zaidi. Kuweni marafiki, boresheni mawasiliano kila siku , heshimianeni maisha yatasonga.

Lizzy my dear, asante nimependa mchango wako.
Nimesema sina ujanja kwa kuwa ninataka kuingia kwenye ndoa na huyu mtu na kuanza familia,nimekuwa mgumu kutoa maamuzi kwa kuwa marafiki zangu wengi wanalalamika kuhusu ndoa zao, nina ndugu wenye matatizo na ndoa zao, na mbaya zaidi mimi binafsi nimekuwa kwenye familia yenye wazazi wote wawili wanaoishi nyumba moja lakini ni afadhali kila mmoja angechukua ustaarabu wake..nadhani nikifikiria hayo yote ndiyo yananifanya niwe mwoga nikidhani na mimi ya kwangu itakuwa hivyo.

ningependa kuwa kwenye ndoa ya mpaka kifo kitutenganishe hilo la mkataba limenijia tu kama solution baada ya kuona kwanini watu wang'ang'aniane matatizo siku zote 365 kesi kila leo!! Namuomba Mungu anisaidie kwa kweli.
 
ni kijana mstaarabu na sio mvuta bangi, uoga wangu ni kutokana na ndoa nyingi nizionazo
Sasa sweeetdada hivi wewe unadhani ndoa zote zitakuwa sawa? Yani wewe na dada yako mlio zaliwa tumbo moja hamko sawa, vipi ndoa ziwe sawa.

Wewe kama umependa olewa tu, kama hujapenda hapo bora ukae pembeni ungojee uliye mpenda.
 
Nadhani kuwa baada ya kuogopa sana, na kupiga chenga, na saa umefanya maamuzi ya kuolewa, umefanya tathmini ya mambo muhimu kwako.
nadhani umeshawaza jinsi utakavyojiepusha na mambo usiyoyapenda,
mengine unayaacha tu.
Muhimu kama walivyosema hapo juu usiingie ukiwa na lengo la kuvizia tatizo ukimbie.
matatizo yako mengi sana, hayana hesabu, mtazamo wako juu ya hayo matatizo, na reaction yako ndio itakayokutofautisha na hao unaowaona.
all the best, karibu kwenye chama kizuri ajabu, kama akili zako ziko kichwani
 
Toa fikra mbaya akili mwako,japo inawezekana mazingira uliyokulia nawatu wanaokuzunguka ndoa zao zina matatizo ni zamu yako kuhakikisha ndoa yako inakua ya tofauti kwa kuifikiria positivu na utaona ndoa yako inaenda vizuri,mie mwenzio bado naivutia pumzi nikiingia humo nimejipanga kuenjoy tu na hakuna kuachana mpaka kifo!ckubali wala kuruhusu binadam yoyote awe sababu ya kuvunja ndoa yangu!uvumilivu,iman na busara vitadumisha ndoa yako!
 
Nadhani kuwa baada ya kuogopa sana, na kupiga chenga, na saa umefanya maamuzi ya kuolewa, umefanya tathmini ya mambo muhimu kwako.
nadhani umeshawaza jinsi utakavyojiepusha na mambo usiyoyapenda,
mengine unayaacha tu.
Muhimu kama walivyosema hapo juu usiingie ukiwa na lengo la kuvizia tatizo ukimbie.
matatizo yako mengi sana, hayana hesabu, mtazamo wako juu ya hayo matatizo, na reaction yako ndio itakayokutofautisha na hao unaowaona.
all the best, karibu kwenye chama kizuri ajabu, kama akili zako ziko kichwani

Asante Haika kwa mawazo na ushauri wako.nitatia maanani uyasemayo. Ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom