ndoa inanishinda nipen mawazo yenu

habari wana jamii forms, napenda mawazo yenu na michango mnayotoa humu,,mimi ni mama wa mtoto mmoja nina miaka 23
naomba msaada jamn,nina mume ambaye nipo nae kwa miaka sita na nimezaa nae mtoto mmoja, kiukweli huyu kaka ni malaya cna kutokana na tabia yake hapo nyuma kwani aliowa wake 2 kabla yangu na wakaachan akidai hawafai walikuwa na tabia mbaya

ameshanisaliti mara nyingi sana mpk sasa na ushahidi nikapata lkn aliomba msamaha coz nlikuwa bdo nampenda tukaendelea na maisha,,

hivi sasa kanikataza kushika simu yake yaani tunagombana kila siku, kuna siku nilikuta kamtumia binti fulani pesa kwa njia ya m-pesa nilipomuuliza ni nani tuligombana cna akadai ni mama wa mtoto wake,, lakini nilichunguza nikakuta ni uongo kwani namba ya mzazni mwenzake naijua na hawezi kumuita mpenzi kwani huyo mzazi mwenzake keshaolewa,,

nilimpigia huyo binti nikamuuliza yeye ni nani lakini matokeo yake alinitukana akaniambia sijaona wanaume nini???akasema yy hakumtongoza mume wangu bli mume wangu ndiye aliyemtongoza kiukweli niliumia cna nikalia mpaka nikachoka,,nikataka nirudi kwetu lakini nikaenda kwa mama mmoja rafiki wa familia akanishauri nisiondoke nikae nivumilie,,
kwa upande mwingine huyu mume wangu ananijali na familia kwa ujumla lakiniatatizo ni umalaya,,
natamani hata nitoke jne coz na mm najijua ni mzuri bado nafikiria nahitaji mawazo yako.

Waache mwewe waruke angani kuku endeleeni kutembea ardhini. Inamaana wewe unasubiri kengele ndio ujue lakuamua? Au hujui one mistake one goal. Ustaarabu duniani?! Nani kasema ! Au ukimwacha utakonda? Kama vipi mpe nafasi aliyetayari. Huu mtazamo tu.
 
'Mpende akupendae' na 'kisicho riziki hakiliki' na mwisho 'la kuvunda halima ubani' mmeo huyu ni serial cheater na huenda hatumii condom,tafakari..............
 
Pole sana, since umeweka email yako nitakuemail , nijaribu kukusaidia...ushauri wangu:
Kama huyu bwana anatoa hela bila shida na wewe hujasoma, muombe uende nje kusoma na mwanao walau first degree afund kila kitu...
Kama nje ni shida tafuta shule hapahapa , so u r busy with sth, naomba usiendelee kukutana naye kimwili, the most u can get out of this is quality education, mengine nitakuadvice, kama una ujuzi wowote na huna kazi, nipm nitakusaidia

Eng Nsiande
Nsiande ushauri wako ni mzuri sana nauafiki lakini hapo kwenye nyejundu mh....hapana na pananifanya nijiulize mara mbili...Mke wa ndoa, unamkatalia mumeo on what grounds?? Ni malaya!!! ushahidi?

Jamani nyie watu hebu achem mashara usijeshangaa akichukua uamuzi huu akafikishwa baraza ka msisiri kwa kesi ya kumnyima mumewe haki ya ndoa (na nakuhakikishia hadi kanisani mume ataungwa mkono) Mke huna mamlaka juu ya mwii wako kwa mumeo naye kwako.........sasa sijui utaanzia wpi kumnyima ah........nyie acheni tu
 
cha msingi bidada umri wako bado mdogo waweza olewa tena kwann usubili maradhi kwan hao wenzako c waliolewa kwann ww usiondoke wenzako wameondoka kuna wengine wanaushaur wa pumba ni bora kuwapotezea mbn wenzio wameolewa na wamezaa na hyo mumeo hapo chapa rapa
 
Nsiande ushauri wako ni mzuri sana nauafiki lakini hapo kwenye nyejundu mh....hapana na pananifanya nijiulize mara mbili...Mke wa ndoa, unamkatalia mumeo on what grounds?? Ni malaya!!! ushahidi?

Jamani nyie watu hebu achem mashara usijeshangaa akichukua uamuzi huu akafikishwa baraza ka msisiri kwa kesi ya kumnyima mumewe haki ya ndoa (na nakuhakikishia hadi kanisani mume ataungwa mkono) Mke huna mamlaka juu ya mwii wako kwa mumeo naye kwako.........sasa sijui utaanzia wpi kumnyima ah........nyie acheni tu


akishindwa basi atumie kondom,mumewe akimuuliza why using a condom,,,amweleze mumewe hofu yake juu yake...kama mume ana akili atasikiliza kilio cha mkewe......

otherwise tendo la ndoa litumike kuweka sanctions,hakuna kumpa mpk awe na uhakika amejirekebisha umalaya wake mume ACHOOSE kama anataka bado kushiriki na mkewe then ajirekebishe au imekula kwake....hata wakipelekwa kanisani/mahakamani wakisikia story yake/upande wa pili napo watakubaliana kuwa this is necessary to keep her safe...

otherwise huyo baba ni FATAKI anatake advantage kuwa mkewe ni mdogo sana hawezi kujiwekea maamuzi and she is also financially insecure...........miss nora,tambua wewe ni mama ushakuwa mtu mzima you can make decisions,muonyeshe huyu baba you can make decisions INDEPENDETLY without him,fuata ushauri wa Nsiande kama huna shule ingia shule tafuta kazi huyu baba akishakuona unaprogress and you can stay well without him trust me ataanza KUKUHESHIMU...

POLE SANA,i guess wanajaamiii tuwe tunakumbukana katika maombi kwa wenzetu wanaopitiwa na mitihani kama hii....
 
Mama/Binti uliyataka mwenyewe vumilia mama ingawa sina uhakika kama uvumilivu nao hauna mwisho! Ila jua siku moja yatakukuta makubwa zaidi ya hayo unayoyashuhudia sasa hivi!
 
Dada yangu pole sana ,kwanza sali sana kwa mungu kwa kumwombea toba mumeo kama kuna vifungu vya ibirisi vilivyo mfunga Mungu amfungue,omba toba pia kwa ajili yako,pili mwanamke ni msimamo usibabaishwe na na hali yake ya uchumi bali mueleze kuwa unakerwa na tabia yake ya UMALAYA,
Usiache kumpenda lakini ni vema ukapima Afya yako,na ukatafuta kitu cha kukuingizia pesa ili asiendelee kukukwaza mradi uweze kujilinda wewe na mtoto,
Usifikire swala la kutoka nje ya ndoa dada,hilo sio suluhisho katika maswala ya ndoa ,Mungu ni kila kitu Mungu ndie atakae kusaidia ,MUNGU AKUPE NGUVU.
 
Hakufai hakufai hakufai!
Usiendelee kupoteza muda wako na kujiweka katika hatari ya magonjwa!
Siamini kama ni husband from heaven huyo; so unavyoendelea kukaa naye ndivyo unavyomzuia mume ambaye Mungu amekupangia!
Hao wanaokuambia uvumilie, sidhani kama watakuwa wa msaada kwako au kwa wanao; yale ambayo hatuombi yatokee yakitokea!
 
“A great marriage is not when the 'perfect couple' come together. It is when an imperfect couple learns to enjoy their differences.”:bounce:

Siamini one can learn to enjoy this kind of differences!
 
nashukuru sana kwa ushauri naomba kama kuna mama au mdada au mtu yyte anayeguswa na mm anipe mbinu za kufanya ili niachane nae kwan me mwenyewe nashindwa,,email yangu ni salome_kayombo@yahoo.com

Yaani natamani sana niongee na mama na dada yako, niPM ili tuone kama itasaidia! Pole sana mdogo wangu, yataisha na wewe utasaidia wengine kwa kurefer experience yako!
 
Mydia.......ninachowezakukueleza ni kuwa wakati watakapojitokeza wengi kukushauri nini cha kufanya chukua ushauri wao changanya na akili zako. Ninaelewa kwa wale wapigania hali za wanawake watakuwa wengi sana kwani nia yao ni kumkomboa mwanamke mwenzao ambae kwa mtazamo wao anaonewa........but nakushauri tafuta na ushauri toka upande mwiongine.....mtu/watu ambao wana experience ya maisha ya nje ya ndoa (kwa maana ya walioachana na wenzi wao) hawa nao wakupe experience yao..........si ahisi kama unavyohisi.....kuna challenges as well ambazo pengine zitakufanya utamani ungekuwa bado na mwenzi wako.

So pata experience za pande zote kisha chambua ndipo uamue........usikurupuke
 
Mwambie akufungulie biashara ambayo wewe uakuwa unaimanage huku unasave akiba yako kisiri siri. Biashara ikichanganyia na wewe kuwa na uhakika wa kutokuwa tegemezi kwake kula kona fasta ikiwezekana akupe talaka yako.

Your too young kuvumilia haya madhila ya mume muhuni. Pole sana bibie.
 
Kwa mtu ambaye ndoa anaijua kwa kusoma vitabu au amabaye hajawahi oa ni lazima ushauri atakaotoa hapa siyo practical kwani utatokana na theory zaidi. Kuacha ndoa na mtoto mmeshazaa huwa ni ngumu sana jamani haswa ukifikiria mateso ya mtoto na ukizingatia kwamba huyu jamaa ataendelea kuvuta mwinine. Dada ni kwamba kila ndoa ina matatizo na kinachotofautiana ni aina ya matatizo na kiwango cha uchungu kinacholetwa na hayo matatizo. Nakushauri utafute watua wanaoheshimiana na huyo mumewo pamoja na wazazi wake mumketishe kikao na kumwonya na atubu. Pia kama kuna uwezekano mpeleke kwa viongozi wenu wa dini ili mkayajadili. mi sishauri kuachana kwani inaacha kovu kubwa sana kwa maisha ya watoto.
 
Sheria ya ndoa Tz haiko clear kama unavyodhani. Kama alikuwa si mwanafunzi kuolewa na huo umri ruksa.

huyo hakufai kwa kuwa kama una miaka 23 alikuoa ukiwa @17. alikubaka na anapaswa kushtakiwa. pili, ukiwa tayari kutoka nje unijuze. swala la umalaya ni hatari muulize kama huwaga anatumia condom na ikiwezkana utest hiv na yeye pia. kama mko neg ataogopa kutoka nje. ila usisahau kunijuza ukianza kale ka mpango ka kumuvu auti.
 
I totally agree with you. Kudai talaka sio solution. Nina dada yangu yeye mumewe alifariki wakati yeye bado anadai sana tu. Jinsi alivyokuwa anawapanga wame za watu wakati mume wake tunahisi kafa na gonjwa la kisasa tulikuwa hatuna hamu kabisa. Unatamani umzukie jamaa umwambie anatafuta kifo unashindwa.

Back to the point, mnaosema adai talaka are you sure she can abstain from having sex after divorce? Au ahachike na kuwa kimada wa wame za watu? Si kila mtu anaweza kuishi single. Kingine inaelekea mdada hana kipato kwani ameolewa mdogo maanake hana elimu. Its better to die in marriage than otherwise kwani ukimwi hauko kwenye ndo peke yake.



Kwa mtu ambaye ndoa anaijua kwa kusoma vitabu au amabaye hajawahi oa ni lazima ushauri atakaotoa hapa siyo practical kwani utatokana na theory zaidi. Kuacha ndoa na mtoto mmeshazaa huwa ni ngumu sana jamani haswa ukifikiria mateso ya mtoto na ukizingatia kwamba huyu jamaa ataendelea kuvuta mwinine. Dada ni kwamba kila ndoa ina matatizo na kinachotofautiana ni aina ya matatizo na kiwango cha uchungu kinacholetwa na hayo matatizo. Nakushauri utafute watua wanaoheshimiana na huyo mumewo pamoja na wazazi wake mumketishe kikao na kumwonya na atubu. Pia kama kuna uwezekano mpeleke kwa viongozi wenu wa dini ili mkayajadili. mi sishauri kuachana kwani inaacha kovu kubwa sana kwa maisha ya watoto.
 
Back
Top Bottom