Ndoa imekuwa ndoano....!

Sabry001

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,064
353
Hallow wapendwa wa hapa MMU, za leo? Jamani mkistaajabu ya Musa utayoana ya firauni! Nadhani ni last week niliwapa story ya I'L KILL HIM 4 MY KIDS, bs jana yametokea ya kutokea, yule dada kanipigia simu kaniambia yule mwanamke alieolewa na mtalaka wake amemjia kwake anamlilia amsaidie kuondokana na balaa la yule mwanaume. Eti mwanaume halali nyumbani, anachukua mshahara wake, anampiga na mbaya zaidi analetaga wanawake wengne humo humo ndani anapoishi analala nao. Sasa eti kamfata huyu rafiki yangu anamuomba ampe ujanja wa jinsi alifanya kipindi kile mpaka akaweza kuondokana nae. Huyu best yangu ameniambia akikumbuka nyodo za huyu dada alivyokuwa anamzaraugi, anam2kana, anamsingizia mambo ya uongo na zaidi alivyomchukua mumewe hadi akamuoa, leo yamemkuta zaidi ya yale yaliyomkuta mwaka 2005, alijickia kulia na kucheka ila ki2 pekee alichoweza kumwambia ni umevuna ulichopanda,ila km umechoka ondoka nenda kwenu au muwekee sumu kwenye chakula afe! Haha.... Kwa kweli nimemuona huyo mwanamke hana akili, eti unaenda kumuomba ushauri mwanamke uliemvunjia ndoa eti umfanyeje mume? AMA KWELI MALIPO NI HAPA HAPA NA SIO AKHERA!
 
Malipo duniani. Mume wa mtu sumu!!
Nafikiri ushauri aliompa wa kuondoka ni mzuri kuliko wa sumu. Usishangae shosti maana maji ya shingo yakikufika unatapa tapa.
 
Ukipanda mema utavuna mema,ukipanda mabaya nayo pia utayavuna!thus mwachen ale matunda machungu aliyoyapanda,si alifikir atafaidi!cha mtu sumu
 
Mh pole yake,ila na sie wanawake tujifunze mwenzio aliondoka na wewe unaenda kujipachika tu,hukai chini ukatulia ukajiuliza tena kwa makini kama mwenzangu kaondoka mie nitapaweza kweli! Siku zote mfupa uliomshinda fisi usidhani wewe mbwa utauweza!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom