Filipo
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 9,342
- 5,536
Ninachojua mimi ni kwamba, kanisa haliwezi kuvunja ndoa. Pale inapoonekana kuna mapungufu yoyote kama uzizi, kichaa, uchawi au kutokuelewana kabisa ndani ya nyumba, basi kanisa linaweza kuridhia mtenganishwe na sio kuvunja ndoa maana kanisa linaamini kwamba ndoa inaunganishwa na Mungu. Na alichokiunganisha Mungu, binadamu hawezi kutenganisha!
Chakufanya hapo, kwa mtizamo wangu ni kwamba, huyo dada adai talaka huku akijua kabisa kwamba hataweza kufunga ndoa yoyote ya kikristu. Labda serikalini au dini nyingine. Kwa kweli imekula kwake.
Kuhusu huyu jamaa, aende akawaone madaktari kwanza wamwambie tatizo lake hasa ni nini na kama lina tiba atumie. Wengi walikuwa na tatizo hili, wakapata matibabu wakapona. Kwahiyo akapimwe kwanza. Kama halina tiba, sina la kusema zaidi ya kumpa pole.