Ndiyo Waswahili na Yanayotufanya Tuwe Waswahili??

Mkwaruzo

JF-Expert Member
Feb 21, 2011
563
98
1. Unawasalimia watu usiowajuwa na kutaka urafiki na kila
anayetaka kuzungumza na
wewe, halafu unaanza kumwita mtu huyo (usiyemjuwa undani wake wala tabia zake)aunt au anco!.
2. Asilimia 90 ya CD pamoja na cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki (sio original copies).
3. Stoo yako imejaa vitu
(makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji. Kwa mfano, karpet
ukilitoa hulitupi n.k.
4. Una machupa ya maji matupu na ya shampoo, chupa za perfume pamoja na vipodozi
vingine umeweka tuu kwenye rafu au meza yako wala huna shughuli navyo.
5. Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali, chidi, mamu, dida, kibabu, n.k.
6. Hakuna mtu katika familia yako anayetoa taarifa kwako
anapo kuja kukutembelea,
wanajileta tu, hata hawatazami idadi ya watu wanaokuja wala kufikiria watalala wapi!
7. Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.k ulivyochukua sehemu kama vile mgahawani
(Restaurant).
8. Mama yako ana migogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa siku 10 au zaidi.
9. Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga
ni nafuu (mfano usiku sana) na mara nyingi huwa una beep tu hutaki kujitia hasara hata kama
wewe ndiye uliye na haja hiyo.
10. Ulipokua mdogo nguo
unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi.
11. Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa, kwa
kuwa unataka kumridhisha kila mtu kwa zawadi huko unakokwenda.
12. Unapomsaidia mtu na
akafanikiwa basi utakuwa
unapita na huku unasema kama sio mimi asingekuwa vile yule.
13. Wale tunaowasaidia wengi wanakosa shukurani na badala yake wanasema, eti kaniletea kijisimu hiki, si hata hapa ningeweza kukipata? Ndio zawadi ya Ulaya hii?! Halafu
wanacheka!
14. Hatuvai nguo nzuri au mpya na kujipamba tunapokuwa majumbani mwetu isipokuwa
tunapokwenda maharusini,
khitma au kwenye mialiko ya futari au pale tunapoalikwa vyakula na marafiki!
TUBADILIKE!!
 
pamoja na kuweka post hii hivi, najuwa kuwa na wazungu wana mabaya yao, waarabu na mabaya yao, wachina pia wanayo mabaya yao na wengineo, hivi na wao wanajinasibisha na mabaya yao kupitia lugha (au asili yao)?
 
Lakini umesahau yakuwa unapenda kuwasema watu maovu yao na kusahau mazuri yao.
 
Back
Top Bottom