Ndiyo Hosea ulisema ziko kesi 5 kubwa so far tumeona 3 Ulimaanisha hizi?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Leo nimeona nirudi hapa mkekani kuuliza hili swali kama kawaida yetu tukiwa tunataka kujifunza .

Majigambo , majivuno , matambo na vijembe vilimwagwa kwa nyakati mbali mbali .Baadaye tumeona matukio ambayo wengi wanayaita kiini macho nami naitikia kwamba huenda yakawa maigizo kweli .

Sasa tumesha ona kesi za EPA , Mramba na madaraka mabaya na sasa Mgonja.Je tuamini kwamba ulikuwa una maanisha kesi hizi na bado 2 au ulikuwa humainishi hili bado kesi hizo zinakuja ?

Waziri mkuu fate ya Hosea na Mwanyika namna gani ama wewe uko likizo kama majaji hadi urudi ndipo useme kinacho endelea ?
 
Wajuvi hakuna aliyeko karibu na Hosea na Pinda atupe yanayo jiri huko ndani ?
 
I thought Mramba, Yona and Mgonja was one case?

Mimi nimezitenganisha ili nione kama hizi ndiyo hesabu za Hosea ama ni mie nakosea ?Ndiyo maana nauliza kama kuna mjuaji atupe ajualo .
 
Kiongozi Lunyungu

Source yangu moja ilijulisha hata kabla sekeseke halijaanza kuwa, watakaofikishwa Mahakamani ni pamoja na:

Mramba
Yona
Mgonja
Vicent Mrisho
Karamagi
Chenge
Lowassa na
Mwandosya
 
Mdau Lunyungu! Kwa mahesabu ya Hosea nadhani hapo hujakosea kitu, suala la Karamagi nadhani DPP amerudisha jalada kwa kuwa cha kumshitaki jamaa 'hakionekani'. Kwa sasa waliobaki nadhani ndo wale Pinda anaosema nchi itatikisika na nadhani ni zamu ya Lowasa (kumbuka huyu anaheshima ya uwaziri mkuu).

Kwangu mimi nchi isitikisike kwa kumpeleka mahakamani huyu jamaa na hapo ndo tutaweza kuona mapungufu makubwa yaliyokatika katiba yetu

KATIBA BORA NI ILE INAYOTENGENEZWA KWA MANUFAA YA UMMA
 
Wadau nina washukuru kwa kunifungua masikio nisikie na macho nione .Mie sasa nangoja ila kama Karamagi hana la kujibu basi Lowasa atakuwa hana pia maana skandali lao si moja ama ilikuwaje siku zile ?
 
Mkuu Lunyungu, si akina Lowassa na akina Karamagi pekee wasio na la kujibu, kwani hata hao akina Mramba, ukichunguza kwa undani, wana lolote la maana linaloweza kuwaletea matatizo (basing on kind of mashitaka yaliyofunguliwa dhidi yao?
 
Back
Top Bottom