ndivyo wanaume wawazavyo kuhusu sex

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
Kama madege yanavyotua na kuondoka ndivyo mawazo kuhusu sex huja yenyewe kwa mwanaume! Binadamu hawezi kuwa amekamilika akiwa kimwili na kiroho peke yake bila hisia (emotions).
Pia kuna tofauti kubwa sana namna mwanamke na mwanaume wanavyoweza kufanyia kazi emotions kwenye ubongo.

Bila kufahamu tofauti hizi kati ya mwanaume na mwanamke wakati mwingine hupelekea suala la mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume kuwa na matatizo hasa kutokana na upande mwingine kushindwa kuelewa mwenzake anahitaji nini au kitu gani na wakati gani.

Linapokuja suala la emotions mwanamke ana uwanja mkubwa sawa na barabara yenye uwezo wa kupitisha magari 8 kwa wakati mmoja (eight lanes super highway) wakati mwanaume ni sawa na barabara moja ya kwenda kijijini kiasi kwamba magari hata mawili kupishana ni kasheshe.

Hii ina maana kwamba kumkumbatia mwanamke huweza kumpa raha na msisimko wa ajabu kihisia na kumsikiliza akiongea humpa raha na kumpa ahuaeni kuliko kawaida.
Wakati mwanaume kuongea sana bila kutoa point kwa maneno machache anaona unampotezea muda wake.

Pia mwanamke huweza kukumbuka kutukanwa, au kupigwa na anaweza kukumbuka rangi ya chumba mlichokuwa wakati wa hilo vagi, shati mwanaume ulivaa, sura yako wakati mnapigana au kutukanana na siku, mwezi na mwaka kwa kuwa inahusishwa moja kwa moja na hisia zake kwenye hiyo super highway, wakati mwanaume anaweza akawa baadhi ya vitu hakumbuki.

Wanawake hupenda kuongea kuhusu hisia zao all the time.

Linapokuja suala la kuwaza kuhusu sex basi mwanaume huweza kuwaza kuhusu sex kila baada ya dakika mbili na mwanamke huweza kuwaza sex wengine ni siku kadhaa katika mwezi.
Je, ndo kusema mwanaume muda wote yupo kwenye foreplay na ndiyo maana huwa na dakika chake akikutana na mwanamke na kutaka kwenda south pole moja kwa moja kuchimba gold hata kabla mgodi haujawa tayari!

Kuingia na kutoka kwa mawazo kuhusu sex kwa mwanaume ni sawa na ndege zinavyoingia na kutoka katika International Airport kama vile Amsterdam, au London Heathrow na mwanamake ni kama kiwanja cha ndege kule Nduli - Iringa kiasi kwamba wakati mwingi ndege hata zikifika zinaweza zisitue hadi hali ya hewa iwe nzuri (hadi mwanamke akaribie kuwa fertile)

Hii ina maana kwa mwanaume mawazo kuhusu sex hutua kwa wingi kama madege makubwa kila baada ya dakika mbili (kutua na kuondoka) na mwanamke ni sawa na kiwanja kidogo ambapo ndege ndogo za mawazo ya sex (tena private jet) hutua kwa mwezi angalau siku chache tu au kwa siku mara moja.
Kwa mwanamke foreplay ni saa 24 kabla ya sex, wakati mwanaume foreplay ni dakika 3 kabla ya sex.
Hapa bila mwanaume kufahamu tofauti iliyopo na mwanamke mahusiano ya mapenzi huweza kuwa ya kuumiza au kutimiza wajibu tu.

Ndiyo maana linapokuja suala la kutaka sex mwanaume ndiye mara nyingi hulianzisha, ingawa hii haina maana kwamba mwanamke kama anataka sex kwa mumewe asubiri mume aanze.

Wanaume hupenda kutafakari kuhusu sex all the time.

Mengineyo!
Data zinaonesha kwamba wanawake wengi huvutiwa na wanaume ambao wamewazidi umri zaidi ya miaka miwili na kuendelea iia wanaume ambao ni warefu kidogo kuliko wanamke wenyewe ingawa wanawake wakiulizwa huwa wanaruka kimanga.

Pia wanawake wengi huvutiwa na mwanaume kwa sababu ya ukubwa wa wallet yake na reputation au status aliyonayo katika jamii na si sura, size, rangi au kitu chochote kwenye mwili wake.
 
Ihamishwe haraka, kabla ya hali ya hewa kuchafuliwa hapa kwenye siasa.
 
Jasusi,

Kichwa kimejieleza vizuri, ilikuwaje ukawahi kusoma hii thread? Au ndio ule UMBEYA wa kwetu?

Naaamini aliisoma (kama ambavyo mimi nimefaynay) ili apate kufikisha hoja aliyotoa maana haiwezekani kupendekeza kitu hicho bila kuwa kwenye thread husika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom