Ndevu zitaniharibia uhusiano wangu.

dada white

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
1,228
514
Nataman nikamuambie hivi "Mpenzi wangu nakupenda ila tatizo linakuja pale unapotaka kunibusu yaani ndevu zako kali kama pin huwa unanichoma pindi unaponibusu maeneo fulan ya mwili wangu" Kweli kwenye mapenzi wadada tunavumilia mengi.
 
Mapenzi yana rangi nyingi aisee..
Juzi kaja mtu hapa anasema yeye bila ndevu hajisikii raha..
Wewe leo tena ndevu ni kero...lol
Sasa sijui tufanyaje sie wajukuu wa Osama!!
 
kuna jamaa alikuwa na rasta toka akiwa na 18 mpaka 30 alipata dada mmoja matata sana, dada akamwambia anaogopa akikumbatiwa na rasta eti zitamnyonga, jamaa kesho yake kaja kijiweni kanyoa rasta zoooote, hahhhaha mapenzi noooma mnooooo!!!
 
The Boss tutakuja kurushiana ngumi humu aisee..
Mtu kusoma hajui hata picha jamani..ha!

wala msimkamie dada wa watu mwayego! ye kajionea the boss nae mbeijing kaona bora amuulize ye anakunwaje!ahahahhahahha uwwwiii mbavu zangu,the boss mi sijasema lakini:bolt:
 
pacha si ungenyoa tu!kwa hiyo ukawa mduchuuu!hata busu lenyewe likaishia hapo hapo!

Kunyoa inakuwa ngumu pacha..
Unajua ndevu kwetu wengine ni 'identity' aisee..
Tutazishape kila aina ya stahili lakini sio kuzitoa...
 
Kunyoa inakuwa ngumu pacha..
Unajua ndevu kwetu wengine ni 'identity' aisee..
Tutazishape kila aina ya stahili lakini sio kuzitoa...

hilo la identity nalo neno bwana!ila zisizidi sana kiukweli zinakera zikiwa nyingi mno
 
Back
Top Bottom