Ndesamburo kupeleka wagonjwa loliondo kwa kitambulisho cha mpiga kura ni sawa??

yeye anataka kuswaidia wa jimbo lake iwe shabiki wa CDM au CCM
Hajasema kadi za chama zinatumika kama kitambulisho.
Hili ni funzo kwa watu wasiopenda kujiandikisha kupiga kura
 
Nia ya hichi kitambilisho ni kujua usahihi Wa kitongoji unachokaa. Kama huna peleka barua ya mtendaji. Yeye alijitolea kwa watu Wa jumbo lake ambao hawana uwezo kifedha.
 
yeye anataka kuswaidia wa jimbo lake iwe shabiki wa cdm au ccm
hajasema kadi za chama zinatumika kama kitambulisho.
Hili ni funzo kwa watu wasiopenda kujiandikisha kupiga kura

kitambulisho cha mpiga kura si cha chama..tuko pamoja soma vizuri
 
kitambulisho cha mpiga kura si cha chama..tuko pamoja soma vizuri
wewe unajichanganya nashauri uridie kuisoma post yangu kwa utulivu.
Nimemaanisha kitambulisho cha kura anakiitaji ndesa ili ajiridhishe mpewa ofa ni mkazi wa jimbo lake.
 
vp mzee na ww ulitaka kupelekwa nn?kwa akili ya kawaida km huna kitambulisho njia pekee ya kukutambuluisha kwamba ww ni mkazi wa jimbo lake ni kwenda na barua ya serikali ya mtaa,hamna ubaguzi wa chama hapo ndio maana akasema kitambulisho cha kupiga kura ambacho kinatumika kwa sasa sehem nyingi km kitambulisho cha makazi na uraia kwa ujumla
Fikiria mara nyingi bingwa kabla ya kupost thread zako,usikurupuke tu !!!!!
 
Namuunga Mkono Ndesamburo katika utaratibu wake wa kuwatambua anaowapa Msaada wa usafiri. Tuelewe unapochukua abiria kwenye chombo chako usalama wao ni wajibu wako. Hili limekaa vizuri hasa ukizingatia kwamba wananchi wengi wa tanzania kitambulisho pekee walichonacho ni hiyo kadi ya mpiga kura...
 
Je na mabenki yanapohudumia wateja kwa kutumia kitambulisho cha kupigia kura ni sawa? kama sawa soma yafuatayo:

ndesa ni mbunge wa jimbo la moshi mjini anatoa msaada kaw watu wake wa jimbo ili kukwepa uchakachuaji unaonyasha kitambulisho cha kura maana utajulikanan kama wewe ni mmoja wao. tukumbuke kuwa kumsafirisha mtu mpaka loliondon i gharama so hawezi kusaidia kila mtu aende kule.
 
Safi sana mzee Ndesamburo nakuunga mkono kwa msaada ulioutoa kama mbunge kwa wananchi wa jimbo lako,wabunge wengine waige mfano wa mzee Ndesamburo kwa jinsi alivyoamua kuwasaidia wananchi wa jimbo lake.
 
Ushauri mzuri lakini kama msaada umelenga wananchi wa jimbo lake yupo sawa kabisa Mzee Ndesapesa kwani ktk vitambulisho cha mpiga kura ndicho kitambulisho halisi ambacho kinakutambulisha ila kama nawe ulitaka kupelekwa kumbe ni Mamluki pole sana.Misaada mingi hutolewa na masharti ata nchi hupata misaada kwa masharti sembuse hili la Mzee fuata masharti ukwee Helcopter
 
...mwanzisha thread donge la nini!! Patriot at work!! Sio m'bunge wetu wa Tanga mjini (Nundu) anayetoa mikopo (isiyo na tija) kwa akina mama wa CCM tu!!! Aibuuuuuuu yenu!!!
 
polesana m nshakunywa maji yangu .sikunyingi karibu kiteto
 
Ndesa
hapo fikiria mara mbili mzee wa ngu kumbuka sio waote walaiofanikiwa kupata hivi vitamublisho vya kihuni.....waligawa wanavyojua wao kwa muda wao iweje mtu anatoka moshi unambagua ugonjwa wake kwa kitambulisho cha kura..yawezekana alimpigia wa ccm....nakutakia mema na baraka ktk msada wako

Ni sawa kabisa kwa kuwa ni sehem ya kutoa elimu ya uraia ili watu wafahamua umuhimu wa kujiandikisha kuw mpiga kura.
 
polesana m nshakunywa maji yangu .sikunyingi karibu kiteto

mkuu naona umeshambuliwa kama mwizi,pole ila bora umewaeleza jf kuwa we si mamluki bali ulitaka kujua kama ni halali. Ila wengi wamekujibu,nami naongeza kuwa ktk taifa kama Tz,ID ambayo wanayo wengi ni kadi ya mpiga kura,ukija passpot utakuwa wachache,kadi ya chama,utawaacha wengi pia atabagua,kadi ya benki utawapata wangapi?n.k. Kwa ili mzee Ndesapesa ametumia busara!hongera Mbunge,natamani ungekua mbunge wa huku kwetu Muleba ya Kaskazini!
 
Kampeni za uchaguzi wa 2015 zimeshaanza mapema safari hii kwa kutumia mgongo wa Wagonjwa? Ndesamburo kama anahuruma na wagonjwa mbona anawabeba na Helkopta yake kwa nauli ya Sh.Milioni 2 toka Arusha? pesa anazopata kupitia Helkopta yake ni mara elfu ya gharama za kuwabeba wakazi wa Moshi kwa njia ya barabara!!

Huu ni Ufisadi!!!!
 
Mleta hoja anahoji kutumia kitambulisho cha mpiga kura kwa kuwa kati ya Watanzania 40 million waliojiandikisha kama wapiga kura ni 12 million sawa na 30%. Kwa takwimu hizi Mh Ndesamburo anapotumia kitambulisho cha mpiga kura kuandikisha wanaohitaji tiba kuna 70% ya wakazi wa Moshi Mjini ambao hawajajiandikisha kwenye daftari la mpiga kura watakosa hii fursa ya kwenda kupata tiba hii.
 
Kwani hapo kosa linakuwa la nani? Mh Ndesamburo aliyejitolea au mwananchi ambaye kwa sababu zake binafsi ameamua kutojiandikisha?
 
vp mzee na ww ulitaka kupelekwa nn?kwa akili ya kawaida km huna kitambulisho njia pekee ya kukutambuluisha kwamba ww ni mkazi wa jimbo lake ni kwenda na barua ya serikali ya mtaa,hamna ubaguzi wa chama hapo ndio maana akasema kitambulisho cha kupiga kura ambacho kinatumika kwa sasa sehem nyingi km kitambulisho cha makazi na uraia kwa ujumla
Fikiria mara nyingi bingwa kabla ya kupost thread zako,usikurupuke tu !!!!!

hapo kwako ni sawa.
Je kwa wale ambao hawajafikisha umri wa kisheria kujiandikisha kupiga kura.
Kimsingi hawa sio wahitaji wa hiyo tiba?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom