Malafyale
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 13,813
- 11,126
[FONT=Arial, sans-serif]Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Moshi Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Justin Salakana, amefuta kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa sasa, Philemon Ndesamburo (Chadema) katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Wakili wa Salakana, Elizabeth Minde, alimweleza Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Stella Mugasha, kuwa mteja wake ameamua kuacha kuendelea na kesi hiyo na kuiomba mahakama hiyo kuifutilia mbali kesi hiyo namba mbili ya mwaka 2010.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Wakili wa Serikali, Stella Kachenje, hakupinga maombi hayo na kuiomba mahakama hiyo imuamuru Salakana awalipe fidia ya gharama za usumbufu kwa maelezo kuwa wamekuwa wakitumia gharama na muda kufika mahakamani hapo na mlalamikaji kuamua kuiondoa kesi hiyo mahakamani.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Hata hivyo, Jaji Mugasha aliamuru kila upande kubebe gharama zake ulizotumia katika kesi hiyo na kuamua kuifuta kesi hiyo.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Katika madai yake ya msingi, Salakana anadai jywa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana haukuwa huru na haki kwa kuwa ulitawaliwa na kasoro kadhaa za kukiukwa kwa sheria za uchaguzi huku vitendo vya rushwa, kashfa na vitisho vikitawala katika zoezi hilo lililompa ushindi Ndesamburo.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Salakana alidai kuwa Ndesamburo alimkashifu kwa kuueleza uma kwamba hana nyumba mjini Moshi na mtu atakayeonyesha nyumba yake atamzawadia Sh. milioni mbili huku viongozi wa Chadema wakiwamo Madiwani wa sasa Jomba Koyi wa Kata ya Njoro na Steven Ngasa Kata ya Kiusa walitoa maneno ya vitisho wakati wa kampeni kwamba Chadema isiposhinda damu itamwagika ama watu kuchinjwa.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Kufutia madai hayo, Salakana aliiomba mahakama hiyo kutamka kufuta matokeo ya uchaguzi huo kwa madai kuwa haukuwa halali na kutaka Ndesamburo azuiwe kugombea tena kiti cha ubunge.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Hivi karibuni, Salakana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mjini, hapa alisema uwezekano wa kuendelea na kesi hiyo ni mdogo kutokana na kukabiliwa na ukata wa fedha za kuendesha kesi hiyo.[/FONT]
[FONT=Arial, sans-serif]Nilifungua kesi namba mbili ya mwaka 2010, gharama za kuwalipa mawakili na ikizingatia kwamba patahitajika fedha zaidi hapo mbeleni kesi itakapoanza, kwa maana ya gharama za mashahidi na za mawakili hivyo uwezekano wa kuendelea na kesi ni mdogo,alikaririwa Salakana akisema.[/FONT]
CHANZO: NIPASHE