Buyaka
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 1,643
- 1,786
Ni pale aliposema bungeni kwamba, viongozi wakitaka kujua hali halisi ya maisha ya Watanzania basi wapite na helikopta wataona kwa karibu, kwa mfano kuna watu mpaka leo hii wanaishi maporini, hawajulikani ni kina nani, na ukipita na gari au ndege huwezi kuwaona, na si vizuri kuwaacha nyuma wengine kimaendeleo, ni lazima tuendelee kwa pamoja.
Ulikuwa ni kama mpira wa kona alivyoshukiwa na mbunge wa CCM na washangiliaji, au niseme gombania goli , kipa mmoja washambuliaji kibaaao!
Wabunge wa CCM wakamuuliza Mheshimiwa Ndesamburo, nyinyi CHADEMA si mnafagilia kupunguza gharama za serikali kwa viongozi kutumia vyombo vya usafiri vya nafuu, sasa gari na helikopta kipi aghali? CCM wakadai kwamba kwa kweli hakuna chama mbadala kama wabunge wenyewe wa CHADEMA ndio wana mawazo hayo.
Lakini hata hivyo kuna hoja za maana alizotoa, kama alivyomlipua Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi kwamba ni failure lakini amongezewa muda baada ya umri wa kustaafu kufika, kinyume na sheria. Alimtaka aondolewe haraka wa sababu ni mzee na hana utaalam maalum unaohalalisha kumuongezea muda kama sheria inavyotaka.