Ndege zinamsaidia nini bibi yangu kule kijijini?

KILA NCHI NI VIZURI KUWEPO NA SEKTA YA USAFIRI KUPITIA ANGA...KIKUBWA NI KUWEPO UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA UHAKIKA WA SHIRIKA HIYO PAMOJA NZEGE ZAKE....

OVA
Aisee kumbe huwa kuna wakati unakuwa na point nzuri!
 
Hakuna lami na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,

Je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.

Wataalamu msaada wenu.

Siyo ndege tu jiulize sana je UDOM itamsaidia nini, Nyerere bridge, standard railway Dar - mwanza, jiulize hata barabara ya lami Dar mtwara itamsaidiaje wakati let's say yupo kibondo huko. Watu wengine kazi yao kuwaharibia wenzio siku khaaaa
 
Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa multiplier effect, kwanini iwe ndege na sio bandari, hoteli za kitalii, treni, kampuni ya TTCL nk. kwa mfano serikali imechukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Bhatti ambao ni wamiliki wa Airtel waliokuwa wakiwa sehemu ya umiliki wa TTCL je ununuzi wa hizo hisa uliogharimu zaidi ya billioni 15 unakusaidiaje,
Kwa kesi ya ATCL pamoja na ukweli kuwa si watanzaniawengi wenye uwezo wa kupanda ndege hii haiondoi ukweli kuna faida kama wananchi tutaipata kwa mfano faida ya moja kwa moja miezi 2 kabla ya hizi ndege kuja shirika la ATCL lilitangaza nafasi za ajira takribani 18. japo sio wewe au bibi yako tayari kuna watanzania takribani 18 ambao watanufaika moja kwa moja, hawa watu watapata vipato ambavyo vitaendesha maisha yao yao ya kila siku na jamaa zao, fedha zao zotakuwa chanzo kwa wengine kupata riziki hiyo moja.

Kwa kuwa shirika ni la serikali, tunatarajia kupata kodi ambayo hulipwa na kila abiria anayesafiri, na kila ndege inapotua katika uwanja wa ndege kuna ada inalipia, kupitia hiyo serikali itapata fedha ambazo zitatumika kuagiza dawana bidhaa muhimu kama mafuta ambayo yanaleta bidhaa kwako na bibi yako. hiyo mbili

ya tatu kupitia sekta ya anga kuimarika kutapelekea sekta nyengine kama ya utalii kukuwa na hivyo kuongeza mapato ya kuja kujenga hiyo barabara, badala ya watalii kushukia nchini kenya na kupanda usafiri mwengine sasa watakuwa wanakuja moja kwa moja jambo litakalowapunguzia usumbufu na kuwavutia kuja kwa wingi, lakini pia sekta ya biashara za kimataifa itaimarika kwa kuwa na usafiri wa uhakika ambao wafanyabiashara wengi huzingatia katika kuhakikisha wanafanya biashara kwa wakati ili kuokoa gharama zinazoweza kuongezeka kwa kuwa na mfumo mbovu wa usafiri wa anga. hili litatupelekea kuongeza akiba ya kutosha ya fedha za kigeni ambazo zitasaidia katika manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi na kuimarisha shilingi yetu
Mkuu utapoteza muda bure kumwaga nondo zenye mashiko kama hizi. Tatizo kuubwa humu JF haswa siku za hivi KARIBUNI kumejitokeza tabia za kitoto ambapo badala ya kuukubali ukweli watu hubeza tu pasi na hoja zenye mantiki. Wako weengi sana na wanashambulia kama manyigu lakini ukiingia mitaani utagundua ni kwa kiasi gani wananchi hasa wanaojituma na kufanya kazi kwa bidii wanaukubali uongozi wa MAGU na yote yanayofanywa na serikali yake.
 
wewe hujui faida ya ndege katika nchi hii unaishi karne gani nina wasiwasi na elimu yako , acha mhe, rais wetu afanye kazi , watanzania tunamkubali sana
 
Hakuna lami na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,

Je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.

Wataalamu msaada wenu.
Magari ya mwendokasi Dar yanamsaidiaje huyo bibi yako huko kijijini? Mbona yakawepo na sasa tunafurahia huduma hiyo? Jihoji kabla hujapost ujinga JF
 
Ndege zilikuwepo ktk shirika ambalo liliendeshwa kwa HASARA kubwa hadi kutengeneza MADENI kila kona ..... sababu kuu ikiwa ni UONGOZI MBOVU, UBADHILIFU kukosekana kwa UBUNIFU pasi na kusahau kutokuwepo kwa UZALENDO miongoni mwa viongoz na watendaji wa shirika .....

Kwa vigezo hivyo hapo juu don't expect any positive social - economic changes ....

Lakini kama uliwasikia vyema Mh. Rais JPJM, Speaker Job Ndugai, Waziri Makame Mbarawa na wengineo ktk sherehe ya UZINDUZI wa ndege 2 mpya za serikali ..... MABADILIKO CHANYA kwa ATCL yanatarajiwa kuanzia sasa .... by so doing serikali itapata MAPATO YA KUTOSHA hivyo kuwezesha upatikanaji wa huduma za kijamii zitakazokufaidisha wewe na hata huyo bibi yako huko kijijini
Thanks kwa msasa mkuu.ila wafunze na wenzako basi wajue kujenga hoja na si matusi
 
Tunataka mambo mengi ikiwa ni pamoja na kukuza sekta ya utalii...ndege zitawaleta watalii moja kwa moja. zitarahisisha usafiri sio lazima wewe upande...tutasafirisha mizigo na wenye uwezo... zitapanua wigo na kukuza uchumi. wewe utafaidika uchumi ukiwa mzuri bibi yako atapata dawa na huduma nyingine na atapunguziwa makali ya maisha kwa hali moja au nyingine. Uligwa bebesh!!?
Asante sana mkuu,hakika we ni Gt.nimekuelewa,umenielewesha bila matusi
 
Yaaani bora mmejibu wanajamvi, watz wengine akili sijui zikoje kama wew mtoa mada umeshindwa kumsaidia bibi yako huko kijijin unafkria nani atamsaidia? Ndo nyienyie hata nyoka akikimbilia ndani mnatoka wote nje mnasubuli serikali ije iwasaidie kumtoa, sisi tnaangalia maendeleo ya nchi kiujumla cyo ya bibi yako kijijin, parafini we
Mkuu bibi yangu ujue emebeba mabibi wengi ndani yake.na ni vyema ungejikita kwenye mada
 
Humu jukwaan twatofautiana uelewa na mengineyo mengi .... yahitaji uvumilivu wa kiwango cha juu ili uweze ku-socialize
Yaani mtu badala ya kutoa hoja anaanza kuhoji elimu yangu.sasa najiuliza nani mwenye elimu ndogo hapo kati ya mimi na yeye
 
Huyu mleta mada hajafikiria yeye anamsaidiaje bibi yake wa kijijini anakimbilia ndege ambazo zimenunuliwa na serikali na hajafikiria fastjet wanamsaidiaje bibi yake. Kuna mambo mengi ambayo serikali inafanya mfano uhakiki wa vyeti feki ina maana bibi yake ana cheti halali?
kwanza huyo bibi yako kaisaidia nini nchi hii
 
Aise pole mkuu wa nchk kwa kuongoza nchi kubwa tena yenye watu wa uelewa mdogo kama hawa....
 
Kuna watu kila kitu wao ni kupinga tu tena bila logic. Mbona uulizi uwanja wa taifa unamsaidia nn bibi yako aliye ukerewe?
 
Uliza pia hostel zinazojengwa chuo kikuu cha Dar es salaam zinamsaidiaje bibi yako. go Magufuli maneno ya watu yasikurudishe nyuma na jitihada zako za kweli kweli...
Nyinyi ndiyo mnaomuangusha Rais, kweli umeshindwa kumjibu huyu mtanzania mwenzako kwa hoja?
 
Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa multiplier effect, kwanini iwe ndege na sio bandari, hoteli za kitalii, treni, kampuni ya TTCL nk. kwa mfano serikali imechukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Bhatti ambao ni wamiliki wa Airtel waliokuwa wakiwa sehemu ya umiliki wa TTCL je ununuzi wa hizo hisa uliogharimu zaidi ya billioni 15 unakusaidiaje,
Kwa kesi ya ATCL pamoja na ukweli kuwa si watanzaniawengi wenye uwezo wa kupanda ndege hii haiondoi ukweli kuna faida kama wananchi tutaipata kwa mfano faida ya moja kwa moja miezi 2 kabla ya hizi ndege kuja shirika la ATCL lilitangaza nafasi za ajira takribani 18. japo sio wewe au bibi yako tayari kuna watanzania takribani 18 ambao watanufaika moja kwa moja, hawa watu watapata vipato ambavyo vitaendesha maisha yao yao ya kila siku na jamaa zao, fedha zao zotakuwa chanzo kwa wengine kupata riziki hiyo moja.

Kwa kuwa shirika ni la serikali, tunatarajia kupata kodi ambayo hulipwa na kila abiria anayesafiri, na kila ndege inapotua katika uwanja wa ndege kuna ada inalipia, kupitia hiyo serikali itapata fedha ambazo zitatumika kuagiza dawana bidhaa muhimu kama mafuta ambayo yanaleta bidhaa kwako na bibi yako. hiyo mbili

ya tatu kupitia sekta ya anga kuimarika kutapelekea sekta nyengine kama ya utalii kukuwa na hivyo kuongeza mapato ya kuja kujenga hiyo barabara, badala ya watalii kushukia nchini kenya na kupanda usafiri mwengine sasa watakuwa wanakuja moja kwa moja jambo litakalowapunguzia usumbufu na kuwavutia kuja kwa wingi, lakini pia sekta ya biashara za kimataifa itaimarika kwa kuwa na usafiri wa uhakika ambao wafanyabiashara wengi huzingatia katika kuhakikisha wanafanya biashara kwa wakati ili kuokoa gharama zinazoweza kuongezeka kwa kuwa na mfumo mbovu wa usafiri wa anga. hili litatupelekea kuongeza akiba ya kutosha ya fedha za kigeni ambazo zitasaidia katika manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi na kuimarisha shilingi yetu
Very well and clear argument...
 
Back
Top Bottom