Ndege zinamsaidia nini bibi yangu kule kijijini?

Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa multiplier effect, kwanini iwe ndege na sio bandari, hoteli za kitalii, treni, kampuni ya TTCL nk. kwa mfano serikali imechukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Bhatti ambao ni wamiliki wa Airtel waliokuwa wakiwa sehemu ya umiliki wa TTCL je ununuzi wa hizo hisa uliogharimu zaidi ya billioni 15 unakusaidiaje,
Kwa kesi ya ATCL pamoja na ukweli kuwa si watanzaniawengi wenye uwezo wa kupanda ndege hii haiondoi ukweli kuna faida kama wananchi tutaipata kwa mfano faida ya moja kwa moja miezi 2 kabla ya hizi ndege kuja shirika la ATCL lilitangaza nafasi za ajira takribani 18. japo sio wewe au bibi yako tayari kuna watanzania takribani 18 ambao watanufaika moja kwa moja, hawa watu watapata vipato ambavyo vitaendesha maisha yao yao ya kila siku na jamaa zao, fedha zao zotakuwa chanzo kwa wengine kupata riziki hiyo moja.

Kwa kuwa shirika ni la serikali, tunatarajia kupata kodi ambayo hulipwa na kila abiria anayesafiri, na kila ndege inapotua katika uwanja wa ndege kuna ada inalipia, kupitia hiyo serikali itapata fedha ambazo zitatumika kuagiza dawana bidhaa muhimu kama mafuta ambayo yanaleta bidhaa kwako na bibi yako. hiyo mbili

ya tatu kupitia sekta ya anga kuimarika kutapelekea sekta nyengine kama ya utalii kukuwa na hivyo kuongeza mapato ya kuja kujenga hiyo barabara, badala ya watalii kushukia nchini kenya na kupanda usafiri mwengine sasa watakuwa wanakuja moja kwa moja jambo litakalowapunguzia usumbufu na kuwavutia kuja kwa wingi, lakini pia sekta ya biashara za kimataifa itaimarika kwa kuwa na usafiri wa uhakika ambao wafanyabiashara wengi huzingatia katika kuhakikisha wanafanya biashara kwa wakati ili kuokoa gharama zinazoweza kuongezeka kwa kuwa na mfumo mbovu wa usafiri wa anga. hili litatupelekea kuongeza akiba ya kutosha ya fedha za kigeni ambazo zitasaidia katika manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi na kuimarisha shilingi yetu
 
Nani kakwambia kipimo cha vipaumbele vya nchi ni mahitaji yako na bibi yako? Au kwa vile wewe na bibi yako hamna uwezo wa kupanda ndege basi usafiri wa ndege ufutwe?
 
Bibi yako anaenda hospitali akiumwa? ama akienda sokoni kuuza mazao yake anapita barabara zipi? ama wewe kusoma umejifunza je kuandika na kusoma, kama umejifunzia nyumbani bila kwenda shule kabisa utakuwa na hoja?
Hizo barabara na hospitali anazokwenda bibi zinajengwa kwa pesa itakayoingia kutokana na hizo ndege.

Manufaa usiangalie hizo ndege utanufaika eti kwa ajili ya kupanda, bali panua zaidi ubongo upate kupata mambo ubongo unayostaili kuyapata.
 
Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Duh! siamini kama kuna mtanzania bado anaweza kuzungumza hivyo, yaani hata shule kidogo hamna. hebu jiulize kwanza serikali inapata wapi fedha kwa ajili ya maendeleo? unadhani ni kodi tu? kalagabaho wewe!!
 
Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Kwani daraja la kigamboni linamsaidia nini huyo bibi yako?

Je gesi iliyogunduliwa mtwara inamsaidia nini bibi yako?

Kwani hizo ndege wenye uwezo wa kusafiri nazo hawalipi nauli? Hiyo nauli inamsaidia nini bibi yako?

Nadhani majibu kwa njia ya maswali yatakujengea uelewa.
 
Watu wanaosema kwanini ndege zinanunuliwa ilihali sio watu wengi wana uwozo wa kukata nauli. Mkae mkijuwa, kipato cha mTz wa leo, sio kipato cha mTz wa miaka mitano au kumi ijayo. Kwa jinsi tunavyo endelea kiuchumi, usafiri wa anga hapa nchini na bara lote la Africa utakuwa ni mwingi na warahisi sana. Ndio maana serikali inajipanga kukarabati viwanja vingi na kwa haraka. Usishangae miaka michache ijayo watu watukuwa wanajazana kwenye ndege kwenda kula krismasi kwao kuliko kwenye mabasi.
 
Wakati simu za mkononi zilipoanza watu wengi walifikiri hawatakuwa na uwezo wa kuzimiliki lakini Leo mambo ni tofauti inawezekana miaka michache ijayo usafiri wa anga litakuwa jambo rahisi na la kawaida na utakuwa unakwenda kumuona bibi yako na kumpelekea zawadi ya vitenge kwa kupanda ndege za Magufuli .
Pia kuna kodi itakayopatikana ,ajira,kama ATCL itajiendesha kwa faida serikali itapata gawio lake kama inavyopata kutoka NMB na mashirika mengine.
Kwahiyo kijana wa Chadema aka wapinga maendeleo bibi yako atafaidika tu usihofu.
 
Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Sio kitu kitakachofanywa na serikali kitamsaidia kila Mtanzania. Kuna mengine yatakupita kama ulivyokupita ustaarabu wa kupiga mswaki kila ukiamka na unapoenda kulala. Au kunawa mikono kila unapotoka maliwatoni. Subiri kuna wakati utafika utanufaika kwa urefu wa nyanyadu yako. Watanzania wenye uhitaji wa ndege ndio wakati wao huu wa kunufaika....tunaenda kwa awamu. Tulia dawa ikuingie.
 
Kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa multiplier effect, kwanini iwe ndege na sio bandari, hoteli za kitalii, treni, kampuni ya TTCL nk. kwa mfano serikali imechukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Bhatti ambao ni wamiliki wa Airtel waliokuwa wakiwa sehemu ya umiliki wa TTCL je ununuzi wa hizo hisa uliogharimu zaidi ya billioni 15 unakusaidiaje,
Kwa kesi ya ATCL pamoja na ukweli kuwa si watanzaniawengi wenye uwezo wa kupanda ndege hii haiondoi ukweli kuna faida kama wananchi tutaipata kwa mfano faida ya moja kwa moja miezi 2 kabla ya hizi ndege kuja shirika la ATCL lilitangaza nafasi za ajira takribani 18. japo sio wewe au bibi yako tayari kuna watanzania takribani 18 ambao watanufaika moja kwa moja, hawa watu watapata vipato ambavyo vitaendesha maisha yao yao ya kila siku na jamaa zao, fedha zao zotakuwa chanzo kwa wengine kupata riziki hiyo moja.

Kwa kuwa shirika ni la serikali, tunatarajia kupata kodi ambayo hulipwa na kila abiria anayesafiri, na kila ndege inapotua katika uwanja wa ndege kuna ada inalipia, kupitia hiyo serikali itapata fedha ambazo zitatumika kuagiza dawana bidhaa muhimu kama mafuta ambayo yanaleta bidhaa kwako na bibi yako. hiyo mbili

ya tatu kupitia sekta ya anga kuimarika kutapelekea sekta nyengine kama ya utalii kukuwa na hivyo kuongeza mapato ya kuja kujenga hiyo barabara, badala ya watalii kushukia nchini kenya na kupanda usafiri mwengine sasa watakuwa wanakuja moja kwa moja jambo litakalowapunguzia usumbufu na kuwavutia kuja kwa wingi, lakini pia sekta ya biashara za kimataifa itaimarika kwa kuwa na usafiri wa uhakika ambao wafanyabiashara wengi huzingatia katika kuhakikisha wanafanya biashara kwa wakati ili kuokoa gharama zinazoweza kuongezeka kwa kuwa na mfumo mbovu wa usafiri wa anga. hili litatupelekea kuongeza akiba ya kutosha ya fedha za kigeni ambazo zitasaidia katika manunuzi ya bidhaa na huduma nje ya nchi na kuimarisha shilingi yetu
Kwanza, nikushukuru kwa kumpa somo halisi huyu mleta mada ili nina wasiwasi kama atakuelewa.

Pili, Usishangae ukisikia huyu uliyemjibu ana elimu ya Chuo Kikuu!

Tanzania kuna vituko!
 
Umempa majibu mazuri mnoooo. Lakini nina wasiwasi kutokana na upeo wake atakuelewa.
 
Hakuna lami,.na hajawahi na wala hategemei kupanda ndege,je zitamsaidia nini yeye hizi??hata mimi binafsi sielewi zinanisaidia nini maana sina pesa ya kulipia kwenye ndege.wataalamu msaada wenu
Zitakusaidia wewe uende kwa haraka kumsalimia bibi yako kijijini.
 
Nani kakwambia kipimo cha vipaumbele vya nchi ni mahitaji yako na bibi yako? Au kwa vile wewe na bibi yako hamna uwezo wa kupanda ndege basi usafiri wa ndege ufutwe?

Yeye alichokuwa anasema vipaumbele vingefuatwa kwanza huduma za jamii kwanza baadaye hiyo midege yenu!!!
 
Back
Top Bottom