Dickson Ng'hily
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 451
- 485
Sina hakika kama Wapo Radio wamefika eneo la tukio...Mimi ninaongea sasa nipo huku na nimezungukia maeneo yote ambayo ndege hizo zilionekana kabla ya Tanzania kuwaomba kuacha. Nimeongea na Mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na mkuu wa brigedi ya kusini inayosimamia mikoa tisa, pia nimefanikiwa kupenya mpaka Malawi na kuzungumza na watu kule. Kiufupi hakuna ndege zinazoruka kwa sasa..Ni kweli kulikuwa na taharuki na kuna baadhi ya watanzania wamekimbilia Musumbiji na hasa vijana na baadhi kutafuta maeneo ya kununua na kujenga nje ya mkoa wa Ruvuma.Biashara zinaendelea kama kawaida na wavuvi bado wanavua na hasa baada ya kutoziona ndege hizo na kuhakikishiwa usalama wao na serikali ya Tanzania. Picha namba 1 ni Mkuu wa Mkoa Mh. Mwambungu akizungumza na wananchi wa Mbambabay nyuma yake anaonekana Mkuu wa Brigedi ya kusini, Kamanda John Chacha. Picha namba 2 ni Makamanda ambao ni wajumbe kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa..Alikuwepo OCD akimwakilisha RPC, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa, RCO, Mkuu wa Magereza Mkoa na kamanda John Chacha. Picha namba 3 ni mimi mwenyewe nikisaidiana na wavuvi kuvuta mtumbwi wao nchi kavu,. Picha namba 4 niko na Mashaka Mgeta (Mwandishi wa Habari-Nipashe + wavuvi tukitoa nyavu kwa mtumbwi). Picha namba 5 nikiwa ufukweni mwa Ziwa Nyasa na nyuma yangu ni wavuvi plus wafanyabiashara wa samaki...