Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,498
- 19,339
Likipelekwa Mahakama ya Kimataifa, ninaomba Tanzania iwakilishwe na mwanasheria mzuri, siyo hao wababishaji. Wasistize dondoo tano tu katika kesi hiyo;
Dondoo ya nne itatokana na sheria za kimataifa kuhusu maji yaliyoko mipakani baada ya kuonyesha kuwa maji hayo hayana mwenyewe. Wakumbushe tena kuwa yale makubalianao ya kugawana maji hayo kulikofanywa na wareno kule kusini hayajawahi kufanyika upande wa kaskazini kuihusisha Tanzania kwa vile sehemu zote mbili za ziwa zilikuwa zinatawaliwa na mwingereza.
Uingereza kuhamisha mpaka wa Nyasaland kuufanya ukutane na ule wa Tanganyika ilikuwa ni makosa ambayo hayawezi kufuatwa chini ya makubaliano ya OAU, kwa vile Tangayika ilikuwa chini ya League of Nations, na ilitakiwa uingereza iirafu League of Nations kuhusu nia yake ya kuinyima Tanganyika uhuru wa kutumia maji yale lakini hawakufanya hivyo.
Dondoo ya kwanza iwe ni kukumbusha kuwa mkataba wa Berlin wa 1885 kuhusu bonde la Kongo ulikuwa umeliacha Ziwa nyasa pamoja ni mito yote katika eneo hilo kuwa ni maeneo huru yatakayotumiwa na nchi zote.
Dondoo ya pili iwe ni kukubali kuwa mkataba wa Heligo wa 1890 ulitaka himaya ya ujerumani iishie kwenye ziwa Nyassa; lakini wakumbushe tena kuwa wakati wa mkataba huo hakukuwa na himaya yoyote iliyopewa eneo la ziwa lile kwa vile Uingereza ilishapinga Ureno (ambayo ndiyo ilikuwa imechukua eneo lile wakati wa makubaliano ya Berlin) isikalie eneo hilo kutokana na waingereza wawili (Rhodes na Livingstone) kuwa walikuwa tayari kwenye eno hilo na wasingekuwa chini ya utawala wa wareno; mabadiliko hayo yalikuwa yameliacha eneo lote lile likiwa halina himaya.
Dondoo ya tatu ni kuwa, himaya ya British Central Africa ilipoundwa mwaka 1902, kwa kufuata makubaliano ya Berlin, ilitangaza kuwa eneo la BCA litakuwa ni magharibi na kusini mwa Ziwa Nyasa, na hivyo kuliacha ziwa hilo halina mwenyewe tena.