Ndege za Malawi zafungasha virago Ziwa Nyasa

Hili ni pigo kwa mabwana wa vita waliokuwa wanasisitiza kwamba tupigane vita. Mgogoro huu utamalizwa kwa diplomasia na tunashukuru Mungu Tanzania imejaaliwa kuwa na wanadiplomasia mahiri. Aliyekuwa anachochea vita sasa apiganishe ng'ombe wake zizini siyo kutaka kuua watu wasio na hatia.
 
hahaha, nikikukamataa! utantambua....chezea mutz veve

duh!!!! we ni noma. ilitakiwa wewe ndo uwe frontline, yule mwanamama wa Malawi, Joyce lazima angesalimu amri ndani ya siku mbili tu mwa'ngu, hakyanani we ni kidume, we ni noma!!!!!!!!!!!!!!!!! ha ha haaaaaa!!!!!!!!!!!!
 
duh!!!! we ni noma. ilitakiwa wewe ndo uwe frontline, yule mwanamama wa Malawi, Joyce lazima angesalimu amri ndani ya siku mbili tu mwa'ngu, hakyanani we ni kidume, we ni noma!!!!!!!!!!!!!!!!! ha ha haaaaaa!!!!!!!!!!!!

usimsifie sana hakawii kutangaza ndoa huyo.
 
Sasa kazi iliyobaki Jamaa yetu amtokee yule mama,ahakikishe anamtwanga mimba ili Wamalawi watuheshimu.
 
Hili ni pigo kwa mabwana wa vita waliokuwa wanasisitiza kwamba tupigane vita. Mgogoro huu utamalizwa kwa diplomasia na tunashukuru Mungu Tanzania imejaaliwa kuwa na wanadiplomasia mahiri. Aliyekuwa anachochea vita sasa apiganishe ng'ombe wake zizini siyo kutaka kuua watu wasio na hatia.

Bila mkwara wa vita wamalawi hawakuwa tayari kuondoka. wakupiganisha ng'ombe wa kwenye zizi lake ni j banda alie tuvamia kwenye nchi yetu.bado ninaamini kuwa kilicho mfanya j banda akafyata mkia ni mkwara wa kivita na sikingine.mazungumzo ya kidiplomasia yatafanyika mzuzu 20/8/12 siku ambayo bado haijafika.na km ataendelea tuko tayari kuitafuta amani kwa upanga kwa sababu nayo ni amani.kwani kuna amani yakutafutwa kwa mazungumzo na ya kutafutwa kwa upanga.zote ni amani.imebaki juu ya j banda kuchaguwa akitaka amani kwa mazungumzo tutazama nae akitaka kwa upanga tutaibuka nae pia.sisi ni twanga kote kote.
 
pamoja kwamba wamalawi wamefyata mkia baada ya tishio la kivita,mgogoro huu wa mpaka kati yetu na wao si wakupuuzwa ata kidogo,either litafutwe suluhisho la kudumu kabisa kwasababu si mara ya kwanza kuibuka kwa mgogoro huu or kujiweka tayari kwa wakati wowote cuz wamalawi wanaonekana km wameamua kubuy more time halafu waje upya wakati huo labda tumejisahau.mimi naamini kabisa mgogoro huu utaisha kwa njia ya kidiplomasia na vita si suluhisho la kudumu,tuinvest zaidi ktk diplomacy.
 
Sisi kwa kuridhika na HEADING ni noma...yaani leo watu wanavochangia kama sio wale ambao wiki sasa mlikuwa wakali kama nyuki...
 
tuzipige tu ili heshima iwepo....si ajabu wanatulia mingo taimingi hapo.....ukiona kobe kainama ujue anatunga sheria....hawa hawana akili dawa yao ni kuwaonyesha kuwa dharau na kiburi si maungwana.

wewe si unataka vita basi uende vitani na wa kufa uwe wewe tuone kama kweli kuna mtu anapenda kufa
 
sijui ni kweli au uongo.Maana hata Ebola vyombo vya habari baadhi vilisema haijafika TZ wakati wakazi wa karagwe wanasema vingine..

watu wanachakachua habari tatizo. Ngoja tuamini tu hali ni shwari ziwani.
 
MALAWI imesema imeondoa ndege zake zilizokuwa zikifanya utafiti wa mafuta katika Ziwa Nyasa kwa kuwa haitaki kuingia vitani, badala yake imeamua kupeleka mgogoro huo Mahakama ya Kimataifa.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Mambo ya Ndani na Uhusiano wa Kimataifa kwa Mambo ya Kiusalama wa Malawi, Uladi Mussa alipokuwa akizungumza na gazeti linalochapishwa nchini humo la Nyasa Times.

"Nawahakikishia wananchi mtaendelea kuishi kwa utulivu. Tupo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania, bila shaka mambo yataenda vizuri. Kama hali ikishindikana tutalipeleka suala hili kwenye Mahakama ya Haki ya Kimataifa," alisema Mussa.

Kauli ya Waziri huyo imekuja wakati baadhi ya wananchi wa Malawi wanaoishi katika Vijiji vya Karonga na Chitipa vilivyopo kando ya Ziwa Nyasa upande wa Malawi wakiwa wameanza kuvihama vijiji hivyo kuhofia usalama wa maisha yao. Baadhi ya wakazi hao wamekaririwa na Nyasa Times wakisema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo kunusuru maisha kutokana na kuwapo kwa dalili za kutokea vita kati ya Malawi na Tanzania.

Waziri Mussa amesema suala hilo la mgogoro wa mpaka litaamuliwa kwa njia ya amani na hivyo kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao bila wasiwasi. Waziri huyo aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali ya Malawi ina ushahidi wa kutosha kuwa ziwa lote la Malawi (Nyasa)ni mali ya Malawi na Tanzania haina nguvu ya kuwasimamisha kuendelea na kazi ya kutafuta mafuta.

"Kimsingi hapa hakuna hoja ya kubishania. Wote tunajua ziwa hili ni mali yetu (Malawi)," alisema.
"Kama malalamiko haya yangekuwa yametolewa na Msumbiji, hapa tungekuwa na hoja ya kubishania, lakini si Tanzania." alisisitiza.

Alisema ushahidi wao wa mipaka ni wa tangu mwaka 1890 wakati ambako wakoloni wa Uingereza na Ujerumani walitiliana saini juu ya suala hilo. Aliendelea kueleza kuwa umiliki huo wa ziwa umeongezewa nguvu na maazimio ya mwaka 1963 ya Wakuu wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) kwamba wanachama wanapaswa kuheshimu mipaka waliyorithi kwa wakoloni.

Kauli za wananchi

Wakati Serikali ya Malawi ikitoa msimamo huo watu kadhaa waliohojiwa wameonyesha hofu ya nchi hizo kuingia katika vita.Heckley Christopher ambaye ni raia wa Malawi anayefanya biashara eneo la Mbambabay mkoani Ruvuma anasema:

" Malawi ni nchi ndogo sana kupigana na Tanzania, ni nchi yenye mikoa minne tu, kukiwa na vita itaangamia mara moja."

Raia mwingine wa Malawi ni Vilion Gordon ambaye alisema Tanzania na Malawi ni marafiki wa siku nyingi, hivyo hawana sababu za kugombania ziwa ambalo lilikuwapo tangu enzi hizo. "Nashauri wakae chini wapatane, kwa nini tugombane sasa wakati ziwa hilo lilikuwapo tangu enzi hizo?"alisema.

Mtanzania mkazi wa Kijiji Lundo kilichoko Mbambabay mkoani Ruvuma, Zakhia Chengula ameitaka Serikali ya Tanzania kuendelea kuimarisha ulinzi na kukubali kuingia katika mazungumzo na Malawi badala ya kufikiri vita.
"Hapa sisi ni kwetu, vita ikiingia sisi tutakufa tu hakuna pa kukimbilia. Tunaiomba Serikali iimarishe ulinzi eneo hilo na ikae na Malawi kuzungumzia mgogoro huo," alisema.

Mkuu wa Wilaya mpya ya Nyasa, Ernest Kahindi alisema hakuna hofu yoyote kwa wakazi wanaoishi kando ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania. Amewataka wananchi hao kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali kama kawaida kwani suala hilo sasa linashughukiliwa kitaifa.

"Mwanzoni kulikuwa na hofu kubwa, lakini baada ya Serikali ya Tanzania kutoa tamko la kutaka ndege za Malawi ziondoke na zenyewe kutii amri hiyo, hakuna tatizo lolote," alisema na kuendelea; "Shughuli katika eneo hili zinaendelea kama kawaida. hakuna mwananchi aliyepigwa risasi wala ndege iliyotunguliwa, mambo yako shwari."

Jeshi laimarisha ulinzi

Katika hatua nyingine Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limeimarisha ulinzi katika mwambao wa Ziwa Nyasa na kupiga marufuku wananchi kukatisha eneo lao la jeshi. Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Kyela waliozungumza na gazeti hili jana walisema kuibuka kwa mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi, kumesababisha kuongezeka kwa ulinzi katika eneo hilo.

"Mara ya kwanza tulikuwa tunaingia tu pale kambini kama tumeagizwa vitu kama mayai, vocha na vitu vingine na wanajeshi wa pale tunawapelekea, lakini sasa tangu kuibuka kwa mgogoro huo wa mpaka wa Ziwa Nyasa na hawa wa Malawi tumezuiliwa kabisa kuingia hapa" alisema mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina Hamis.

Chanzo cha hofu

Jumatatu wiki hii, akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe aliitaka Malawi kuziondoa ndege na kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta katika eneo hilo kwa kuwa ni mali ya Tanzania.

"Serikali ya Tanzania inapenda kuyaonya na kuyataka makampuni yote yanayoendelea na shughuli za utafiti eneo hilo zisitishe mara moja kuanzia leo (Jumatatu)," alisisitiza Membe.

Mbali na Waziri Membe viongozi wengine waliozungumzia mgogoro huo na kuitaka Malawi iache uchokozi ni Samuel Sitta na Mwenyeti wa Kamati ya Bunge ya masuala ya ulinzi, Edward Lowassa. Wakati Sitta akiwataka Watanzania kuendelea nashughuli zao bila hofu kwa kuwa Serikali iko tayari kwa tishio lolote, Lowassa alisisitiza kuwaTanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.



 
Angalia isiwe mtego wakati wakijiandaa na vita nyie mkidhani mambo yamekwisha. Maana nasikia kuna mibomu inalipuka Kibamba.
 
Umilikiwa wa nusu ya ziwa kwa Tanzania hautegemei maamuzi ya mahakama yoyote duniani. Wamalawi wakiamua kwenda mahakani waende lakini msimamo wa Tanzania ni mgao pasu kwa pasu.
 
Back
Top Bottom