Ndege ya Rais yazuiliwa

=TAMUCHUNGU;3201487]hakuna shirika la ndege hapa duniani linaloitwa QATAL,wala hakuna waziri anayeitwa NDUNDU.
Halafu hii habari ni ya kiumbea kwa sababu hili gazeti halijui hiyo ndege iko nchi gani zaidi ya kuzusha nje ya nchi.gazeti makini haliwezi kuandika udaku kama lilivofanya hili.wajinga ndio waliwao.

NIKISOMA MSG YAKO JUU NA KUSOMA TAARIFA YA HAPO CHINI NAONA KAMA WEWE NDIE MJINGA ZAIDI NA MMBEYA ZAIDI TENA SIKU NYINGINE WAKIKUTUMA CHOMOA JF NOMA ITAKULA KWAKO MPWA

Halafu hii habari ni ya kiumbea kwa sababu hili gazeti halijui hiyo ndege iko nchi gani zaidi ya kuzusha nje ya nchi

halafu wewe wewe unasapoti kwa KING

quote_icon.png
By Kang
Waandishi wetu wa habari noma, kwanza sio
Davous ni Davos na muhimu zaidi haipo Sweden ipo Switzerland. Yaani mambo ya kugoogle kwa dakika mbili yanawashinda.

kama ulikuwepo mkuu,hawa jamaa wababaishaji kweli,hata shirika la ndege eti wanaandika QATAL,Waziri NDUNDU mara nje ya nchi,afazali nawe umeliona hilo...Ndo matatizo ya copy and paste kaka

tamuchungu
kama ulikuwepo mkuu,hawa jamaa wababaishaji kweli,hata shirika la ndege eti wanaandika QATAL,Waziri NDUNDU mara nje ya nchi,afazali nawe umeliona hilo...Ndo matatizo ya copy and paste kaka.

teeeheeeteeehhhhh

EMBU NINUKUU
 
kama udaku hito switzerland inafanya nini jamani??anyway napita tu leo naeekea chamazi kujianda na mechi
 
Habari zinaweza zikawa na ukweli ndani yake ila typing error zimekuwa nyingi mapaka story yenyewe inataka kupoteza uhalisia wake kuelekea kwenye udaku.
 
kama ulikuwepo mkuu,hawa jamaa wababaishaji kweli,hata shirika la ndege eti wanaandika QATAL,Waziri NDUNDU mara nje ya nchi,afazali nawe umeliona hilo...Ndo matatizo ya copy and paste kaka.
Nyani haoni kundule, maana ya neno "AFAZALI" ni nini?!
 
Waandishi wetu wa habari noma, kwanza sio
Davous ni Davos na muhimu zaidi haipo Sweden ipo Switzerland. Yaani mambo ya kugoogle kwa dakika mbili yanawashinda.

Inspite of those minor flaws, the core of the subject remains crystal clear. The story was intended to expose lavish spending done by the mindless government on covering for seemingly needless costs while thousands of patients' lives are at stake owing to ongoing medics strike. Spending Tshs 3M taxpayers money on payment for unnecessary 'tour' to Switzerland must be condemned and faultfounded by any conscious citizen.
 
kama ulikuwepo mkuu,hawa jamaa wababaishaji kweli,hata shirika la ndege eti wanaandika QATAL,Waziri NDUNDU mara nje ya nchi,afazali nawe umeliona hilo...Ndo matatizo ya copy and paste kaka.
Ni kweli kuna makosa ya kiuandishi kwenye bandiko hili. Lakini kitu cha kujiuliza hiyo ndege ipo? Kama haipo iko nje kwa muda gani? Na wewe unayetafuta hitilafu za kiuandishi ili ung'ang'anie hapo kuficha uchi wa serikali yako, hujui kama unatakiwa kuanza kwa herufi kubwa unapoandika sentensi yako? Hujui kila unapoweka koma unatakiwa kuacha nafasi? Na neno AFAZALI umelitoa wapi na ni lugha gani?! Matatizo ya kuwapiga watu mawe huku ukijificha kwenye nyumba ya vioo!!!
 
"Jana Rais Kikwete ameondoka, yeye na msafara wake watatumia zaidi ya sh milioni 300 kwa siku nne tu, atakazohudhuria mkutano wa uchumi, Davos nchini Sweeden. Angekuwa na ndege yake, gharama zingepungua,"

Hv Davos ni Sweden au Uswisi?
 
• IKO NJE KWENYE MATENGENEZO, SERIKALI YAKWAMA KUILIPIA

na Mwandishi wetu

UKATA unaoikabili serikali, umesababisha kukwama kuilipia ndege maalumu ya Rais, inayofanyiwa matengenezo nje ya nchi, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Kutokuwepo kwa ndege hiyo, kumesababisha Rais Jakaya Kikwete na ujumbe wake wa zaidi ya watu 14, ulioondoka nchini jana kwenda Davous, nchini Sweden, kuhudhuria mkutano wa dunia wa mambo ya uchumi, kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Qatal. Habari ambazo gazeti hili imezipata, zilisema kuwa ndege ya Rais mahususi kwa ajili ya safari za aina hiyo imezuliwa nje ya nchi baada ya serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo yake.

Kutokuwepo kwa ndege hiyo iliyonunuliwa kwa sh bilioni 40 na kuibua mzozo mkubwa wakati serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kunaelezwa kuwa kumeongeza gharama kubwa kwa ziara za Rais Kikwete ambaye amekuwa akitumia ndege za kawaida kwenye safari zake nje ya nchi. Habari kutoka ndani ya msafara wa Rais, zilisema kuwa zaidi ya sh milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya kugharimia ziara hiyo ya siku nne nchini Sweeden. Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatumika ndani ya siku nne kuanzia Januari 25 hadi 29 ambapo Rais na ujumbe wake watakuwa wanahudhuria mkutano huo ambao wataalamu wa uchumi, wameuelezea kwamba hauna tija kwa taifa. Inaelezwa kuwa Rais Kikwete ameshahudhuria mikutano hiyo mara nyingi, lakini hakuna faida inayopatikana kitaifa baada ya serikali kushiriki katika mikutano hiyo inayoratibiwa na Wizara ya Fedha na Uchumi. “Jana Rais Kikwete ameondoka, yeye na msafara wake watatumia zaidi ya sh milioni 300 kwa siku nne tu, atakazohudhuria mkutano wa uchumi, Davos nchini Sweeden. Angekuwa na ndege yake, gharama zingepungua,” kilisema chanzo chetu cha habari. Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa kwa takriban miezi miwili sasa, ndege hiyo iko nje ya nchi ikifanyiwa matengenezo kutokana na kuwa na hitilafu.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Ndege za Serikali, Keenan Mhaiki, alikiri kuwa ndege hiyo iko nje kwa matengenezo, lakini alisema ni matengenezo ya kawaida yaliyomo ndani ya ratiba ya ndege hiyo ya kisasa. “Ndege ya Rais iko kwenye matengenezo. Sio kwamba ni mbovu, hapana ni matengenezo ya kawaida ambayo yanachukua zaidi ya mwezi mmoja,” alisema Mhaiki. Alipoulizwa kwamba ndege hiyo iko nje kwa muda mrefu baada ya serikali kukwama kulipa deni la matengezo yake, Mhaiki alikana na kuongeza kuwa hana taarifa za serikali kushindwa kulipia deni la matengenezo. “Kwanza nikwambie tu kuwa ndege hiyo sio mbovu, lakini pia sisi hatuhusiki na malipo ya matengenezo yake, kwa kawaida ikishakuwa tayari tunapewa taarifa nasi tunaandaa utaratibu wa kuifuata,” alisema.

Alipoulizwa kuhusiana na serikali kukwama kuikomboa ndege ya Rais, Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu, alijibu kwa kifupi kwamba hawezi kuulizwa swali hili kwenye simu. Alipotakiwa kufuatwa ofisini ili kutoa ufafanuzi, Waziri Ndundu alikuja juu na kusema yuko jimboni, hivyo waulizwe wasaidizi wake walioko Dar es Salaam. “Mimi niko jimboni, pale ofisini kuna watendaji wa wizara. Mimi siyo wizara, nenda pale utapata majibu yote,” alisema Waziri Ndundu

Hivi hili gazeti halina EDITOR ama ndio yaleyale tunayopita kulalamikia aina ya watendaji waliojaa serikalini. Lakini zaidi hili ndio gazeti linalopigania uwajibikaji, serikali makini na ethics??? Mmiliki angeonyesha mfano wa uongozi makini kwa kumuwajibisha mhusika wa kosa hili.....
 
Ndege tuloambiwa tule nyasi kumbe ilikuwa used, haya ndio matatizo ya 10%
 
Hivi hili gazeti halina EDITOR ama ndio yaleyale tunayopita kulalamikia aina ya watendaji waliojaa serikalini. Lakini zaidi hili ndio gazeti linalopigania uwajibikaji, serikali makini na ethics??? Mmiliki angeonyesha mfano wa uongozi makini kwa kumuwajibisha mhusika wa kosa hili.....
Maeditor wanakimbizana na vijisent vya wanasiasa, hawana muda wa kupitia hivi vitabloid vyao, nachukia waandisha wa bongo kama ukoma, Pasco included.
 
• IKO NJE KWENYE MATENGENEZO, SERIKALI YAKWAMA KUILIPIA

na Mwandishi wetu

UKATA unaoikabili serikali, umesababisha kukwama kuilipia ndege maalumu ya Rais, inayofanyiwa matengenezo nje ya nchi, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Kutokuwepo kwa ndege hiyo, kumesababisha Rais Jakaya Kikwete na ujumbe wake wa zaidi ya watu 14, ulioondoka nchini jana kwenda Davous, nchini Sweden, kuhudhuria mkutano wa dunia wa mambo ya uchumi, kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Qatal. Habari ambazo gazeti hili imezipata, zilisema kuwa ndege ya Rais mahususi kwa ajili ya safari za aina hiyo imezuliwa nje ya nchi baada ya serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo yake.

Kutokuwepo kwa ndege hiyo iliyonunuliwa kwa sh bilioni 40 na kuibua mzozo mkubwa wakati serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kunaelezwa kuwa kumeongeza gharama kubwa kwa ziara za Rais Kikwete ambaye amekuwa akitumia ndege za kawaida kwenye safari zake nje ya nchi. Habari kutoka ndani ya msafara wa Rais, zilisema kuwa zaidi ya sh milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya kugharimia ziara hiyo ya siku nne nchini Sweeden. Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zilisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatumika ndani ya siku nne kuanzia Januari 25 hadi 29 ambapo Rais na ujumbe wake watakuwa wanahudhuria mkutano huo ambao wataalamu wa uchumi, wameuelezea kwamba hauna tija kwa taifa. Inaelezwa kuwa Rais Kikwete ameshahudhuria mikutano hiyo mara nyingi, lakini hakuna faida inayopatikana kitaifa baada ya serikali kushiriki katika mikutano hiyo inayoratibiwa na Wizara ya Fedha na Uchumi. “Jana Rais Kikwete ameondoka, yeye na msafara wake watatumia zaidi ya sh milioni 300 kwa siku nne tu, atakazohudhuria mkutano wa uchumi, Davos nchini Sweeden. Angekuwa na ndege yake, gharama zingepungua,” kilisema chanzo chetu cha habari. Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa kwa takriban miezi miwili sasa, ndege hiyo iko nje ya nchi ikifanyiwa matengenezo kutokana na kuwa na hitilafu.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Ndege za Serikali, Keenan Mhaiki, alikiri kuwa ndege hiyo iko nje kwa matengenezo, lakini alisema ni matengenezo ya kawaida yaliyomo ndani ya ratiba ya ndege hiyo ya kisasa. “Ndege ya Rais iko kwenye matengenezo. Sio kwamba ni mbovu, hapana ni matengenezo ya kawaida ambayo yanachukua zaidi ya mwezi mmoja,” alisema Mhaiki. Alipoulizwa kwamba ndege hiyo iko nje kwa muda mrefu baada ya serikali kukwama kulipa deni la matengezo yake, Mhaiki alikana na kuongeza kuwa hana taarifa za serikali kushindwa kulipia deni la matengenezo. “Kwanza nikwambie tu kuwa ndege hiyo sio mbovu, lakini pia sisi hatuhusiki na malipo ya matengenezo yake, kwa kawaida ikishakuwa tayari tunapewa taarifa nasi tunaandaa utaratibu wa kuifuata,” alisema.

Alipoulizwa kuhusiana na serikali kukwama kuikomboa ndege ya Rais, Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu, alijibu kwa kifupi kwamba hawezi kuulizwa swali hili kwenye simu. Alipotakiwa kufuatwa ofisini ili kutoa ufafanuzi, Waziri Ndundu alikuja juu na kusema yuko jimboni, hivyo waulizwe wasaidizi wake walioko Dar es Salaam. “Mimi niko jimboni, pale ofisini kuna watendaji wa wizara. Mimi siyo wizara, nenda pale utapata majibu yote,” alisema Waziri Ndundu

Hivi hili gazeti halina MHARIRI ama ndio yaleyale ya watendaji waliojaa serikalini tunaolalamikia kila kukichwa. Lakini zaidi hili ndio gazeti linalopigania ajenda za uwajibikaji, serikali makini na maadili??? Mmiliki angeonyesha mfano wa uongozi makini kwa kumuwajibisha mhusika wa kosa hili.....

Lakini pia inashangaza kuona wale ambao walipinga kununuliwa kwa ndege hiyo (mimi nilipinga bei ya manunuzi hayo huku nikiamini katika umuhimu wa Rais kuwa na ndege ya uhakika) na hata kudai kuwa endapo mgombea wao angeshinda Urais wangeliuza ndege hiyo na kuwa Rais anapaswa kutumia ndege za kibiashara sasa wapo mstari wa mbele kuugulia machungu ya kukosekana kwa ndege hii.....Ujanjaujanja bana
 
Hilo dege halina maaana kabisa,lingekuwapo gharama ni kubwa za kusafiri na hilo dege bana; huyu mkweere kama akili zake ziko timam aanze kusafiri na ethiopian airline, tena hukuuu daraja chee, economy!
 
Kitu kimoja Kikwete ameimprove kwenye uongozi wake: Kama alivokuwa Mkapa, amejifunza usugu wa kupuuza maneno ya watu mbalimbali na sasa anafanya yale yaliyo moyoni mwake na washauri wake basi. Siku hizi hata mpige kelele vipi kuhusu safari zake so long as kusafiri nje ni hobby ataenda tu ikibidi hata mle nyasi.
 
kama ulikuwepo mkuu,hawa jamaa wababaishaji kweli,hata shirika la ndege eti wanaandika QATAL,Waziri NDUNDU mara nje ya nchi,afazali nawe umeliona hilo...Ndo matatizo ya copy and paste kaka.
pia hakuna nchi inaitwa Sweeden na Sweden.
 
Back
Top Bottom