Ndege ya Rais yagongwa na Gari la Usalama wa Taifa

angalau imegongwa na gari la usalama wa taifa.......manake ingegongwa na gari nyengine ya airport sijui hii kesi ingekuwa na ukubwa wa kiasi gani
 
Gari la usalama wa Taifa limegonga au limegongeshwa..............(?) subirini kifuatacho kwani injiihii vituko vinapokezana kijiti
 
Mi nadhani hii ni sabortage, wameamua kuigonga ili kuhalalisha ubovu wa ndege hii. Maana kuna maswali mengi kuhusu uimara na usalam wa ndege hii. sasa ili kufunga mjadala jamaa wa usalama wa Taifa wameigonga na mchezo ndo umeishia hapo.
 
na sasa tusubiri gharama za matengenezo yake. Au guarantee zinacover ajali za aina hiyo?
 
Hii, imekaaje tena??? Gari limegonga ndege???Yaani nimeshindwa kuelewa kabisa.
Mimi ndio ilibidi niulze lakn sikupata jibu.......hiyo ndege ilikuwa imepaki wapi? barabarani au kwenye maegesho ya magari au ilikuwa inaaktiza samora avenue?.......yaani utata m2pu
 
Hilo ni changa la macho,
1. TISS wametumwa na serikali wameigongesha uli kesho waseme imekufa kutokana na ajali hiyo.
2. TISS wametumwa waigongeshe ili watu wapate kula, ni ndege yenye gharama ya dollar million 40, hapa tusipokuwa makini tutaambiwa matengenezo inabidi yakafanyike ujerumani na gharama itakuwa dollar million 6, kumbe imechunwa rangi tuu.

Mjinga ndiyo aliwao.
 
Mimi ndio ilibidi niulze lakn sikupata jibu.......hiyo ndege ilikuwa imepaki wapi? barabarani au kwenye maegesho ya magari au ilikuwa inaaktiza samora avenue?.......yaani utata m2pu

Hii inanikumbusha pale mwanza baada ya ndege(mnyama) jina bwana afya kugonga ndege (kifaa cha uchukuzi ).
Hii ndege iliyumba na kutaka kuanguka .Hii ili sound kidogo clear

Lakini hii ndege ya Rais nayo sijui ilikutwa vipi na gari hilo
 
makubwa! madogo yana afadhali........., kuishi kwingi kuona mengi........ukishangaa ya firauni utachoka na ya Musa........should i go on..........?
 
Nina wasiwasi na hiyo fact yako bwana Mkubwa Mushi kwa sababu taarifa zilizopo ni kuwa ndege hii haiwezi kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma. Ilielezwa ilipofika kuwa ina uwezo wa kutua kwenye viwanja vitano tu Tanzania namely; Mwalimu Julius Nyerere (Dar), KIA, Zanzibar, Mtwara na Mwanza.
Huko Dodoma ilifikaje na kutuaje ili kumpa lift Ballali?

Unabisha kwamba Ballali hakupewa lifti na Rais wakati akitokea Dodoma kujieleza kuhusu mambo ya EPA?
Na kauli ya Dr kwamba ndege ilitumika kubeba mizigo ya Ballali unaichukulia vipi?
Kweli wengine mna kazi...Haswa aswa wapita njia.
 
THis can happen only in Tanzania. Ama kweli, hatuishi vituko. Ni gari la usalama tena kutoka Ikulu, ndilo liliigonga hiyo ndege ikiwa imepaki kwenye hangar. Sijui walifuata nini karibu na ndege hiyo ambayo haitumiki
 
THis can happen only in Tanzania. Ama kweli, hatuishi vituko. Ni gari la usalama tena kutoka Ikulu, ndilo liliigonga hiyo ndege ikiwa imepaki kwenye hangar. Sijui walifuata nini karibu na ndege hiyo ambayo haitumiki

Naomba unijibu swali langu la msingi maana naona kuna watu credible ambao hawakubaliani na mimi kuwa alipewa lifti huyo Ballali.
Sasa kwani Rais ana ndege ngapi?
 
Tatizo
Viongozi wetu na sisi waafrika wengi tunamatatizo fulani fulani,Sasa mpaka uje utafute kugongesha ndege na gari ili iwe nini?? huo sio tatizo kweli la IQ?

Kama mimi Rais na Binadamu wa kawaida unatakiwa utoke mbele ya wananchi wako na uwaombe msamaha na uwaambie ukweli nchi imenishinda,sera zangu zimefail na mawazo yangu yamefail.Eiza yakiwa direct kwa mimi kudhani ndivyo sivyo ama kwa indirect yakichangiwa na watumishi walio chini yangu.

Hivyo nitatangaza kuachia ngazi na kutangaza mchakato wa uchaguzi wa kumpata Rais ambaye ataweza ku deliver wananchi watakayo.

IQ ndogo inatokana na
Pamoja yakua una nia njema na wananchi wako Lakini umeshaona kabisa no way out ya kuwasaidia na bado ukang'ang'ania hiyo nafasi tena kwa kucheza usanii hapo ndipo wenzetu wanapotuhoji IQ yetu.
Usanii wa nini ?umeshindwa nyosha mikono juu mapema na utaonekana shujaa na utaheshimika sana kitaifa na kimataifa.
 
kwa sasa ndege ya rais wetu imepaki uwanja wa Mw nyerere terminal one.
kuhusu kufanya kazi au kutokutokufanya hiyo ni issu nyingine kwasababu kila safari anatumi emirates.

Ba ndugu, niliwahi kuwa mmoja wa abiria wa shirika la ndege la Tanzania wakati wa Mkutano wa Sulliavan, duh yaliyojiri KIA inasikitisha, tumefika airport wakati wa kucheck in watu waliokuwa wanaenda Mwanza na Dar kwa ATCL wakaambiwa wa Mwanza wasubiri precision sababu ndege zao zinatumiwa na Rais na kuwa hiyo iliopo inapita Dar kuchukua abiria wanaoelekea J'burg, sijui yaliyojiri kwa abiria wa Mwanza kwani me safari yangu ilikuwa ni ya J'burg nikitokea KIA. Sometime tunawalaumu ATCL kumbe utawala wetu ndio waharibifu.
 
Naomba unijibu swali langu la msingi maana naona kuna watu credible ambao hawakubaliani na mimi kuwa alipewa lifti huyo Ballali.
Sasa kwani Rais ana ndege ngapi?

Hii ndege hapo Dom vp inatua kweli?
 
Ndege imeharibika sehemu nyeti na inalazimika kupelekwa ilikotengenezwa. Serikali ambazo zinamiliki ndege kama hiyo ya Gulfstream 550 ni Argentina, Ujerumani, Ugiriki, Israeli, Singapore, Sweden, Uganda na Marekani. Na watu/kampuni binafsi zipo Saudi Arabia, Uturuki na Marekani.
 
Back
Top Bottom