Ndege ya precision air yatua uwanja wa kimataifa wa songwe mbeya ni safari yake ya kwanza,yapokelewa

Ina maana ndege ya precision kutua Mbeya imekuwa kama ujio wa papa Benedicto kwa wana Mbeya mpaka wakusanyane hivo,inekuwa Mwanza kila ikitua wanakusanyika hivo na kucheza ngoma mbona kazi zingekuwa hazifanyiki,mbona ile ya rais ilitua lakini hatukuona shamrashamra kama za leo

Hiyo ndio ndege ya kwanza ya abiria ..schedule flight Kutua mbeya ni ni formalities kusherekea wakati wa kuzindua routes...hata hapa DAR ndege zikizundua routes ni lazima kuwe na sherehe...
Hataki wana wa mbeya wajimwagee...
 
Dodoma na Iringa lini? Tumechoshwa na Shabiby..!

Kwa Hali ya nchi sasa muda si mrefu mikoa mingi itapata ndege kwa bei nafuu..hasa ushindani utapozidi kuingezeka kwenye route za DAR...mwanza..kili...zanzibar ..Arusha ..Mtwara . Kibiashara maeneo hiyo yana abiria kipindi chote kutokana na utalii,biashara,mazoea ya wenyeji kutumia ndege...,mkoa wa Mtwara umeibuka baada ya wimbi la gas kuwa watumiaji wazuri sana wa ndege...
Hadi sasa mikoa au maeneo yafuatayo yanaweza kuwa na schedule flights iwapo wakazi wa maeneo husika watazoeshwa uhakika wa ndege na unafuu kuondoa Imani kuwa ndege ni gharama ....muda si mrefu wenye mabasi watapata ushindani wa kweli..

DAR
Zanzibar
Pemba
Kili
Arusha
Dodoma
Tabora
Kigoma
Mwanza
Bukoba
Mara
Mwanza
Katavi or rukwa

Mikoa hiyo Ina viwanja venye uwezo wa Kutua ndege za abiria 70 na kuendelea Kama ATR au Focker.....lakini lazima mashirika ya ndege yakubali kuingia entry costs Kama cost of building new needs or demand...hii inaweza kuchukua Zaidi ya miaka hata miwili ya kupata hasara...lakini baada ya hapo itakuwa faida baada ya kuwa na customer base ya kutosha.
 
Sie tuliokuwa tunalazimika kusafiri kwa masaa 10 kufika Mbeya toka Dar tunajua umuhimu wa kuanza rasmi kwa safari hizi Mbeya.



Sie tuliokuwa tunalazimika kutumia USD 290 karibu 415,000 one way kwa kufika Mbeya kwa FlyLink au Auric tunajua umuhimu wa kuanza kwa safari hizi za leo kwa Tsh 165,000.



Wananchi wa Mbeya walisubiri kwa muda mrefu sana kuifikia siku ya leo,wana haki ya kushangilia na sie tulio mbali lakini tutanufaika kwa hili tunafurahi pamoja nao.

Well-done Mr Shirima, Well-done Precision! Karibu sana Mbeya! Enzihizo wakoloni waliita Mbeya “Moon Bay”!
 
Vichekesho hivi.........ndege ya kibiashara inatua watu mnatoka maofisini kwenda kuichezea ngoma?
Wakati Scandinavia ilipoanza safari kwenda mbeya mbona hamkuichezea ngoma pia.

Bado sana - hayo matumizi ya fedha hapo nani amelipia?
Au ndo zile fedha kutangaza maendeleo ya CCM??

BADO SANAAAA!!!
Miafrica tunapenda kufanya mambo ya hovyohovyo tu!

Hii ni nini sasa....
IMG-20130116-WA0034.jpg

acha chuki kwani kuna cent yako imetumika kwenye kusheherekesha? na ina maana hujui umuhimu wa usafiri wa ndege kwenye kurahisisha usafiri kwa wafanyabishara wa mkoa wa Mbeya?
 
Hongera wana Mbeya na hata mikoa jirani watafaidika Rukwa na nchi jirani pia wataunganisha flight kuja Dar au hata Nje ya Tanzania.Hongera Precision
 
Tunataka Fast Jet nao waanze kupeleka ndege zao MBY

Hao hawakawii, wako mbioni. Nadhani huu mwaka hauishi, watakuwa washatangaza dau la Mbeya.

For your info
Uwanja uko wilaya ya Mbeya vijijini. Mwaka juzi na mwaka jana utawala wa Mbeya mjini (Mbeya City Council) walitaka kupanua mji ili eneo la Songwe ulipo uwanja iwe ni sehemu ya jiji la Mbeya. Viongozi wa wilaya ya Mbeya Vijijini waligoma kuafiki wazo hilo la kilaghai, kwa sababu sehemu ya mapato ya uwanja inaingia katika mfuko wa wilaya ya Mbeya vijijini. Uwanja wa ndege pamoja na viwanda vya saruji na nguo ni vyanzo vikubwa vya kipato kwa wilaya hiyo.
Nawapongeza Precision kwa kuanzisha usafiri wa ndege zao kwenda Songwe.
 
tuwaunge mkono precisionair kwani ni shirika la wazawa kuliko fastjet ya wazungu

Kwangu mimi nafuu nipande Air Tanzania kuliko Precision. wazawa ni ATCL.
Na kama giraffe amekufa, basi nitamuendea kasuku, maana unafuu wake ni mara kumi zaidi ya Precision wanyonya pochi.
Ile ni KQ ndogo tu, sema hujui.
 
Jamani mie biashara ya videge vidogo ilikuwa ni issue kwangu. All I can say it "Well Done Precision, MBY here we come":cheer2:
 
acha chuki kwani kuna cent yako imetumika kwenye kusheherekesha? na ina maana hujui umuhimu wa usafiri wa ndege kwenye kurahisisha usafiri kwa wafanyabishara wa mkoa wa Mbeya?
Haahahahahaaa.........
Waambieni wajenge Terminal 3 JNKA, waache porojo.
 
Kwangu mimi nafuu nipande Air Tanzania kuliko Precision. wazawa ni ATCL.
Na kama giraffe amekufa, basi nitamuendea kasuku, maana unafuu wake ni mara kumi zaidi ya Precision wanyonya pochi.
Ile ni KQ ndogo tu, sema hujui.

Mkuu umesema kweli hawa precision ni KQ ndogo, karibuni itakua inamilikiwa na KQ kwa asilimia nyingi za share.... Serikali inatakiwa ikaze buti na AIR TANZANIA!!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom