Mama Mdogo
JF-Expert Member
- Nov 21, 2007
- 2,961
- 2,138
Kwanini unakosa uzalendo na ndege zetu? Kwani viongozi wetu si wanapanda ATCL? Mungu awe nawe katika safari yako.
Ndugu yangu, mbona nina uzalendo mwingi tu, wiki juzi nimesafiri na ATCL toka Dar to Mwanza na siku tatu baadaye kurudi Dar licha ya kwamba mwaka jana waliniudhi walipoteza ndoo yangu ya samaki. Kuhusu viongozi wetu wengi hawapandi zile ATCL ndogondogo, wanapanda Boeing tu. Hata nao mbona huwa wanapanda Precicion ATR 72, wanaipenda utafikiri yao! Hapa nilipo Precision wamenipa room kwenye hotel moja hapa Rock City, dalili ni kuwa leo sitaondoka hapa! Namwamini Mungu, ila ungeshuhudia hiyo hekaheka iliyoipata hiyo ATCL kama huna ujasiri na/au huna majukumu ya kusafiri huko na huku usingependa kusafiri na ndege tena, yaani imeserereka, ikayumba, ikachupa na kusave!!! Jamani wana JF naona nikilala hapa sitasinzia nikiwaza safari ya kesho na ATR 45 or 72. Mbona nina imani kubwa tu, na kesho naamini nafika Dar salama wa salimini. Amen