Ndege ya ATCL Yapata Kizaazaa Mwanza

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Taarifa nilizoskia sasa hivi ni kwamba ndege ya ATCL imeleta kizazaa Mwanza baada ya kuteleza na kuhama katika njia yake ya kutua (runway) wakati ikitua..habari njema ni kwamba hakuna walioumia..tunazidi kufuatilia..

Kutoka Michuzi:

1.JPG


3.JPG


5.JPG


DSC00851.JPG


Picha za setalaiti za ripota wa Globu ya Jamii zikionesha hali halisi ilivyo muda huu katika sehemu ya tukio la uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya Boeing 737 ya ATCL kupata ajali baada ya kutua leo asubuhi

DSC00850.JPG


DSC00853+%282%29.JPG


DSC00849.JPG


Image007.jpg

Ankal Michuzi

picha za ndege Boeing ya ATCL iliyopata ajali
Mwanza leo asubuhi ndo hizi ila nimepiga na simu sababu ni ngumu kwenda kwenye kiwanja
Mdau Eric

(akiwa amekwama airport Mwanza)

HABARI TOKA MWANZA ZINASEMA NDEGE AINA YA BOEING 737 YA ATCL ILIYOKUWA IKITOKEA DAR ASUBUHI HII IMEPATA AJALI NDOGO WAKATI IKITUA KATIKA UWANJA WA MWANZA IKIWA NA ABIRIA 46 HIVI.



HAKUNA ALIYEPATA MADHARA NA
ABIRIA WOTE NA WAFANYAKAZI WAKO SALAMA NA WAMESHAONDOLEWA SEHEMU YA TUKIO.

RIPOTA WA GLOBU YA JAMII ALIE JIJINI MWANZA AMESEMA NDEGE HIYO YENYE NAMBA YA MRUKO TC 100 ILIPATA DHAHAMA HIYO WAKATI ILIPOTUA KWENYE BWAWA KUBWA LA MAJI LILILOTUAMA KWENYE NJIA YA KUTULIA (RUNNAWAY) UWANJANI HAPO KUTOKANA NA MVUA KUBWA INAYONYESHA.

INASEMEKANA MAJI YALIINGIA KWENYE INJINI MOJA AMBAYO IKAZIMIKA NA KUIFANYA NDEGE IACHE NJIA NA KWENDA PEMBENI, BAADA YA KUWA IMEMALIZA UMBALI WA KAMA MITA 1200 TOKA ITUE KWENYE YA UWANJA HUO WENYE UREFU WA MITA 3000. MGUU WA TAIRI LA MBELE ULIKATIKA.

HABARI ZINASEMA UWANJA UMEFUNGWA KWA MUDA, NA KWAMBA KINACHOFANYIKA HIVI SASA NI KUANGALIA NAMNA GANI NDEGE ZINGINE ZITAVYOTUA (DISPLACEMENT) KWANI BOEING HIYO IKO KARIBU KATIKATI YA UWANJA NA MKIA WAKE UNAGALI KWENYE BARABARA YA KUTULIA. HIVYO KAMA NI NDEGE KUBWA ITAKUWA SHIDA KUTUA HAPO HADI ITAPOWEKWA KANDO HIYO BOEING. NDEGE NDOGO ZINAWEZA KUPITA.

 
Ni ile aina ya Boeing 737.
Habari hii nimeisikia Redio One sasa hivi..Watu wa Mwanza tupeni details basi!
 
Taarifa nilizoskia sasa hivi ni kwamba ndege ya ATCL imeanguka mwanza baada ya kuhama katika njia ya kurukia wakati ikitua..habari njema ni kwamba hakuna walioumia..tunazidi kufuatilia..
hiyo ndege ilikuwa inatokea wapi kwenda wapi na iliruka saaa ngapi?
 
Kichwa cha habari ni potofu. Ndege ilikuwa inatua maji yakaingia kwenye injini ikazima na ndege (B737-200) ikaserereka nje ya runway na nose gear ikaharibika. Huko sio kuanguka. Hakuna majeruhi.
 
Ni jambo la kushukuru once haijaua, majanga ya ki utawala tuliyonayo yanatosha yakitokea mengine mbona itakuwa balaa.
 
Kichwa cha habari ni potofu. Ndege ilikuwa inaua maji yakaingia kwenye injini ikazima na ndege (B737-200) ikaserereka nje ya runway na nose gear ikaharibika. Huko sio kuanguka. Hakuna majeruhi.
ilikuwa inaua nini? hiyo runway inamaji? hayo maji yaliingiaje?
 
hiyo ndege ilikuwa inatokea wapi kwenda wapi na iliruka saaa ngapi?
MASWALI MENGINE BANA!

Unaambiwa imeacha njia wakati ikitua Mwanza, still unauliza ikiwa inaenda wapi!

Mambo ya muda pia si muhimu sana kwa sasa..the thing you were supposed to ask is the condition of the pax!...huh!
 
Ni ile iliotuacha Dar wakati sisi tunasubiri ATCL ya kuja Tabora na Kigoma nafikiri. Iliondoka Nusu saa kabla ya hii ya Kigoma, tupeni habari jamani
 
MASWALI MENGINE BANA!

Unaambiwa imeacha njia wakati ikitua Mwanza, still unauliza ikiwa inaenda wapi!

Mambo ya muda pia si muhimu sana kwa sasa..the thing you were supposed to ask is the condition of the pax!...huh!
PJ, unanipa wasiwasi na chanzo cha habari yako!
Ndege ilikuwa inatua MNZ, sawa lakini ilikuwa inatokea wapi? Arusha? Dar? Kigoma? Nairobi?
 
MASWALI MENGINE BANA!

Unaambiwa imeacha njia wakati ikitua Mwanza, still unauliza ikiwa inaenda wapi!

Mambo ya muda pia si muhimu sana kwa sasa..the thing you were supposed to ask is the condition of the pax!...huh!

PJ habari ni za kweli na uwanja umefungwa kwa leo.
 
PJ, unanipa wasiwasi na chanzo cha habari yako!
Ndege ilikuwa inatua MNZ, sawa lakini ilikuwa inatokea wapi? Arusha? Dar? Kigoma? Nairobi?
Sitakujibu kitu!...sick and tired!..i hate childish questions...nimesema wenye details zaidi watuambie, unaniuliza mimi...kweeek!
 
Back
Top Bottom