Ndege? Ndege mpo?

Kuna sehemu inaitwa Mto Mbezi. Ukiitaja harakaharaka inakuwa na maan nyingine. Jaribu kidogo kwa sauti ya chini...
 
Nimekumbuka pale Lugalo kulikuwa na nyumba ilikuwa na mashine ya kusaga iliandikwa kwa maandishi makubwa lakini bila kuacha nafasi kati ya neno inasema"Hapa tunasagananakukoboa" Umeipata hiyo??
 
Nimekumbuka pale Lugalo kulikuwa na nyumba ilikuwa na mashine ya kusaga iliandikwa kwa maandishi makubwa lakini bila kuacha nafasi kati ya neno inasema"Hapa tunasagananakukoboa" Umeipata hiyo??

lugalo ya iringa au dar kweli watu mna vituko sana nimecheka
 
Kuna kituo Mwananyamala-Ubungo kinaitwa Popobawa, Konda anaulizia 'nani Popobawa?', utaskia jitu fasta 'shusha, au mimi apa'.
 
OOh thanx sana wadau yaani nimecheka saana....hadi machozi.

makonda wa arusha wao hupenda kupiga busu kwa nguvu akiashiria dereva asimamishe gari, usiombe uwe kwenye siti karibu yake utadata na hayo mabusu ya kujambisha.
 
  • Thanks
Reactions: mja
Kuna kituo pale Tanga kinaitwa kituo bangi, konda akikaribia utasikia "oya suka acha bangi" kama mgeni imekula kwako.
 
Kwenye basi la kwenda Buguruni likikaribia sokoni pale Blue rose/Sewa au mabasi ya Mwenge yanayopita Sinza yakifika Africa Sana pale Corner bar/Ambiance utasikia nani nyumba ndogo watu wanaitikia mimi.
 
Moshi kuna kituo kinaitwa "kazi".
Konda: "Oyaa abiria, hamna kazi?"
Abiria: Shusha..
Konda: "Dereva, Acha kazi!"

Mkubwa last time nilimwambia konda, "acha kazi"
akanambia kazi hakunaga kituo tena.
 
Hahaha..umenikumbusha konda leo asubuhi tukishuka daladala posta,
Konda: "Wa mwisho anafagia gari..lol!"
 
haha haaa!mmenikumbusha hotel za uswahilini!utasikia!
Muuzaji:nani kuku?
Mteja:mimiii..!
Muuzaji:nani ng'ombe?
Mteja:mimi hapa kaka!


teh teh teh.......................haha......haaaaaa!
muuza:nani mbuzi:
mteja:mimi hapa kaka!......................teh teh teh..............ngileka Ruwa...............
 
gongo la mboto mpoooooooo....kimyaaaah jamani gongo ya moto mpoooooo........abiria tupimieeeeeeeeeeee
 
Akili za makonda ni hovyo sana, pale safari resort karibu na kimara takribani mwezi mmoja uliopita lilidondoka kontena na kupoteza maisha ya watu watatu. Baadhi yao siku hizi utasikia wakipaita \chinjachinja/ au \kontena/
 
dah! hii inanikumbusha iringa wakati tunatoka mjini kwenda tosamaganga, kuna kituo kinaitwa kibwabwa, yaani utasikia konda akianza kupiga debe, IPOGORO, KIBWABWA, MSEKE NJIA PANDA TOSA.......basi mkifika hapo karibia na KIBWABWA, utasikia, KIBWABWA YUPO?
 
sinza makaburini, OYAA MWISHO WA NYODO MPO? hapo MWISHO WA NYODO = MAKABURINI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom