Ndege? Ndege mpo?

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Konda: Ndege? Ndege mpo?
Abiria: Shusha...
Konda: Waache ndege
(Hapa huwa najiuliza wameshushwa raia au ndege?)
Konda: Kipawa?
Abiria: Wote kimya... Konda anachukulia hamna wa kushuka anamwambia
dereva "Ongeza salio mwana"
Konda: Tazara?
Abiria: Kimya pia... Konda anaonekana kujawa hasira... na kutoa maneno
ya chinichini...
Konda: Kwa jazba anasema HUU NDO MWISHO WA 200!
Abiria: Kimya pia
Gari linavuka TAZARA kwenda zaidi... Sasa konda anajua kupakia
ishakuwa nuksi maana abiria hawashuki.
Konda: Abiria hamna ngozi?
Abiria: Kimya...
Mfano mwingine ni kama upo Morogoro Rd...
Konda: Migomigo?...
Abiria: Shusha... (sasa asoelewa maana ya migomigo ameliwa)
Konda: Usalama? Abiria hamna usalama?
Abiria: kimya
Konda: Chai?
Abiria: Shusha...
Kwa kawaida lugha wanayotumia makondakta ni ya wenyeji wa Dar. Wale
wageni hupitilizwa sana kwenye vituo na kubaki kulalama bila msaada.
Ukimwambia abiria 'Abiria hamna chai' usitarajie alotoka Arusha na ni
mara yake ya kwanza kuwa Dar aelewe anatakiwa kushuka kafika Magomeni
Mwembechai.
 
mi sijakufaham....

haha haaa!mmenikumbusha hotel za uswahilini!utasikia!
Muuzaji:nani kuku?
Mteja:mimiii..!
Muuzaji:nani ng'ombe?
Mteja:mimi hapa kaka!
 
rolling on the floor laughing loud.....nimecheka sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa jf kuna mambo!
 
  • Thanks
Reactions: mja
wengine utasikia kula vichwa,
au mchawi anakuja...akimaanisha kuna gari jingine linabeba abiria kuelekea wanakoenda wao
 
Some days natoka cnza tumefika kwa Remi konda akaita: Kwa marehemu?
Tulipofika makabulini nikasikia konda anauliza tena: alipozikwa marehemu?
 
Some days natoka cnza tumefika kwa Remi konda akaita: Kwa marehemu?
Tulipofika makabulini nikasikia konda anauliza tena: alipozikwa marehemu?
hahaaaaaaaaaaaaaaaaah duh jina la sinza kwa Remmy linapotea sasa
 
Ahahahahaaah! Kweli sisi wa huku Kavifuti tukija huko Dar inabidi tusicheze mbali na wenyeji wetu ili tusipotee!!
 
Kuna kingine, Mbezi beach pale.
Jogoo!! Utasikia Kuku dume!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom