Ndege Kuwa rahisi kama dala dala

Unaposema hivyo; hivi umezingatia kipato cha wengi ambao hawajapanda ndege kikoje???? Kama hiyo ya Dar -Mz (return) Tshs 190,000/- unadhanini WALALA HOI wangapi (ambao hadi leo wanagombania 3rd class ya TRC kwenda na kurudi makwao) wanaweza kuunguza hicho kiasi USEMACHO NI KIDOGO SANA kwenda safari hiyo??Usiusemee moyo wa mwenzako au mfuko wake Sheikh!!! Mtaani hali kiuchumi ni mbaya kuliko udhaniavyo.....
 
daladala zina bus stop nyingi tu along the road, natumaini ndege pia wataweka plane stop kibao angani
 
Hivi kuna ndege yoyote inayofanya safari zake Dar - Dodoma au Dodoma - Mwanza?
 
Ha ha haa! ni vizuri kuishi kwa matumaini. Ndege ztaendelea kuwa ghali tu. Unaweza kusafiRI kwa bei cheap, lakin viwanja vingi viko mbali na miji, ambapo ukishuka kwny ndege unatakiwa kchukua taxi kwa wastan wa tshs 25K. Bado ni ishu kwa wengi.
 
what?? unalinganisha wapi na wapi? domestic flights za tz bado ni juu mno ukilinganisha na kipato cha wananchi
 
Hutakiwi kujisifu hata siku moja. Hapo airport JNIA ukienda hakuna hata ndege moja ya Tanzania zimejaa ndege za kutoka nchi za wenzetu sisi tumebaki kumiliki kiwanja tu. Tulikua na kibajaji kimoja kilikua kinaenda Kigoma na Mwanza kwa sasa hakipo tena. Aibu kweli yaani unaenda uwanjani unazikuta hadi Air Burundi wakati wao kila siku walikua wanapigana sie na amani yetu tumebaki na viwanja tu. Ni sawa na kua na mke harafu ukamweka rehani kwa watu wawe wanakugongea tu wewe unabaki jina kua una mke
 
Mkuu hujamsikia yule bwana mkubwa Mattaka wakati wa kustaafu? alisema yeye pale ATC hata kama sasa hakuna ndege,anajivunia kubadili nembo ya ATC. Hao ndio tunaowapa kuongoza mashirika yetu. Na kwa mtindo huo miaka kadhaa ijayo sijui hali itakuwaje.
 
Hivi kuna ndege yoyote inayofanya safari zake Dar - Dodoma au Dodoma - Mwanza?
na hii ni challenge nyingine, miaka 50 ya uhuru ni mpaka kukodisha ndege ili ufike baadhi ya maeneo, ni akina nani hao wa kukodisha hizo ndege ...au shirika lianzishwe likisubiri "Boys II Men" wakiendea forms za kugombea ulaji ndio wapate wateja!?
 
Unajua kua Nauli ya ndege kutoka Kigoma kwenda mwanza Return tiket ni sh 630,000/=? Zaidi ya wafanyakazi wa UN unategemea nani atapanda hiyo ndege. Nauli ya Kutoka Kigoma-Mwanza ni sawa na nauli ya Dubai
Hiyo nauli ni mshahara wa miezi sita kima cha chini!
 
Back
Top Bottom