Ndalichako: Wanaodaiwa na HESLB tutaweka majina yao magazetini kuwashinikiza kulipa

Ni bora tulipe kabla hatujadhalilika isitoshe unapolipa unatoa fulsa kwa wanao na ndugu zako nao kupata elimu ya mkopo pia unafungua milango ya baraka.
 
Waziri wa elimu Joyce Ndalichako amesema wana mpango wa kuweka majina ya wadaiwa na bodi ya mikopo kwenye magazeti ili kuwashinikiza walipe, amewaasa wadaiwa wakiwapo wabunge walipe ili majina yao yasiwekwe.


Hilo ni wazo zuri, tatizo Watanzania hatuna uzalendo na nchi yetu mtu amemaliza kusoma na kazi amepata lakini hataki kulipa anajiunga na wasiopata kazi akijifanya naye hajapata kazi.Dawa ni hiyo hiyo, maanake wakati tunasoma tulikuwa kelo sana kwa serikali mkopo ukichelewa tu tunaandamana au tunagoma kuingia madarasani mpaka serikali ituingizie boom, hongela mama Ndalichako kama alivyosema Rais nchi hii bila kwata hatuendi.
 
Hata waki bold jina langu kwa red kazi bureee,sio kama sitaki kulipa bali sina cha kuwalipa, wangenipa kazi ningewalipa bt kwa hivi wanajisumbua sana sana watanipa kick nami nionekane kama wale wanaodaiwa na sirikali..
 
Wao nao mbona walisomeshwa na serikali na hawaanzi kulipa ndio wawaadai vijana ambao hawana ajira.
 
Ndalichako Mama, deni lako tunalikumbuka ila jinsi ya kukulipa ndo shida tunatoa wapi sasa?? ushauri wa bure samehe madeni yote tuanze Moja
 
tatizo sio kushindwa watu wapo tayari kulipa lkn bodi inashindwa kuweka mechanism nzuri ya kuwafikia.. halafu wakati mwingine mtu unalipa mkopo mpaka unaisha lkn ukihama kazi na kwenda ofisi nyingine unakuta rekodi zako zinaonyesha unadaiwa deni lile lile.. hiyo bodi ijipange kwanza kabla ya kuanza kuwadhalilisha watu magazetini.. mi nishamaliza deni lkn nishahawahi kutangazwa kama mdaiwa sugu na kunisababishia usumbufu mkubwa.. nilipowauliza wakaniomba msamaha na kusema hawatarudia tena lkn wakarudia tena.. sasa hivi wakinitangaza tena sikubali lazima niwashitaki
Walikutangazaje mkuu mbona sisi hawatutangazi?
 
Waziri wa elimu Joyce Ndalichako amesema wana mpango wa kuweka majina ya wadaiwa na bodi ya mikopo kwenye magazeti ili kuwashinikiza walipe, amewaasa wadaiwa wakiwapo wabunge walipe ili majina yao yasiwekwe.


Waziri kabla ujatoa majina fatilia kwanza nani na nni Wako kazini,ila ukitoa jina la mtu hana kazi toka kamaliza masomo ni kudhalilisha kwenye magazeti.Mpatie ajila alafu mpe mda alaafu anza kumdai.
 
tatizo sio kushindwa watu wapo tayari kulipa lkn bodi iikibidiashindwa kuweka mechanism nzuri ya kuwafikia.. halafu wakati mwingine mtu unalipa mkopo mpaka unaisha lkn ukihama kazi na kwenda ofisi nyingine unakuta rekodi zako zinaonyesha unadaiwa deni lile lile.. hiyo bodi ijipange kwanza kabla ya kuanza kuwadhalilisha watu magazetini.. mi nishamaliza deni lkn nishahawahi kutangazwa kama mdaiwa sugu na kunisababishia usumbufu mkubwa.. nilipowauliza wakaniomba msamaha na kusema hawatarudia tena lkn wakarudia tena.. sasa hivi wakinitangaza tena sikubali lazima niwashitaki
Wenye kilio kama chako tupo japokuwa si wengi ki hivyo. La msingi tuwe na tabia ya kulipa madeni yetu bila shuruti.
 
Mkopo wenyewe wameuwekea riba, inayoitwa Retention fee kitu ambacho hakikuwepo kwenye mkataba wao wa awali.

Wezi wezi tu hawa
 
Unaweka majina ya nni?
Kwenye ualimu walidai kuna grant na mkopo. Grant hatukutakiwa kurejeshs ila sasa tunarejesha zote na retation fee.
Isitoshe ilitakiwa walau wanaofanya kazi kwenye public sector wangepewa hata robo ya msamaga wa mkopo kama motivation. Cha ajabu unaajiriwa na govt. msalary njiwa na bado wanakata mule mule sawa na wale wanaotumikia private sector wenye mishahara mikubwa na kwa faida ya bwana kheri.
Hvi vitu tunaomba vifanyiwe marekebisho lkn hamna lolote.


Ndiyo shida ya Watanzania. Ni shida dunia nzima na tunafahamika hivi. Umepokea mkopo unatakiwa kwenda kulipa. Suala la ajira haliwemo kwenye makubaliano ya mkopo uliopewa. Tuone sasa kama hamtalipa!
 
Hahaha nimemkimbuka mdegela na mkiza ghafla
Ndelichako akome, mimi niliomba kazi ya kudai madeni pale Bodi ya mkopo, ila nilinyimwa nafasi, kisa sina ndugu pale, sasa sina ajira unategemea ntalipaje mkopo, nipe ajira uone kama ntakwepa?
 
Hahaha nimemkimbuka mdegela na mkiza ghafla
daaa, jichek akili mkuu, unakumbuka mbwea hao? mtu km mdegera unamkumbuka ili iweje? mi hata nikikutana nae, huwa najifanya simmkumbuki hata kama idea ikinijia, kuna siku nilimwagia maji machafu, alikuwa karibu na dimbwi mi napita uku badrive, nililazimika kuingia dimbwini ili nimuogeshe.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom